Kuhusu hili la kununua gari kuna siri nyingi tu, kuna magari utaona yanauzwa rahisi na ni matoleo ya miaka ya karibuni kuanzia 2005 na kwa bodi utayaona yanapendeza lakini kumbe mengine yalipata ajali na kuwa right - off huko yalikotoka ama yameenda miles/km nyingi lakini yamefanyiwa maujanja wa clocking- (kurudisha speedometer)
Popote utaponunua ni muhimu sana jaribu kuomba full service history book na original registration book, hapo utaelewa ukweli kuhusu hiko chombo.
Mimi personal opinion yangu ni kwamba kuana grade 3 ambapo Grade 1, UK made, kwa sababu ya manufacture standard UK wana viwango vyao kwa kila gari na wanamlazimisha manufacture atimize viwango, kiusalama na umadhubuti viwango vyao viko juu ukilinganisha na Japan, mfano Rav 4 ya Japan na ile ya UK, ingawa ya Japan itakuwa na vikorombwezo (luxuries) zaidi (DVDs, navigation etc) lakini ya UK itakuwa na extra safety features,
Grade 2 ni Japan kwa sababu anagalau waweza pata history book ya kuiamini kidogo ingawa jamaa zetu wa Kipopo wamekuwa wanafoji, jitahidi kununua kwenye makumpuni ya kueleweka na sio wale ma-agenti wababaishaji.
Grade 3 ni Dubai huku kwa kweli ni kubahatisha, unaweza kupata gari kama inavosema kwenye registration book ama ukapata gari bodi tu, miezi 6 spana mkononi.
Mwisho kama unanunua huku kwetu Tanzania hapo ni akili na macho ndio muamuzi, unaweza kutafuta fundi unayemuamini ili akusaidie kukagua.