Dr. Slaa ziarani Manyara

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willbroad Slaa, anatarajiwa kuanza ziara ya ujenzi na kukagua uhai wa chama katika maeneo mbalimbali ya wilaya za Mkoa wa Manyara,siku ya Jumamosi, tarehe 18-26, Mei 2013

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu Dkt. Slaa ataambatana na watendaji wa Makao Makuu ya CHADEMA pamoja na wabunge wote wa CHADEMA Mkoa wa Manyara. Akiwa katika ziara hiyo, mbali ya kupokea taarifa na kukagua uhai na ujenzi wa chama katika maeneo atakayopita, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atafanya mikutano ya hadhara takriban miwili kwa kila siku pamoja na mikutano ya kikazi ya ndani, ambapo atakutana na wanachama na viongozi wa maeneo husika.

Ratiba ya ziara hiyo itakuwa kama ifuatavyo:

Atawasili Babati Mjini 18/5/2013 asubuhi; ambapo kutakuwa na mapokezi na kisha salamu kwa wananchi eneo la Minjingu, baadae atakuwa na mkutano wa hadhara saa 9 mchana viwanja vya Kwaraa, Babati mjini. Akiwa njiani kuelekea Hanang, tarehe 19/5/ 2013, Katibu Mkuu atapita na kuwasalimia wananchi wa maeneo ya vijiji vya Masqaloda, Measkron, Nangwa na Dirma, kabla ya kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo ya Balangida na Gendabi (Hanang). Tarehe 20/5/2013, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atafanya mikutano ya hadhara Basutu (Hanang) na Hydom(Mbulu)

Siku ya tarehe 21/5/ 2013, Katibu Mkuu wa CHADEMA atakuwa na mkutano wa hadhara Dongobesh na Mbulu Mjini. Tarehe 22/5/2013 akiwa njiani kuelekea Babati Vijijini, Katibu Mkuu atawasalimia wananchi wa vijiji vya Mutuka na Mwikansi kabla ya kufanya mkutano wa hadhara Galapo Babati vijijini kuanzia saa 8 mchana.

Siku ya tarehe 23/5/ 2013, Katibu Mkuu atakuwa na mikutano ya hadhara maeneo ya Riroda, Dareda na Bashnet, Babati Vijijini. Tarehe 24/5/2013, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakuwa Simanjiro na atafanya mikutano ya hadhara katika maeneo ya Musitu wa Tembo, Ngorika na Ngage.

Siku inayofuata, tarehe 25/5/2013, Katibu Mkuu atakuwa na mikutano ya hadhara katika maeneo ya Orkesimet, Namaruru kisha atamalizia kwa kufanya mkutano mkubwa Mererani kuanzia saa 10 jioni.

Imetolewa leo, Mei 17,2013 na;

Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa CHADEMA.
 
Imekaa vizuri sana ! Kila la kheri Dr Slaa , inafahamika kwamba wewe ni kiboko yao , maana kila unapopita hata Magamba ya mpingo yanapukutika yenyewe ! PIIPOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOZZZZZ !!!!!!!
 
Nagu na Ole Sendeka hawana Amani kabisa,wanamhanya Dr ile hakuna.
 
Mi nikiona taarifa kwa vyombo vya uma naogopa maana huwa akili inaclick kwenye teuzi za sijui mabalozi na ulaji mwingine wa lejaleja
 
Nagu na Ole Sendeka hawana Amani kabisa,wanamhanya Dr ile hakuna.

Akiwa Simanjiro atakipigisha ile mbaya na James Ole Millya ambaye ni adui mkubwa wa Sendeka.
 
Hiyo ni poa kwa sana.,Lakini mbona sijaona ratiba ikionyesha kata ya Magugu?Pale ni kata yenye watu wengi na nilishapita pale nikaona wananchi wana kiu ya mabadiliko na wanasubiri harakati kwa hamu kubwa.Yote kwa yote kila la kheri ninawatakia.
 
Hiyo ni poa kwa sana.,Lakini mbona sijaona ratiba ikionyesha kata ya Magugu?Pale ni kata yenye watu wengi na nilishapita pale nikaona wananchi wana kiu ya mabadiliko na wanasubiri harakati kwa hamu kubwa.Yote kwa yote kila la kheri ninawatakia.

Mkuu Ranks nadhani wahusika wamekusoma.
Mkuu Tumaini Makene fanyia kazi hili.
 
Last edited by a moderator:
Hapo kuna watu kwa sasa hawana amani, wanapanga kufanya hujuma. Dr Slaa ameiweka pabaya band ya muziki inayoimbiwa na Komba...hujipambanua kwa wimbo fulani...CCM inawenyewe...."yaani sio ya watanzania wote" ni watu fulani fulani tena wa hatari, watu kama chenge, Nchemba, Balali, kinana (simba wa tembo)....
 
Gooood planned! sasa nI kwakutumia Helcopter au?
 

Ukiangalia kwa makini hiyo ratiba utagundua Dr Slaa atakuwa very busy kwa siku 9 mfululizo.Hii inaonyesha Dr Slaa anatimiza kwa vitendo agizo la Baraza Kuu la kukisimika chama vijijini.
 
Ukiangalia kwa makini hiyo ratiba utagundua Dr Slaa atakuwa very busy kwa siku 9 mfululizo.Hii inaonyesha Dr Slaa anatimiza kwa vitendo agizo la Baraza Kuu la kukisimika chama vijijini.

You are very right!...
 
Vipi hakutakuwa na ufunguzi wa matawi ya chadema wakati wa ziara hiyo?
 
Nashauri pia Ukimaliza Manyara, apange ziara pia ya maeneo ya Mwanga, Same, Mombo, Korogwe, Lushoto, Muheza, Tanga mjini na Pangani.
lengo ni kumaliza ukanda mzima wa kaskazini kuizika CCM kabisa kabisa.
 
Hongera slaa manyara kwa cdm 2015 ila mumesahau kiteto kwa ole nangoro viva cdm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…