Dr Tulia Ackson Miaka yote aikuwa wapi?

Dr Tulia Ackson Miaka yote aikuwa wapi?

mkimpa ubunge huyu dada, nitawadharau sana wanyakyusa.
Nilimuona jana kwenye tv na yule mwingine S. H. Amon wakihamasisha kitu. Kilichonichekesha ni Amon kusema eti "elimu, elimu, elimu" ndio nikajua hawa jamamaa hawawezi kueleweka mpaka wakiwekwa benchi!
 
nakumbuka kukusoma huku ukitangaza nia. au ndio kusema mpinzani wako kakuzidi kete? pambana kama unaweza badala ya kutulilia sisi.
 
Haya mambo yalikuwepo toka siku nyingi tena mashindano hasa .Nakumbuka tulikuwa wadogo tunayaona haya.Naona wewe akili zako zote umejaa siasa kuna watu wanaona mbali zaidi ya siasa , vile vile kufufua ngoma za asili ambazo siku nyingi zilishaanza kusahaulika anatakiwa kupongezwa badala ya kushutumiwa .Badilikeni jamani.

Umesema vizuri Falema. Mwaka fulani kanda ya Ziwa wanasiasa kadhaa waliwashauri wananchi wa Jimbo moja wamchague ubunge msomi wao mmoja mtu wa Kimataifa hivi huenda siku moja atapata nafasi moja ya juu nchini. Huyu msomi alikuwa ameoa raia wa kigeni. Wakakataa kwa sababu hiyo. Wakampiga chini wakachagua mbunge ambaye kama alisema kitu Bungeni basi ni mara moja. Walijuta. Miaka mitano hakuna maendeleo. Acha watu wa kwao Mhe. Naibu Spika wapime wenyewe. Usijaribu kuwarubuni na wewe pia (mtoa mada wa mwanzo - Erthy). Ushauri tu kwa shemeji zangu wa Kandete, Mwakaleli, Isange na Rungwe yote.
 
Mbona Mr Sugu aliingia kwa gia ya kuendeleza Hiphop Mbeya na hatukusikia yote hayo,na kuna wengine wamekuwa maarufu kwa kutukana viongozi,mwache Tulia atulie na amang'oma yake.Hata asipoleta hiyo mipalaano Tu;ia atakuwa mbunge tu .Mambo ya watu wa CCm waachie wenyewe kama vile mambo ya Chadema mlivyoachiwa wenyewe kikolo.
Kutumia ngoma za asili ili kupata mteremko wa ubunge ni sawa na kuwadhalilisha watu wa Rungwe .
 
Time will tell.ila anachamsha mji amefanya mambo mengi,kikubwa kama ana nia ya dhati na jimbo lake.
 
Wakuu natanguliza salamu ,

Naomba kuweka wazi kabisa kwamba mimi ni mwenyeji wa Mkoa wa Mbeya , Wilaya ya Kyela , kijiji cha Kajunjumele ,utamaduni wa Kyela na Rungwe unashabihiiana kwa kiasi kikubwa sana , wakazi wengi wa Wilaya hii ni Wanyakyusa , japo kuna makabila mengine.

Tunazo ngoma za asili ambazo kwa uchache ni Mang'oma , Ipenenga , Samba nk , na tumecheza ngoma hizi kwa miaka mingi bila msaada wa hela ama chochote kutoka kwa yeyote , kama kuna aliyetoa chochote basi alitoa kama vile PDG Ndama Mutoto wa ng'ombe anavyowapa wanamuziki wa FM ACADEMIA .

Sasa cha kushangaza mwaka huu amezuka mfadhili wa ngoma za asili aitwaye Tulia Ackson , Huyu tetesi zinadokeza kwamba lengo lake si kufadhili ngoma za asili , maana alikuwepo miaka yote na alikuwa na uwezo kama huu wa leo , lakini hakufanya hivi , taarifa zinaonyesha kwamba amelenga kurubuni wakazi wa Rungwe ili achaguliwe mbunge uchaguzi ujao .

Mbinu hii ya kizamani haikubaliki , na naomba kuchukua nafasi hii kuwaasa wana Rungwe kumuogopa huyu mama kama ukoma .

Dr Tulia aliyeingia bungeni na kubebwa kwa mbeleko ya chuma hadi kwenye unaibu spika , amekuwa mstari wa mbele kudhalilisha na kunyanyasa wabunge wa upinzani , amezima mijadala mingi yenye tija ili kuokoa chama chake , huyu hawezi kuwa msaada wa Akina Mama wauza ndizi na maziwa wa ushirika au Kiwira , hafai hata kuwa Mwenyekiti wa kijiji cha Makandana , hafai .

Dr Ngunangwa aliwahi kuwauliza waliokuwa wanajipitisha kwenye jimbo lake huko Njombe na kutoa zawadi za baiskeli nk , kwamba WALIKWINA ? yaani kwa kiswahili , MIAKA YOTE WALIKUWA WAPI ?

Nakala ya uzi huu imfikie JOHN MWAMBIGIJA .
Young man, get a life...inakusaidia nini kujenga chuki kwa Dr. Tulia? Amekwambia ana lengo la kugombea ubunge? Bavicha mbona mna roho mbaya hivyo? Hutaki na hata hupendi utamaduni ngoma zenu zipate zipate mtu wa kusambaza kwa ufadhili?
 
nakumbuka kukusoma huku ukitangaza nia. au ndio kusema mpinzani wako kakuzidi kete? pambana kama unaweza badala ya kutulilia sisi.
Ni kweli nimetangaza nia lakini si Rungwe , mimi nimejipanga kumuondoa Nkurunzinza Mwakyembe Kyela .
 
Haya mambo yalikuwepo toka siku nyingi tena mashindano hasa .Nakumbuka tulikuwa wadogo tunayaona haya.Naona wewe akili zako zote umejaa siasa kuna watu wanaona mbali zaidi ya siasa , vile vile kufufua ngoma za asili ambazo siku nyingi zilishaanza kusahaulika anatakiwa kupongezwa badala ya kushutumiwa .Badilikeni jamani.
Shurti asigombee ubunge ili nia yake iendelee kuwa njema
 
Sauli na mwambigija walikwina pia? Kipindi wanaelezea matatizo ya jimbo la rungwe na huku wakiwemo siku zote wanaona.walikwina?
Unauliza tu ! Hao unaowasema hapa wanaishi siku zote Rungwe na wanashiriki hata kucheza hizo ngoma miaka yote , kosa la Sauli ni kujiingiza ccm , atajutia milele ! Ni heri angejikalia kando tu .
 
Unauliza tu ! Hao unaowasema hapa wanaishi siku zote Rungwe na wanashiriki hata kucheza hizo ngoma miaka yote , kosa la Sauli ni kujiingiza ccm , atajutia milele ! Ni heri angejikalia kando tu .
Hahah wapi wewe hao waheshimiwa ulikula nao,kabla ya wao kutangaza nia ama kuanza kampeni? Yuko wapi saiv mzee wa upako,mbona hatumuoni tena saiv?
 
Hahah wapi wewe hao waheshimiwa ulikula nao,kabla ya wao kutangaza nia ama kuanza kampeni? Yuko wapi saiv mzee wa upako,mbona hatumuoni tena saiv?
Utamsikia wapi na Magufuli anaogopa siasa ?
 
Back
Top Bottom