Nyakwec's Bro
JF-Expert Member
- Apr 27, 2012
- 820
- 174
Jamani nataka kutoa heshima kwa jamaa amepita hapa mbele yangu nikajikuta ninamkodorea macho hadi anatokomea,jamaa amebeba ndoo kichwani sinashaka inamaji au mafuta halafu amepanda kibaskeli cha tairi moja speed 120,nimeshangazwa jinsi anavyokwepa mabonde njia zetu za uswahilini utapenda,mambo hayo huwa ninayaona kwenye runinga tu leo nimeshuhudia live bila chenga.
Mambo haya ni vipaji au mazoezi tu na mimi nikifanya miezi miwili hivi ninaweza kujua?wazoefu tujuzane!..
Kuna mambo mengine usipojifunza utotoni,ukubwani utakuwa unatafuta ulemavu tu...
fanya zoezi la kuchemsha mawe ukiona umefanikiwa kuyaivisha basi hamia kwenye hilo la huyo jamaa
pumzi inatafutwa wapi mkuu?...katafute pumzi kwanza....
huu sasa ni uuaji kaka .Ni zoezi rahisi tu hilo.Anza kujifunza kwenye mitelemko mikali yenye mawe mawe,ndani ya siku tatu unakuwa mwalimu.
pumzi inatafutwa wapi mkuu?...
kama swimming na kuendesha baiskeli.Kuna mambo mengine usipojifunza utotoni,ukubwani utakuwa unatafuta ulemavu tu...