Dreamliner, bombardier zingine kuwasili Desemba

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
1138805

NDEGE nyingine mbili kubwa zilizonunuliwa na serikali ili kuendelea kuboresha Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) zitawasili nchini Desemba, mwaka huu. Hayo yalibainishwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe wakati akifungua mjadala wa wazi wa siku mbili, ulioshirikisha wadau wa sekta ya anga jana, ulioandaliwa na Mamlaka ya Usari wa Anga Tanzania (TCAA) wenye kaulimbiu inayosisitiza ‘Matumizi ya Anga katika Kukia Uchumi wa Kati.

Kamwelwe alisema awali ndege hizo mbili, zilikuwa zinunuliwe mwaka 2020/2021, lakini kutokana na umuhimu wa sekta ya anga katika kukuza uchumi wa nchi, serikali imeona ni vema izinunue mapema zaidi. Alisema sekta ya anga inaweza kuikisha nchi kwenye uchumi wa kati na ndege hizo, zikianza kwenda nje ya nchi, zitaiongezea mapato zaidi serikali. Aliwataka wadau wa anga, kujadiliana njia bora za kuchagiza maendeleo ya nchi kupitia sekta ya anga.

Alisema, usari huo unaweza kusaidia nchi kukia uchumi wa kati kwa kusarisha bidhaa hasa za vyakula kama vile samaki na nyama, ambapo nchi za Ulaya zinahitaji zaidi ya tani 200 za samaki. Alisema kwenye sekta ya nyama, Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeshakamilisha ujenzi wa kiwanda cha nyama, ambacho kitapaswa kuhudumia soko la nyama la nchi za nje pia.

Alisema;“Tangu kuingia madarakani Rais John Magufuli amekuwa akisisitiza mchango wa sekta ya viwanda katika kukuza uchumi wa nchi, hivyo basi ifahamike kuwa sekta hii ya usari wa anga inaweza kutoa mchango kwa asilimia kubwa zaidi.

“Kikubwa ni kwamba mnatakiwa kuja na mapendekezo ambayo nitayatekeleza kwa wakati hata ikiwa ni mabadiliko ya sheria yanayolenga kuimarisha usari wa anga nyie leteni tu. “Ninafahamu kuwepo kwa changamoto kadhaa kama vile idadi ya marubani na hata mafundi wa ndege, hayo yote yanafanyiwa kazi ili kuongeza idadi ya wafanyakazi hao watakaofanya kazi kwenye ndege zetu na kuiongezea ufanisi sekta hii.

” Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usari wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari alibainisha kuwa katika kongamalo hilo, watajadiliana namna ya kutumia mashirika madogo ya huduma za ndege katika kuongeza pato la nchi. Hivi karibuni serikali iliipatia ATCL ndege ya Fokker 50, na kuifanya ATCL kuwa na jumla ya ndege saba ikiwemo Boeing 787-8 Dreamliner, ndege mbili za Airbus A220-300 na ndege tatu aina ya Bombardier Dash Q400.

Rais John Magufuli aliwahi kusema kuwa ndege nyingine ya pili aina ya Boeing 787-8 Dreamliner, itawasili nchini mwishoni mwa mwaka huu na ndege nyingine ya nne aina ya Bombardier Dash 8 Q400, nayo itawasili mwishoni mwa mwaka huu au mwaka ujao mwanzoni.
 
View attachment 1138805

Mmmmmmhhhhh
 
Vizuri lakini wasiue mashirika binafsi kama walivyofanya kwa Fastjet ilikuwa ni mkombozi kwa wananchi wanyonge kutokana na nauli zake rafiki lakini hizi za kwetu nauli ni kubwa mno
 
Lete tu madude, business plans zitayakuta huko angani au yamepaki!
 
Mh. Rais John Joseph Pombe Magufuli mwakani tununulie DEGE kubwa la mizigo tupeleke matikiti maji kwenye nchi za wenyewe!
 
Mbona Disemba mbali yaletwe mwezi Agosti,niyapande kwenda kwa manyang`au.
 
Ni vizuri kununua ndege. Shida ni kwamba zisije zikawa liability na kukomba pesa za kodi zetu. Bihashara ya ndege inahitaji umakini wa hali ya juu sana. Kuna nchi za wenzetu wa majuu zinaendesha mashirika yao kwa hasara hat SA ni kila siku serikali inawa bail out. Tujifunze kwa Ethiopia Airline ambao angalau wamefanikiwa. Pia wapunguze siasa na shirika liachiwe uhuru wa kujiendesha.
 
Tatizo mmebana hela hizo ndege hazitakuwa na kazi.zamani zingepiga kazi sababu hela ilikuwepo
 
Back
Top Bottom