Duh,Ugeni wa ghafla

Duh,sikia mwanangu alivyoniambia: Baba nimetumwa na wanao wote nije kukwambia kitu muhimu sana na ninekuja na mme wangu ili kuweka uzito wa jambo lenyewe.Baba umetembea sana duniani,baba umezaa watoto wengi kila nchi,baba una historia ndefu sana na iliyo na kila aina aina ya mikasa.Baba mimi umenizaa na mkeo ambae sio mtanzania lakini umenipa heshima ya kiongozi wa ukoo wako,na zaidi ya hilo umenipa haki ya kuishi kwenye nyumba ya baba yako ujerumani na ndugu zangu wote wamekubali.
Baba unazeeka sasa,hatujui huenda Mungu akakuchukua,sasa kabla hilo halijatokea tunakuomba uandike historia ya ukoo wako Hiyo historia ndio itakuwa dira ya ukoo.Nimetumwa kuja kukuambia maana umri unakwenda hivi sasa,huenda Mola akakuchukua soon.Tutendee haki kwa kutuandikia historia yako.Baba hilo ndio lililonileta hapa Mwanza mimi na mme wangu.Baba unajua mie sio mtanzania na baba ulinifundisha kiswahili leo nakusemesha kiswahili nikiwa na mme wangu.Baba niko chini ya miguu yako,tuandikie historia yako kabla hujafa
 
afadhali umenisaidia kumjibu jamaa
 
Wiki ijayo baada ya sikukuu ya Pasaka kumalizika,mimi binti yangu na mumewe tutasafiri kuelekea alikozaliwa marehemu mama yangu,ambako tutakaa siku 2 na kurejea Mwanza,na baada ya hapo wageni hawa watarejea kwao.
 
Ugeni kwetu ni baraka isitoshe umeshasema mgeni wakondio anakuhudumia huduma muhimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…