Power to the People
JF-Expert Member
- Jul 11, 2007
- 1,198
- 900
Mchepuko asipojitokeza hatapata mgao wa mali anaona aharibu kabisa akijaribu kujitafutia mgao kidogo.
KUna ndugu yangu alikuja kujua mumewe alizaa baada ya mumewe kufa...
Cha ajabu yule mtoto wa nje ni mtoto wa ujanani...ni mkubwa zaidi ya watoto wa huyu ndugu yangu...
Tulishindwa kushangaa kwa nini shemeji alimficha huyu mtoto?
Na kwa nini huyu mtoto alisubiri mpaka siku baba kafa ndo amejitokeza.?
Ukimuangalia carbon copy hakuna haja ya DNA...
Lakini huyu ndugu yangu alimwambia huyu mdada (mtoto wa mumewe)...karibu anytime...hawa ndo wadogo zako...
Lakini kwenye urithi hakuambulia kitu...maana hata babake hakum mention...
Wanaume ni wa ajabu
Ameishi na mkewe karibu miaka 20 na hajawai kumwambia alizaa kabla ya kumuoa...
Familia moja naijua, baba ana mchepuko wa kudumu, watoto wa mchepuko wadogo kuliko wa mke. Watoto wa mchepuko na wa mke wamepelekwa shule moja na baba analipa ada. Watoto wa mke wakirudi nyumbani wanamwambia mama yao shuleni kuna watoto wawili wanaitwa majina kama yetu, mama akapuuzia akijua ni kufanana kwa majina tu.
Baba kapata ajali kafariki watoto na mchepuko hao wakatia timu, mke lipoteza fahamu kwa muda lakini alipozinduka ungefikiri ilikuwa ni sherehe na sio msiba. Mtu kazikwa maisha yanandelea, mchepuko na watoto wawili hawakupata chochote
Mchepuko lazima awe na uchungu,, halii msiba analilia fungu dogo atakalopoekea huku akijua anaweza asipate kabisa........
Hapo lazima kilio cha uchungu kiwe 4×4 by far
Mchepuko lazima awe na uchungu,, halii msiba analilia fungu dogo atakalopoekea huku akijua anaweza asipate kabisa........
Hapo lazima kilio cha uchungu kiwe 4×4 by far
Huyo wa miaka 19 alikuwa wapi muda wote asijiweke sawa. Ningekuwa yeye nimeshindwa kujipanga muda wote huo nakaa kimya hata mazishi naenda kama waombolezaji wengine. Tena nashukuru hatujagundulika na ameshakufa. Mwanamke atakuwa mjinga sana kama atashndwa kujipanga kwa ajili ya watoto wake muda wote huo. Ni aibu kubwa kuleta drama wakati wengine wako kweye majonzi.

Kuna msiba fulani tulishuudia mdada analia kupita wafiwa...kila mtu alikuwa anataka kujua uhusiano wake na marehemu...
Maana si ndugu waka mke aliyekuwa anamjua huyo mdada...
Ila yeye hakutaka kusema kilichokuwa kinamliza...lakini minong'ono sasa...unasikia huyu lazima awe small house...
Mbaya sasa jamaa alikuwa kafa na ngoma...
Hivi unawajua wanaume??? wana siri mno na hawapendi kutambulisha mchepuko yani kama kosa la jinai........
Mie tina nizae na mume wa tu ntachuna hadi mazivu yake ili mradi nipate changu mapema hata akifa nione poa tu.
Wanawake na sisi ni wajinga sana unakubali kuwa mchepuko na kuzaa watoto maana hizo kesi zipo nyingi sana kujitokeza msibani
Very true, kama alishindwa miaka yote 19 huko msibani atapata nini
Huyo ni wale wanaotembea na wanaume wenye fweza zao kwa masharti kama ya World Bank...
Nakupa utakacho...siku ukitia mguu nyumbani kwangu ndio ujue mwisho wako umefika...
Sasa yeye kaona isiwe shida...kama matumizi napata...
Sasa jamaa akifa..ndio hapo...kutunza siri ili kulinda buzi kumemponza
Hamjasema lakini mngefanya nini kama ungekuwa mchepuko ukakakutwa na haya.