heloukiwa na simu ya 3g unaweza kutumia huduma hii, kulingana na maelezo ya vodacom wanasema huduma hii ni free (all data free) wanasema no charge apply when using dstv mobile, nilipojaribu kuangalia ilitakiwa kusajili kwanza baada ya hapo ikaja list ya channel then nikachagua channel nilotaka kuangalia, ila baada ya mda mfupi ikakata, niliangalia balance nikakuta nina 0.00 na kulikua na sh 900 na ckuangalia hata kwa dakika mbili , nilipiga simu nikauliza customer care akasema hawakati hela nilipomwambia mbona nimekatwa alisema nisubiri then akakata simu, nilipopiga mara ya pili niliambiwa na mtoa huduma kuna gharama za internet zinatumika hivyo inanibidi kununua bundle nilipouliza wanachaji kiasi gani ili niweze kununua bundle ya kutosha alisema hafahamu akakata simu, sikuridhika nikapiga simu tena akapokea mwingine nilipomuuliza kama naweza kujiunga na bomba ( unlimited internet ambako kuna ya wiki wanachaji elfu 10, na mwezi elfu 30) ili niweze kutumia dstv mobile alinijibu dstv mobile haihusiani na internet bundle wanachaji hela ya kawaida kwenye simu, ilinisikitisha sana kuona watoa huduma wanapingana, na gharama ni kubwa kiasi kwamba almst ni zaidi ya tsh 600 kwa dakika, je nikitaka kuangalia saa moja itakua kiasi gani..mpaka sasa sitaki kutumia huduma hio kutokana na gharama ( unafuu pekee ni kwamba hulipii huduma za mwezi za dstv)