Binti Magufuli
JF-Expert Member
- Apr 2, 2011
- 7,479
- 5,161
Nilikumiss pia my dia Heaven on earth, nafurahi kukuona hapa ukiwa mzima wa afya.......more blessings upon you
Last edited by a moderator:
''when u lose someone close, remember that they are in a better place now''
May God rest his soul in Eternal peace
AMEN.
jamani mshairi wangu Himidini^^
Pekee twajiongoza
Milima tunapanda
Mabonde twashuka
Jangwa la ukimya
Chozi maji ya kunywa
Jua likituchoma
Mvua inatunyeshea
Adui wametuzunguka
Moyoni twakuombea
Baba twakupenda
Mimi na Heaven on earth,
alama ya uhai wako.
...
Malaika twawatuma
Mwambien nampenda
Hatujamtenga
Dunia imetutenga
Kila pumzi haitaepuka
Tumaini letu baba
Siku akituita Mola
Tutafurahi pamoja
Uko Heaven onheaven
Baba hapa tazama
alama ya uhai wako
...
Tumekua hakika
Mengi tumefunzika
Tele bado kutufika
Mungu aliyekulinda
Nasi bado atupenda
Kwa imani tutashinda
Tunaijenga hi dunia
Iwe njema mithili ya
Heaven on earth
^^
Thanks Lady doctor wangu
Kiukweli kabisa Heaven on earth umenifanya nilengwe na uchozi hapa. Najaribu kufikiria unavyowaza na unavyomkosa mzazi wako. Najaribu kulinganisha na wale ambao wazazi wao bado wako hai lakini hawawaheshimu na kuwapenda.... Dunia mbaya sana hii!!!
Namwomba Mungu, kilio hiki kama ikibidi mabinti zangu wawili wasikilie. Nishuhudie watakavyopambana na maisha katika umri wao wa utu uzima. Niwasimamie mpaka pale watakapoweza kusimama imara katika maisha yao.
Ni kwa mustakabali huu, Heaven on earth namwomba Mwenyezi Mungu, aendelee kumpumzisha baba yako mahali pema peponi, na aendelee kukubariki, akuepushe na mabaya yote ili kile kilio cha "laiti baba angekuwepo" kisitoke kinywani mwako. Ili siku Mungu atakapowaunganisha tena peponi, baba yako akupokee kwa furaha. Amina
Raha ya Milele umpe Eee Bwana, Na mwanga wa milele umwangazie, aendelee kupumzika kwa amani. Watu wote tuseme AMINA!
Mkuu Asprin, umeandika maneno mazito sana ambayo yanahitaji tafakari nzito hasa kwetu sisi vibaya, I always buy your wisdom bro.Kiukweli kabisa Heaven on earth umenifanya nilengwe na uchozi hapa. Najaribu kufikiria unavyowaza na unavyomkosa mzazi wako. Najaribu kulinganisha na wale ambao wazazi wao bado wako hai lakini hawawaheshimu na kuwapenda.... Dunia mbaya sana hii!!!