Drip irrigation system-Gharama

2018

JF-Expert Member
Jan 1, 2018
546
778
Habari
Kuinstall drip irrigation system inaweza kugharimu kiasi gani kwa hekari moja ya shamba?
Nipo Morogoro mjini,na je ntawapata wapi wataalamu ya kazi hii
 
Attachments

  • 20170831_154530.jpg
    20170831_154530.jpg
    359.8 KB · Views: 196
Habari
Kuinstall drip irrigation system inaweza kugharimu kiasi gani kwa hekari moja ya shamba?
Nipo Morogoro mjini,na je ntawapata wapi wataalamu ya kazi hii
Gharama za drip irrigation hutegemea na mambo mbali mbali kama
1.Aina ya zao unalotaka kumwagilia
Mfano dripline za papai ni tofauti na zile za nyanya, hoho na mazao mengine ya mboga mboga kwa hyo Gharama pia hutofautiana
2. Shamba lilivyokaa (topography) na mapendekezo ya mteja
Drip irrigation kwenye shamba ambalo ni flat hutofautiana na shamba ambalo lina mwinuko au mteremko kwa sababu shamba la namna hii utahitaji kuligawa katika plot (head units) ndogo ndogo ili utokaji wa maji uwe sawa kwa kila mmea tofauti na shamba ambalo ni flat lisilo hitaji kugawanywa
Pia mteja anaweza kuamua kugawa shamba lake kwenye plots mfano wateja wengine wanaweza kuamua hekari moja igawanywe mara mbili na kila nusu hekari anaotesha zao tofaut so gharama hapa zitatofautiana
3. Materials zinazotumika
Katika drip irrigation zipo materials kutoka kampuni mbalimbali zenye specifications na ubora tofaut mfano tuongee issue ya wall thickness. Zipo drip zenye wall thickness ya 1mm, 0.6mm, 0.4mm(hizi ndio nyingi sokoni)., 0.2mm na pia zipo dripline za round, flat na nyingine ni pressure compensation na pia zipo za self flushing so Gharama pia zinategemea unatumia materials gani na kutoka kampuni gani mfano Netafim, captain, azud, toro, john Deere, irritec, green agriculture, sertan, vishaka, mertplus, irrist, approtech na nyingine nyingi

Kwa kumalizia kama mkulima unahitaji irrigation system angalia zaidi ubora wa kati na uchukue material ambazo unaweza kuzitumia angalau kwa miaka mitano ili uweze kurudisha Gharama Zako
Pia tafuta mfungaji mzuri ili system yako iweze kufanya kazi kwa tija nzuri
Pia hakikisha unawekeza pia kwenye usimamizi wa mradi wako ili uweze kupata faida kwani unaweza kuwekeza sana kwenye infrastructure na kusahau kuwa usimamizi na agronomia ni msingi. Mfano ukikosea kupiga dawa au kuweka mbolea utaishia kupata hasara na kulaumu drip irrigation

Kwa maelekezo haya karibu tukuhudimie sisi tunafanya design, installation pamoja na uuzaji wa vifaa vya irrigation tupo morogoro mjini na dsm mikocheni
0763347985 / 0673000103
Gharama zetu ni 2.5mil-3mil kulingana na factor nilizoeleza hapo juu
 
Good sana, Mungu akubariki
 
Mkuu mimi ninazo bunda kumi za 1000mtrs mm 16 na vifaa vyake je hizi zinaweza kuhudumia ekari tatu kwa kilimo cha mahindi au mazao yenye space kama hizo? na je gharama za kufunga tu utanitoza sh ngapi ? shamba langu liko flat.
 
Hi mkuu
Ni ngumu kusema moja kwa moja kuwa roller kumi zinatosha shamba la ukubwa gani kwa sababu kuna wengine wanapendelea single row na wengine double row kuendena na zao wanalotaka kulima lakini kwa mazao ya Mboga mboga roller kumi zinatosha hekari mbili na robo hivi for double row na hekari tatu for single row
 
Mkuu mimi ninazo bunda kumi za 1000mtrs mm 16 na vifaa vyake je hizi zinaweza kuhudumia ekari tatu kwa kilimo cha mahindi au mazao yenye space kama hizo? na je gharama za kufunga tu utanitoza sh ngapi ? shamba langu liko flat.
Gharama za kufunga kwa hekari moja ni kuanzia 350,000 mpka 500,000 inategemea na eneo na mapendekezo ya mteja
 
NYANGI IRRIGATION DEPARTMENT -NID
Tujifunze kilimo cha umwagiliaji kwa technology ya esrael. Kwanini kuna baadhi ya wakulima wana vifaa vya kisasa vya umwagiliaji lakini bado wanashindwa kufanikiwa Katka kilimo na kufikia hatua ya kukata tamaa na kuona kilimo hakina faida! Sasa leo nataka tujifunze mambo muhimu ya kuzingatia katika kilimo cha umwagiliaji kitaalamu. Kwanza naomba utambue maana halisi ya UMWAGILIAJI, umwagiliaji ni kumwagilia kiasi cha maji yanayoitajika kwenye mmea kwa wakati husika na kipindi husika, ninaposema wakati husika namaanisha mmea kila unapokua na kuongezeka unakua na maitaji tofauti ya maji unapokua mdogo mpaka unapovuna ila nimeona wakulima wengi wanamwagilia kiasi kimoja cha maji kuanzia mmea upo mdogo mpaka kufikia mavuno hili ni kosa kitaalamu, ninaposema kipindi husika ninamaanisha hali ya hewa kwani kuna kipindi joto linakua kali na mmea unapoteza maji mengi na kipindi joto linakua chini mmea unapoteza maji Kidogo sasa wakulima wengi niliowahudumia awafuati suala hili. Kuna vitu muhimu unaitaji kuvizingatia kabla ya kufanya kilimo cha umwagiliaji kitu cha kwanza mkulima anatakiwa kufanya IRRIGATION PLAN (mategemeo ya kilimo cha umwagiliaji) hii irrigation plan inafanya na utalaamu kwa kuzingatia mambo haya muhimu 1. Muonekano wa Shanna (topographical) 2. Aina ya udongo katka shamba husika, tunalitazama hili kwasababu kuna utofauti wa umwagiliaji ktk kila aina ya udongo mf. Mfinyanzi umwagiliaji wake mdogo kwa kua unatunza maji, tifutifu umwagiliaji wake mkubwa kwa kua unapitisha maji sana. 3. Kiasi cha maji ktk shamba usika na chanzo chake kama ni mto au kisima tunaliangalia hili ili kujua kama kiasi cha maji kinauwezo wa kumwagilia mazao husika bila kuwa na mapungufu. 4. Aina ya zao mkulima analotaka Kulima tunaliangalia hili kwani kila zao linamaitaji yake na pia system ipi ya umwagiliaji inafaa mf. Sprinkle uwezi kuweka kwenye nyanya wala matikiti hivyo kila system ya umwagiliaji uenda na aina ya mazao. Baada ya kila kitu kikiwa sawa ktk IRRIGATION PLAN sasa unakuja hatua nyingine mtaalamu anatakiwa kudesgn ramani ya shamba na ramani ya ufungaji wa Kifaa, mtaalamu akishamaliza kudisign ramani ndipo kifaa hufungwa shamani baada ya hapo mkulima anaitajika kupewa mafunzo jinsi ya kutumia kifaa cha umwagiliaji na kufanya service ndogondogo ktk kifaa baada ya hapo mkulima huyu anaitajika kupewa mwongozo wa umwagiliaji kulingana na aina ya zao, aina ya udongo na kipindi husika, ni vizuri mkulima huyu kutembelewa ili kuona maendeleo yake hususani yule mkulima ambae ni mara ya kwanza kutumia kifaa cha umwagiliaji na yule ambae ana elimu ya kutosha ya umwagiliaji, ni vizuri mkulima huyu apewe spair za kifaa ili ikitokea tatizo dogo ktk kifaa aweze kulitatua mwenyewe bila gharama.
NB
Karibu Asilimia 70 ya kilimo ni umwagiliaji, 10% mbegu Bora, 10% mbolea, 10% madawa na kazi nyingine za shambani mf. Kupalilia., kupandishia udongo nk. Mambo haya 4yanaenda kwa pamoja kama kuna moja halitaenda vizuri linaaribu matokeo mazuri ya kilimo na pia mambo hayo yanaenda kitaalamu pia. Naomba nianze na jambo la pili na kuendelea kwani la umwagiliaji nimeshalizungumzia. MBEGU mkulima anaitajika kutumia mbegu bora za mazao ili kupata matokeo mazuri mf. Folio 1 (F1) . Mkulima epuka kupanda mbegu zilizotokana na uzao wa F1 kwani utapata matokeo Mabaya. MBOLEA mkulima anaitajika kutumia mbolea kwa ratiba husika na kiasi usika kulingana na zao husika inaweza kua mbolea ya asili au kiwandani, mkulima kama atakuwa na uwezo anashauriwa apime udongo wake ili kujua kiasi cha mbolea na mapungufu yaliyomo hii itampa mwongozo mzuri wa uwekaji wa mbolea shambani. MADAWA mkulima anashauriwa kutumia dawa kwa wakati na kwa ratiba inayotakiwa kulingana na zao husika sio mpaka huone ugonjwa ndio upulizie dawa hili ni kosa kitaalamu kwani mpaka ugonjwa unaonekana umeshathiri sehemu kubwa ya mazao hivyo matibabu uwa magumu kama mnavyojua ugonjwa kuingia ni rahisi kutoka ni ngumu, pia tunashauri kupulizia dawa kwa ratiba kwani kuna kipindi mmea hauitajiki kupulizia dawa mf. Kipindi cha uchavushaji mmea hautakiwi kuwa na dawa kwani uchavushaji ufanyika na wadudu mf. Nyuki hivyo mmea ukiwa na dawa awatafika na kufanya uchavushaji hivyo upelekea matokeo mabaya ya mazao kwa uchavushaji ndio mwanzo wa tunda la mmea husika. IMETAYALISHWA NA FREDRICK NYANGI 0719549848
 
Back
Top Bottom