Dr. Slaa: Watanzania wanataka "Safari ya Uhakika"

Dr. Slaa: Watanzania wanataka "Safari ya Uhakika"

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
58,072
Reaction score
134,443
Akihojiwa kuhusu hali ya kisiasa nchini Katibu Mkuu wa CHADEMA alisema watanzania wanatakiwa kuwa makini kuliko kipindi chochote, watoe adhabu stahiki kwa CCM. Alienda mbali zaidi na kusema watanzania wanahitaji safari ya uhakika kufika kwenye kilele cha mafanikio.

Alisisitiza kuwa hakuna sababu ya safari ya matumaini wakati nchi imejaa rasilimali ambazo mataifa ya kigeni wanazitolea macho;

"Kuwa na CCM ni kuishi kwa matumaini, hujui na huna uhakika wa mlo, ajira, shule, soko nk, sasa unahitaji kuishi kwa matumaini na rasilimali zote hizi?" Alihoji Dr.Slaa.

Kauli hii ni pigo kwa Lowasa na kuonekana kufeli dakika za mwanzo


Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), mwaka huu, unaingia kwenye uchaguzi ukiwa na safari ya uhakika na siyo ya matumaini kama ilivyotolewa na mmoja wa watangaza nia ya kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Dk Slaa alisema, kauli hiyo ni moja kati ya nyingi zinazotolewa na viongozi wengi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambazo Watanzania wamechoka kuzisikia na badala yake wanahitaji vitendo.

Alitoa kauli hiyo juzi mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya, alipokuwa akihutubia wakazi wa mji huyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma.

Dk Slaa alisema Watanzania wanahitaji safari yenye uhakika wa maendeleo ambayo watayapata Oktoba, mwaka huu, kupitia upinzani lakini siyo kutoka kwa kiongozi yeyote wa CCM.

"Eti safari ya matumaini, hivi kweli Tanzania iliyojaa kila aina ya madini na utajiri wa kutisha halafu tunasema safari ya matumaini badala ya vitendo? Watanzania tumechoka na kauli za matumaini, tumechoka kuishi kwa matumaini katika nchi yetu," alisema Dk Slaa.

Mbali na hilo, Dk Slaa aliwashangaa baadhi ya watangaza nia wa CCM walioiponda Serikali yao kwamba imeshindwa wakati wao ndio walitakiwa kuwa mstari wa mbele kuondoa kero hizo.

Ukawa wajipanga

Akizungumza kuhusu Ukawa walivyojipanga kuingia Ikulu Oktoba mwaka huu, Dk Slaa alisema wana akiba ya kutosha ya viongozi makini wa kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi.

Alisema wakishika dola hawatakuwa na sababu yoyote ya kukopa viongozi kutoka kwa CCM.

"Hatuna njaa ya viongozi ndani ya upinzani, tunao wa kutosha. Hatuna haja ya kwenda CCM kuwakopa viongozi, Oktoba tupeni ridhaa upinzani tubadili sura ya nchi," alisema.

Kwa upande wake Mbunge wa Mbozi Magharibi (Chadema), David Silinde alisema, licha ya Serikali ya CCM kuamua kugawa majimbo katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kujiokoa, hawataambulia kitu kwani wamejipanga kukabiliana na hali yoyote itakayojitokeza.

"CCM tumewagundua na janja yao, baada ya kuona wabunge wao wamekabwa koo, ndio wanatafuta njia mbadala ya kujiokoa kwa kugawa majimbo, lakini tunasema majimbo yote yaliyopendekezwa kugawanywa Mbeya kama yatapitishwa tunachukua yote," alisema Silinde.
 
Akihojiwa kuhusu hali ya kisiasa nchini Katibu Mkuu wa CHADEMA alisema watanzania wanatakiwa kuwa makini kuliko kipindi chochote,watoe adhabu stahiki kwa CCM.Alienda mbali zaidi na kusema watanzania wanahitaji safari ya uhakika kufika kwenye kilele cha mafanikio.Alisisitiza kuwa hakuna sababu ya safari ya matumaini wakati nchi imejaa rasilimali ambazo mataifa ya kigeni wanazitolea macho."Kuwa na CCM ni kuishi kwa matumaini,hujui na huna uhakika wa mlo,ajira,shule,soko nk,sasa unahitaji kuishi kwa matumaini na rasilimali zote hizi?" alihoji Dr.Slaa.Kauli hii ni pigo kwa Lowasa na kuonekana kufeli dakika za mwanzo

Lowassa anakubalika sana.
Jana kila kona niliyopita watu wanasikiliza hotuba yake.
Nadhani ataleta matumaini mapya.
 
Kweli EL ni mafuriko !
Naamini ndiye Rais kuanzia miezi michache ijayo.
 
Nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa hiyo ni kauli ya Dr Slaa ... CHADEMA na UKAWA wanatakiwa waangalie mtanange wa ndani ya CCM then ndo waje na data zilizokamilika; sasa hivi inaonekana kama UKAWA nayo ni katka timu za CCM...Grrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Hakuna Dawaaaaaa!!!¡!
 

Attachments

  • 1433039194597.jpg
    1433039194597.jpg
    24.9 KB · Views: 1,161
Lowassa anakubalika sana.
Jana kila kona niliyopita watu wanasikiliza hotuba yake.
Nadhani ataleta matumaini mapya.

Wewe ndiyo unayemkubali na UNADHANI atakuletea MATUMAINI mapya.

Umeshaaambiwa hii siyo nchi ya kuishi kwa matumaini, hii ni nchi ya kuishi kwa uhakika lkn kwa ujinga mliojazwa still mko kwenye zama za mawe za kale
 
Slaa ni makini na ndio maana anatoa kauli makini zilizo na ukweli ndani yake iweje tuishi kwa matumaini km wagonjwa
 
Nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa hiyo ni kauli ya Dr Slaa ... CHADEMA na UKAWA wanatakiwa waangalie mtanange wa ndani ya CCM then ndo waje na data zilizokamilika; sasa hivi inaonekana kama UKAWA nayo ni katka timu za CCM...Grrrrrrrrrrrrrrrrrrr


Yaani ww nilikuwa nakuona GT kumbe bure kabisa!! Usichokielewa ni nini kwenye hiyo kauli ya Dr?? Data gani unataka ikiwa umeshindwa kuelewa kauli rahisi kabisa kama hii??

Watu mnakaa kukenulia fisadi kisa njaa zenu bila kutafakari kwa mapana!! Hivi umeshaitafakari cabinet ya Lowasa inayomzunguka?? Mtu una kila kitu alafu unaambiwa uishi kwa matumaini?? Kwa taarifa yako hapo Dr kakutafunia, kazi kwako kutia akili!!
 
Watanzania watajuta kama hawataelewa maonyo yanayotolewa na wachambuzi wa siasa,kwa kipi hasa alichoshawishi jana?
 
Dr slaa ndie Rais ajae CCM waweke mtu yeyote yule lakin wewe Dr slaa tunakuamin na tunaiman na wewe
 
Watanzania tu vilaza sana yaani tumesahau jinsi nyinyiem ilivyochakachua katiba ya warioba na sakata escrow na mengine meengi sasa tunapewa matumaini kama vile wote tunatumiana ARVs
 
Nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa hiyo ni kauli ya Dr Slaa ... CHADEMA na UKAWA wanatakiwa waangalie mtanange wa ndani ya CCM then ndo waje na data zilizokamilika; sasa hivi inaonekana kama UKAWA nayo ni katka timu za CCM...Grrrrrrrrrrrrrrrrrrr
tumikia bwana wako Lowasa achana na Dr.Slaa,huwezi kumkubali Dr.Slaa muda huo unamkubali fisadi
 
Back
Top Bottom