Dunia Adonis afariki dunia

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Posted Date::11/12/2007
Mchezaji wa zamani Yanga afariki dunia Arusha
Na Mwandishi Wetu
Mwananchi

KAIMU Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Arusha (ARFA), Dunia Adonis, amefariki dunia jana.

Habari zilizopatikana kutoka Arusha na kuthibitishwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zinasema kuwa Adonis ambaye alikuwa pia ni mjumbe wa shirikisho hilo, Mkoa wa Arusha alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya figo.

Akizungumza na Mwananchi, Katibu Mkuu wa TFF, Frederick Mwakalebela alisema Dunia anatayarija kuzikwa leo mkoani Arusha.

Alisema shirikisho lake limesikitishwa sana na kifo hicho cha mchezaji huyo wa zamani wa Yanga na kwamba linatoa ubani wa Shilingi 100,000 kwa wafiwa.

"Tumepoteza mtu muhimu sana katika maendeleo ya soka mkoa wa Arusha, Dunia alijituma, alijitolea kwa hali na mali kuhakikisha soka la mkoa wake linakuwa,"alisema Mwakalebela.

Aliongeza: "Pengo lake halitazibika kamwe na tutamkumbuka kwa mengi."

Kwa mujibu wa Mwakalebela, Dunia ambaye alikuwa pia kiongozi wa klabu ya AFC ya Arusha ameacha mke na watoto kadhaa.
 
Back
Top Bottom