DRC yakataza mikutano ya kisiasa

DRC yakataza mikutano ya kisiasa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,610

KINSHASA,CONGO

MAMLAKA nchini Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) zimepiga marufuku mikutano ya kisiasa kufuatia mvutano baina ya wafuasi wa Rais Felix Tshisekedi na wale wa Rais aliyemaliza muda Joseph Kabila.





Tshisekedi alichaguliwa Desemba mwaka jana na kuchukua nafasi ya Kabila ambaye amedumu kwa miongo kadhaa madarakani.

Mvutano umezuka katika mji wa Kinshasa baada ya Jumuiya ya Vijana (UDPS) kutoka chama cha


Tshisekedi kutangaza kuwa kitaandamana dhidi ya mgombea wa Waziri wa zamani wa Sheria kwa urais wa Seneti.

Kamanda wa Polisi Kinshasa Jenerali Sylvano Kasongo alieleza kupitia kituo cha televisheni ya Taida kwamba, Gavana wa Kinshasa amepiga marufuku mikutano ya kisiasa kwa wiki hii.

“Yeyote atakayejaribu kuandamana au kukiuka amri kwa wiki hii atakutana na polisi,” alisema.

Msemaji wa UDPS vijana Fils Mukoko aliwaeleza waandishi wa habari kwamba wanataka kupinga kwa kile wanachokiona kuwa ni sura hizo hizo katika taasisi za serikali.
 
Back
Top Bottom