kinachowashangaza wengi hapa ni ufisadi, wapo wazuri wengi, ila fedha za dhuluma zinapumbaza akili, sio kwamba hawajui ukweli, au hawajui uchumi. Tatizo kubwa ni hali ya kutetea uovu inafanya hata credibility na credintial zako zote kupotea.
Dr Slaa kaamua kutumia elimu yake na uzoefu kusaidia wananchi kutoka moyoni, na watu kama hawa duniani hubakia kwenye mioyo ya watu, huwezi kupambana nao, ni kawaida kuchukiwa kubezwa na kutengwa na wakubwa, ila siku zote wanashinda. kuna ahaja ya kujenga kizazi kinachokubali kuishi kwa kufanya kazi na kushangilia ubunifu, taaluma na uadilifu badala ya sasa mwizi ni shujaa na fisadi ni mjanja.
hongera Dr. Slaa kuwa mfano; wasomi wengi, wanatupa elimu na utu wao kwa rushwa na madaraka mabovu, hakika tutakuenzi milele.