VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Naweza kuamini kuwa sasa umeshaanza kunogewa na vyeo. Ulianza kuwa Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba. Ukafuata kuwa kiongozi wa Kamati ya Bunge Maalum la Katiba. Kama hiyo haitoshi, ukateuliwa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Sasa unataka Uspika wa Bunge.
Ukiwa ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hukupaswa kujitokeza kisiasa na kugombea Uspika wa Bunge. Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali si mtu mdogo. Ndiye Kaimu Mwanasheria Mkuu wa Serikali pale ambapo Bunge hufanyika kwakuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali huwa Bungeni Dodoma. Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni mtu wa kitaifa zaidi.
Kujianikaanika kama kada wa CCM si jambo jema wala vutizi. Kutakuwa na kitu na watu wanaosababisha. Nani kakutuma? Unataka nini hasa? Kwanini? Dr. Tulia, umejianika kama kada. Watumishi wa Ofisi yako na wananchi kwa ujumla watakuonaje ikiwa utaendelea kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali?
Ili kulinda heshima yako, jiuzulu Unaibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na urejee Shule Kuu ya Sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ukahadhiri pale ambapo Uspika utagoma kupatikana. Ujiuzulu haraka!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)