Duka la Dawa Muhimu za Binadamu (Pharmacy): Utaratibu wa Kufuata na Mtaji wa Kuanzisha Biashara

Ndugu yangu, naomba na mimi nikupe mwanga zaidi kwa faida ya wengine.

Kama baadhi walivyosema, kutokana na mabadiliko ya sheria, Tanzania kwa sasa hakuna maduka ya dawa baridi. Tuna maduka ya dawa muhimu (DLDM). Maduka haya yameanzishwa kutokana na utafiti uliofanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) mwaka 2001, na kubainisha mapungufu mengi ambayo yalikuwa yanafanywa katika maduka ya dawa baridi (DLDB). Mojawapo ni kuuza dawa zisizoruhusiwa kisheria kwa kutumia watoa dawa wasio na sifa; kugeuza maduka kuwa maabara na dispensaries na kadhalika.

Kwa ufupi tu, kutokana na hali hiyo, na kwa kuwa Tanzania ilikuwa ina huduma duni ya dawa kwa wananchi walio wengi, (ambao wanapatikana na vijijini na miji midogo), serikali ikaamua kuanzisha mpango wa DLDM kwa lengo la kuondoa matatizo yote yaliyobainishwa kwa utafiti. Pili ilikuwa kuruhusu dawa chache za msingi (few essential medicines) ziwepo kwenye maduka hayo, na watoa dawa wake wapate mafunzo maalumu, ili huduma ziwe bora na za uhakika katika maeneo ya rural, periurban na maeneo maalum yaliyoruhusiwa ambayo hakuna duka la Famasi.


Ili kuweza kuhakikisha haya, ngazi zote za utendaji, yaani ngazi ya kijiji au mtaa, ngazi ya kata, ngazi ya wilaya na mkoa wanahusishwa moja kwa moja katika utekelezaji wa mpango huu.


Sasa utaratibu ni huu:
1. Chukua fomu ya kuanzisha fomu ya kuanzisha DLDM kwa mfamasia wa wilaya unayotaka kufungua duka. Ijaze sehemu A, ukiwa umeambatanisha vyeti vya kuhitimu mafunzo maalumu yaani mmiliki na mtoa dawa, mkataba wa kazi baina ya mmiliki na mtoa dawa, pia commitment letter ya mtoa dawa katika duka hilo. Kama wewe ni mmiliki na pia ni mtoa dawa, huna haja ya kukusanya mkataba huo.
2. Fomu ipeleke ofisi ya kijiji au mtaa ambao duka litakuwepo. Wao watajaza sehemu B.
3. Fomu itapelekwa kwa ofisi ya Kata, watajaza sehemu C. Wakaguzi zaidi ya mmoja watakuja kufanya ukaguzi wa eneo na jengo kama linakidhi vigezo.
4. Fomu itapelekwa ngazi ya wilaya, na kabla hawajajaza sehemu D, watatakiwa kufanya ukaguzi tena kwenye eneo na jengo lako, na kuhakikisha mtoa dawa wako amepatiwa mafunzo. Kama kuna marekebisho utaelezwa na uyafanyie kazi. Lakini kwa kupitia kamati yao ya Chakula na Dawa inayoongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri au Manispaa, itakaa kikao na kuyapitia taarifa za ngazi zote, na za ukaguzi. Maduka yaliyokidhi vigezo, yanapendekezwa sasa kwenda Baraza la Famasi (Pharmacy Council) waweze kutoa vibali. Ukishapata kibali unatakiwa urudi tena kwenye halmashauri au wilayani ukapate Leseni ya Biashara.

Nahisi nimekupa mwanga kidogo zaidi, ila kama ningekuwa na email yako, ningekutumia Kitabu cha mwongozo kinachosimamia mpango huu.

Thank you
Mwananchi mwenzenu.
Ndugu Silumbe naomba unitumie huo mwongozo nami nataka kuwekeza kwenye biashara hii
Email: kivikes@yahoo.com
 
Wakuu nina maswali kadhaa kuhusu hii biashara.
  1. Je, ninahitaji vibali gani? Na vinapatikana katika ofisi zipi na pia itakuwa msaada sana kama itawezekana kuweka gharama zinazolipwa kwa kila kibali.
  2. Je, mtaji kiasi unatosha kufungua biashara hii.
Natanguliza shukrani zangu.

--------
Naamini ulipata mwanga juu ya hii biashara ndugu.............. nipe mwanga namimi
 
Kwanza kabisa tafuta mtu mwenye cheti cha ADO (ulizia pharmacy body ADO ni nini) We mmiliki uwe na cheti cha mmiliki (uliza pharmacy body) Ukishamaliza hayo tafuta sehemu duka muhimu linaruhusiwa (pharmacy body) Tafuta fremu inayolingana na vigezo vya pharmacy body. Mtaji unajikuna mwenyewe sio chini ya m 4

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza kabisa tafuta mtu mwenye cheti cha ADO (ulizia pharmacy body ADO ni nini) We mmiliki uwe na cheti cha mmiliki (uliza pharmacy body) Ukishamaliza hayo tafuta sehemu duka muhimu linaruhusiwa (pharmacy body) Tafuta fremu inayolingana na vigezo vya pharmacy body. Mtaji unajikuna mwenyewe sio chini ya m 4

Sent using Jamii Forums mobile app
Ok mkuu nitafanya hivo mmiiliki lazima awe medical pesonnnel???? na kama ni medical personel ni wa kada ip sana ktk medicine humo humo?
 
Ndugu wadau wa mtandao huu nawasalimu,
Awali ya yote poleni na majukumu, pili hongereni kuwa na kazi maana wengi hulaumu kwa kukosa ajira na kazi kwa ujumla,

Kifupi, nawaombeni maelekezo kuhusu maduka ya dawa mhimu,process za kufungu na gharama zake, Lakini pia ningependa kujua vitu gani vinaruhusiwa kuchanga humo kama biashara, Tatu ningependa kujua sifa na vigezo vya kulangua viwandani na viwanda hivyo ni vipi na vikobwapi,


Asanteni kwa mchango wenu!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo lazima,maana kuna umiliki ambao unaweza ukamili ndege japo we hujui hata kuiendesha,


Ila nashukuru kwa ushauli,nataraji kwenda kuongeza elimu kuhusu taaruma hiyo japo kwa kiasi tayari ninayo,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu wadau wa mtandao huu nawasalimu,
Awali ya yote poleni na majukumu, pili hongereni kuwa na kazi maana wengi hulaumu kwa kukosa ajira na kazi kwa ujumla,

Kifupi, nawaombeni maelekezo kuhusu maduka ya dawa mhimu,process za kufungu na gharama zake, Lakini pia ningependa kujua vitu gani vinaruhusiwa kuchanga humo kama biashara, Tatu ningependa kujua sifa na vigezo vya kulangua viwandani na viwanda hivyo ni vipi na vikobwapi,


Asanteni kwa mchango wenu!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kachukue form ya kuomba kufungua duka la dawa(duka la dawa muhimu) au pharmacy kwa Mganga mkuu wa Wilaya.Mengine yanajieleza kwenye form.
 
Salaam waungwana,

Nmeona changamoto ya kupata matibabu wanayopata watu wa eneo fulani nje kidogo ya jiji (Dar es salaam) kwani zahanati ipo mbali kidogo nikafanya kautafiti na kuona kama nitatoa huduma ya kuuza dawa muhimu ktk eneo hilo nitawasaidia wananchi hao kutokana na adha ya kupata dawa hzo muhimu na mimi nitapata Rizki pia.

Mtaji upo kama M4 hivi nafkiri kwa kuwa ni nje ya mji mtaji huu nadhani utatosha kuanzia.

Hivyo naomba mwenye kujua UTARATIBU na VIGEZO vya kufungua Duka la Dawa anifahamishe naimani atakua amenisogeza hatua fulani mbele pia atawasaidia wengi wenye lengo kama hili.

Ahsante
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom