SoC03 Duara Jeusi kwenye Bahari Nyeupe

Stories of Change - 2023 Competition
May 4, 2023
9
20
Hakuna kitu kikubwa kwenye hii dunia kama maendeleo kwenye jamii, hakuna furaha inayopatikana kwenye jamii kama ya uhakika wa kesho, hakuna furaha zaidi inayopatkana kwenye jamii kama ile ya kufahamu usalama binafsi na tunaowapenda, kuanzia familia, jamaa na marafiki na mpaka taifa kwa ujumla.

Usalama na uhakika wa maisha uliopo kwenye mikono ya watu sawia walioahidi kumshika mkono raia yeyote mwenye utaifa wa nchi.

maisha halisi yanahusisha nyanja zote (siasa, uchumi, masuala ya kijamii, sayansi na teknolojia). Haihitajiki maisha halisi ya mtu yeyote yawe kwenye asilimia zote. Ila kuna nyanja ambazo lazima ziwe na asilimia mia ili kuweka tija ya jamii.

Midomo ya walioaminiwa kupewa viti na kuwazungumzia walio chini na wasio na nafasi yeyote kwenye mfumo, midomo yao imekuwa mikubwa kuvunja maisha halisi yanayotakiwa hata kwa asilimia chache. Sio siasa pekee, bali wote walioko kwenye nafasi ya mfumo fulani. Maslah ya mtu wa chini yanazidi kudidimia na kubanwa kias kwamba hamna namna ya kushika pengine kuona mwanga. Hatuwezi kufika safarI ya mafanikio kamwe.

Mashirika anzishwaji yana midomo mikubwa kwa kuhitaji zaidi ukubwa wa mifuko yao kutuna. Huku mmong'onyoko wa maadili ukiendelea kuitafuna jamii yetu. Dunia ya Upinde wa rangi imekuwa ikimeza mataifa mengi yaliopendeza kwa maadili. Huku na sisi tukiruhusu mashirika mengi kuanzishwa bila kuzuwia na wanaofanya usajili hawafatilii utendaji wa mashirika hayo, leo yamefungiwa kadhaa, je wakati yanaanzishwa nani aliruhusu huu uozo uingie kwenye jamii? Nani alaumiwe? Tunaona mashababi na watu tija na vipawa vikipotelea humo. Kisha kudai haki watambulike. Si vibaya kuiga kitu chenye kujenga ila hili ni dhambi hata kwenye maandiko ya dini zote. Ni upumbavu.

Maisha ya uchumi wa mtu wa kawaida yanazorota kwa upandaji bei kwa kila bidhaa. Ruzuku haziingii kwenye maeneo yanayostahili kumpunguzia mzigo wa ugumu wa uchumi mtu wa chini. Badala yake tunazidi kuona manunuzi ya vitu vikubwa vya thamani. Kujali matumbo ya watu wachache wanaowatumikia wananchi si sawa.

Magari kama Land cruiser L300 na mengine ya mfanowe yananunuliwa kuwafurahisha wachache wenye matumbo makubwa zaidi na waliolala njaa waendelee kuumia na ukubwa wa milima ya ghalama za Maisha matumizi ya tawala zetu ni kubwa yaani tumeenda kwenye matumizi Zaidi ya tunachoingiza mfukoni. Sipo kwenye upande wowote wa siasa ila muh. John Eche ni mtu mzuri sana kuzungumzia mambo kama haya kwa niaba ya mtu wa chini pia wapo wengine kadhaa wenye uthubutu na kujitoa kuwazungumzia wasiozungumza na kusikika kwa wengi. yeyote amfatilie kwenye picha mwendo zake za mitandao atajifunza vyema. na wawajibikaji ni akina nani?

Itoshe kusema Asante Mungu kwa uzima na hali tuliyoikuta kwenye ardhI yetu. Kwa mtu kama mimi wa miaka ya 1990 na kitu imenifunza kwenye hii ardhi ni mapambano na akili inabidi ione mbali kufikia hatua nyengine. Haina haja sana kufanya kazi kwa bidii ila kufanya kazi kwa akili nyingi. vijana wanakosa pa kushika baada ya kumaliza elimu yao ya juu. Elimu na mitaala ni elekezi kwenye ajira pekee kama mkombozi wa kila kitu, ila si elekezi kumfanya mtu aelewe changamoto ya mtaa na uhalisia wa ugumu wa soko la ajira. Elimu ya mtoto sio kumkaririsha ni kumuelekeza mazingira wezeshi ambayo yatatoa mwanga baada ya kumaliza masomo asiitegemee serikali na mashirika kuajiriwa.

Bado tuna fursa nyingi mtaani ukishinda na watu toka nchi jiran (Kenya, Rwanda) wao huziona zaidi na wana uthubutu na mazingira wezeshi kuzifuata na kuchukuwa kila kombolezo la mtu wa ardhi hii ya Tanzanite. Wengi hatuna kitu kichwani na wengi ni tegemezi, ni sababu ya mfumo wa kukaririshwa na si kuona fursa ambazo wenzetu hawana kwenye nchini zao na wakija hapa huzikimbilia. Mazingira wezeshi ni hafifu vipato duni na urasimu mkubwa uliokithiri na yanafunga mboni zetu kwa kuingizwa woga ndani ya vifua vyetu na kukosa uthubutu wa kula keki ya taila letu.

Ardhi imejaa mali, na wazawa wamejaa sifuri, Ni wachache huzivuta na kuzitumia. na inafikia kipindi ambacho unaona bora ya mtu aliyefeli mtaani kuliko msomi. Maana wasomi wachache wenye kujua wapi pa-kushika. Muulize dada yangu Hussna Hassan Msanya, msomi mzur na mtu wa kuaminika kwa yeyote na mtenda kazi hodari ambaye hajawahi pata pahala pa kumuingizia kipato vyeti vyake vinaongea kwa sauti kubwa na uwezo wa kiutendaji.

Tunaweza badilisha haya na kuamua sasa ni kipi cha kufanya kuiunda vyema ardhi yetu. Sihitaji kusema nani ni nani ila najaribu kidogo kuonyesha umuhimu wa maadili na kutojidhalilisha kwenye kizazi cha upinde wa rangi kwa kuwa na msimamo na sautI ya pamoja kukemea hilo. Pia hali ya uchumi wa m-tanzanite kubadilika kwa kumzingatia mtu wa chini zaidi badala ya wachache wanaoonekana wanatija, na kupunguza matumizi yasio na ulazima kuweka ruzuku kwa kipaumbele cha mtu duni anayeshuka kiuchumi kila kukicha na Tatu mitaala ya elimu ya m-Tanzanite. Wazungu husema (if you don't do anything, nothing is going to happen) kama hufanyi kitu hakuna kitakachotokea. maamuzi yetu kama wa-Tanzanite na wateuliwa na wachaguliwa wetu kwenye viti mulivyokalia wote tunaweza jadili na kubadili mwanga halisi wa ardhI yetu tajiri mashariki ya Afrika. tusipofikia maamuzi mazuri tutakosa jawabu kama wazungu walivyoshindwa kuelewa ng'ombe kula nyasi alafu anatoa maziwa.

Baada ya uandishi huu

Nikifanikiwa kushinda nitabadili maisha yangu, maana sina kazi yeyote ni mpambanaji wa mtaani tu majukumu yananiumiza kama mwandishi, ambaye nina elimu ya juu Ya chuo Cha Dodoma kwenye masuala ya Utawa wa uma.

Na sina wa kumuomba zaidi ya Mungu naamini mm ndo mshindi.

Asanteni na tusameheane kama kuna shemu nimeteleza nikaandika maudhui ya kumkwaza mtu .na kuna alama za uandishi hazikuwa sawa. Kikubwa ujumbe wangu utafika pakubwa. na kama itapendeza iwe ujumbe kwa Rais wetu mama Samia Suluhu. Niombeeni nafasi najiamini kwenye utendaji. Maana wengine sisi ni kadari ya Muumba tupo hai ukilinganisha na uhalisia wa maisha yetu.

Rashid Kapande
0659 436 478 (Whatsapp number)
kapanderashid@gmail.com
 
Back
Top Bottom