Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 39,840
- 92,403
Herehoa!
Leo nimeiangalia hii mechi ya hawa mabondia waliozoea kutambiana, nimefurahi kuona sijapoteza usingizi wangu bure.
Pambano lilikuwa zuri Sana. Waandaaaji walijipanga kufanikisha hili, hivyo nawapongeza Sana.
Lakini Kwa vile Mimi nami naishi Mkoa wa Morogoro Kwa kweli najisikia furaha Kwa USHINDI wa Twaha Kiduku ambaye amemtwanga Dulla.
Sasa hakuna ubishi tena kuwa Kati ya Twaha Kiduku na Dulla mbabe Nani kidume Kwa mwenzake.
Kitu pekee nilichojifunza kwenye Pambano hili kutoka Kwa Twaha Kiduku ni Kama ifuatavyo;
1. Usiwe mjivuni.
Twaha Kiduku, sio mjivuni, ninamfahamu Kwa kumuona, na Kwa vile Maeneo anayofanyia mazoezi ni karibu na ofisi yangu, ninaweza Kueleza hili pasipo shida.
Twaha Hana ujivuni, hajisikii na yupo simple Sana.
Hiyo ni akiwa huku kitaa.
Kwa upande wa akiwa ulingoni pia Twaha sio mtu wa ujivuni. Hana mbwembwe, Hana sifa Kama Sisi kina Taikon tunapenda misifa.
Kwenye mechi hii Kwa walioangalia wataungana na Mimi kuwa Twaha tangu anaingia kwenye ukumbi Hana ujivuni, tofauti na Dulla ambaye anapenda mbwembwe na mikwala.
Hii inatufundisha kuwa ajishushaye hukwezwa, ajikwezaye hushushwa.
2. Sio muoga.
Unajua watu wengi hutishwa na mikwala ya Adui zao. Dulla mbabe licha ya mikwala yake isiyoisha, mbwembwe za kuingia ulingoni, na sapoti kubwa aliyonayo bado haikumfanya Twaha amuogope.
Unajua Kwa mtu muoga ni rahisi kutishwa na mambo madogo Kama hayo.
Mechi ya leo inatufundisha kuwa tusitishwe na maneno ya Adui yetu.
3. Ufanisi na Weledi
Twaha kapigana Kwa weledi mkubwa Sana.
Kashambulia kuanzia raundi ya pili mpaka ya mwisho Kwa ufanisi wa Hali ya juu.
Twaha alitumia mbinu ya kushambulia zaidi pasipo kumpa nafasi Dulla mbabe,
Ingawaje raundi ya Kwanza Dulla
akiishambulia zaidi, alimpigaa Jab,/Ngumi Jinni ambayo ilimpeleka chini Twaha na ilibaki kidogo mchezo uishie pale na kuwa TKO.
Kwa Pambano hili, wote walioangalia wataungana na Mimi kuwa Dulla hamuwezi Twaha Kiduku, yaani kampiga Kama mtoto mdogo. Licha ya Dulla kujifanya anafurukuta.
Kesho wanamorogoro tutaandamana kuanzia Mikese mpaka Morogoro mjini, tukiwa na Crown yetu.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Morogoro.
Lala bana kijana wa Makanya
Yule mpembavu katutia aibu sisi wanaume wa dar,leo gari limeondoka ipo siku hata wakezetu wataondoka kwa stahili hii[emoji24][emoji24]
Dula ana mikwara mingi ila Hana uwezo [emoji4][emoji4][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Nimeng'atwa na mbuzi.
Baba sasa ndio kumekucha.
Dullar hawezi mkono..hata mimi nikisimama nae namkalisha vizuri tu.
Nimeng'atwa na mbuzi.
Baba sasa ndio kumekucha.
Huyu kijana wa Morogoro aliyeshinda hivj wamewahi pigana na yule kijana wa Tanga?
Hapo nimekupata Mkuu.Kijana wa Tanga anaogopa,
Anajishaua,nafikiri anaogopa kupasuka.
Mwakinyo ni mzuri lakini sio Kwa kiasi cha kumshinda Twaha Kiduku.
Bahati mbaya sana umechambua Kimahaba na siyo Kiutaalam / Kiufundi zaidi.Herehoa!
Leo nimeiangalia hii mechi ya hawa mabondia waliozoea kutambiana, nimefurahi kuona sijapoteza usingizi wangu bure.
Pambano lilikuwa zuri Sana. Waandaaaji walijipanga kufanikisha hili, hivyo nawapongeza Sana.
Lakini Kwa vile Mimi nami naishi Mkoa wa Morogoro Kwa kweli najisikia furaha Kwa USHINDI wa Twaha Kiduku ambaye amemtwanga Dulla.
Sasa hakuna ubishi tena kuwa Kati ya Twaha Kiduku na Dulla mbabe Nani kidume Kwa mwenzake.
Kitu pekee nilichojifunza kwenye Pambano hili kutoka Kwa Twaha Kiduku ni Kama ifuatavyo;
1. Usiwe mjivuni.
Twaha Kiduku, sio mjivuni, ninamfahamu Kwa kumuona, na Kwa vile Maeneo anayofanyia mazoezi ni karibu na ofisi yangu, ninaweza Kueleza hili pasipo shida.
Twaha Hana ujivuni, hajisikii na yupo simple Sana.
Hiyo ni akiwa huku kitaa.
Kwa upande wa akiwa ulingoni pia Twaha sio mtu wa ujivuni. Hana mbwembwe, Hana sifa Kama Sisi kina Taikon tunapenda misifa.
Kwenye mechi hii Kwa walioangalia wataungana na Mimi kuwa Twaha tangu anaingia kwenye ukumbi Hana ujivuni, tofauti na Dulla ambaye anapenda mbwembwe na mikwala.
Hii inatufundisha kuwa ajishushaye hukwezwa, ajikwezaye hushushwa.
2. Sio muoga.
Unajua watu wengi hutishwa na mikwala ya Adui zao. Dulla mbabe licha ya mikwala yake isiyoisha, mbwembwe za kuingia ulingoni, na sapoti kubwa aliyonayo bado haikumfanya Twaha amuogope.
Unajua Kwa mtu muoga ni rahisi kutishwa na mambo madogo Kama hayo.
Mechi ya leo inatufundisha kuwa tusitishwe na maneno ya Adui yetu.
3. Ufanisi na Weledi
Twaha kapigana Kwa weledi mkubwa Sana.
Kashambulia kuanzia raundi ya pili mpaka ya mwisho Kwa ufanisi wa Hali ya juu.
Twaha alitumia mbinu ya kushambulia zaidi pasipo kumpa nafasi Dulla mbabe,
Ingawaje raundi ya Kwanza Dulla
akiishambulia zaidi, alimpigaa Jab,/Ngumi Jinni ambayo ilimpeleka chini Twaha na ilibaki kidogo mchezo uishie pale na kuwa TKO.
Kwa Pambano hili, wote walioangalia wataungana na Mimi kuwa Dulla hamuwezi Twaha Kiduku, yaani kampiga Kama mtoto mdogo. Licha ya Dulla kujifanya anafurukuta.
Kesho wanamorogoro tutaandamana kuanzia Mikese mpaka Morogoro mjini, tukiwa na Crown yetu.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Morogoro.
Bahati mbaya sana umechambua Kimahaba na siyo Kiutaalam / Kiufundi zaidi.
Kuna Bondia hapa umemtaja kuwa ni Mjivuni mbona nawe pia unaonekana ni Mjivuni na Mbinafsi?
Je, ikitokea wakarudiana na Dulla akaibuka Mshindi utakuja kusemaje labda hapa Kwetu Great Thinkers?
Hapo nimekupata Mkuu.
Pigo Kwa wanaume wa Dar.
Wanaume wa Dar wanamikwara sio tu kwa Mabondia kuna kipindi kulikuwa na Bifu kati ya NAKO 2 NAKO vs wale watoto wa Kinondoni wale watoto wa Kino walikua na Mikwara sana lkn Jukwaani sifuri