Drone ya Putin ilivyokiteketeza kifaru bora cha Uingereza

Juma Wage

Member
Sep 8, 2023
60
201
Duniani kuna vifaru vitatu hatarishi kwa mapigano katika uwanja wa vita.

Vifaru hivyo ni Abraham's cha Marekani, The challenger (Uingereza) na Leopord (Ujerumani)

Hata hivyo waswahili wanausemi "Ivumayo haidumu" na hivyo ndivyo inavyothibitika kwa wababe hao wa ardhini.

Tangu vita ya Russia na Ukraine ianze, silaha hizo za maangamizi zimetumika kwa wingi kumdhibiti Putin.

Challenger na Leopords viliingia vitani kwa madai ya kumfunda Putin kucheza ngoma waitakayo mkoleni.

September 05 mwaka huu kifaru cha Kiingereza "The challenger" kikaangukia mikononi mwa ngariba (Putin).

Kifaru hicho kilikanyaga bomu la ardhini kisha ndege nyuki (drone) ya Russia aina ya "Lancert" kukisambaratisha mithili ya ndafu mbele ya mashababi yenye uchu wa nyama.

Kwa dharau, Rais Vladimir putin ameutangazia umma kuwa anavisubiri vifaru vya Marekani "Abraham's" aviteketeze kama alivyofanya kwa Leopords na Challenger.

Ndimi Juma Wage
Dodoma.

IMG-20230906-WA0022(1).jpg
 
Kwa hiyo vita ndio vimeisha na maeneo walioteka Russia yamekuwa na amani chini ya mtawala mpya dikteta Putin, au sio.
 
Back
Top Bottom