Ndugu wana-JF, naomba mniondolee utata ulionikumba. Kuna tuhuma kwamba serikali inahusika na utekaji wa Dr. Ulimboka na kumfanyia hayo waliyomfanyia. Swali langu la kwanza ni kutaka kueleweshwa kama serikali ilikuwa na nia ya kumuua au kumtesa tu Dr. Ulimboka. Kama serikali ilikuwa na nia ya kumuua, ni kwa lengo gani? Na kama ni kweli serikali ilikuwa inataka kumuua Dr. Ulimboka, inawezekanaje wakatumwa tu watu wa hovyo hovyo ambao wanashindwa kujiridhisha kuwa nia yao imekamilika na kwamba kama hawatakamilisha jambo hilo watakuwa wamewatia matatani watu/chombo kilichowatuma? AU; Ni kweli kwamba kwa PROFESSIONALS kama hao, tunataka tujiaminishe kuwa WALIKOSEA kwa kujiridhisha kuwa Dr. Ulimboka alikuwa amekufa kwa kumuangalia kwa macho tu? Na je, kama lengo lao lilikuwa ni kumtesa tu, ni kwa sababu gani?
Naomba mniweke sawa kabla sijaendelea.