Dr. Slaa: Uongo ni dhambi na siko tayari kuishiriki!

Yericko,

Siasa ya unafiki sipendi. Nimenyamaza lakini naona mnazidi kunichokoza. Ni afadhali mngelikaa kimya kama nilivyonyamaza mimi. Uwongo wowote na upotoshwaji wowote sitauvumilia. Nitaukanusha hapo hapo. Hata kama una lengo lako ambalo silifahamu naomba sana usitumie jina langu. Nimefundishwa uwongo ni dhambi siko tayari kushiriki dhambi hiyo.

sina kikao chochote cha Secretariat sina mpango wowote ninaopanga kuwasilisha popote. Naomba watanzania wapuuze propaganda zote zinazofanyika kwa jina langu.

Ningehitaji kutuma taarifa yoyote kwa umma ningeliita Press Conference Mwenyewe au ningelitumia utaratibu wowote uliouliozoeleka.

Naomba kutoa onyo kwa mtu yeyote awaye, matumizi ya jina la Dr Slaa yakome.
Unahisi nini muda huu ambapo wale walikuwa wanakutusi kwa matusi yote mpaka ya nguoni na kukushambulia kwa kila namna ndio wamegeuka kuwa wafuasi wako!?. Naamini kabisa kuna mahala umeteleza japokuwa kuwa na msimamo tofauti na wenzako si dhambi.

Naamini kabisa kwenye hili si kutofautiana kimtazamo bali umeweka umimi zaidi (Ulitaka na ukaaminisha wewe ndiye utasimama kugombea urais). Hata kina Mbowe na Lowassa wana uchu wa madaraka ila hatua unazochukuwa wewe kisa umenyimwa nafasi si sahihi -nitapingana na wewe mpaka mwisho.

Wewe si mwadilifu hata kidogo kumnyooshea kidole Mbowe -Uzushi na uzindaki ulioshirikiana na Mbowe kuufanya dhidi ya Zitto utakutafuna mpaka unaingia kaburini. Unapaswa unyamaze kwasababu wakati unatumia mabavu kuwaaminisha uma kuwa Zitto ni msaliti na ukafanikiwa sasa ni zamu yako. Wewe ni mbadhilifu kama alivyo Mbowe hilo linajulikana na wanachadema,walifunika kombe mwanaharamu apite.

Soon your Legacy will vanish away, they will cut you down like grass.
 
Slaa kilichomuuma ni yeye kukatazwa kuchukua fomu. Alitaka washindane na Lowassa kidemokrasia. Sasa hivi wanahangaika kumpoza na ahadi.
 
Mahakama ndio chombo cha kutoa haki na kumtambua huyu ni fisadi na huyu si fisadi
mmempeleka mahakama gani kudhibitisha tuhuma zenu hizo?
acheni chuki binafsi.

Kwa hiyo pale Mwembeyanga Dr Slaa alikuwa anamsingizia? Basi sio fisadi mwambieni Dr amsafishe amuombe msamaha
 
acha aende tu kokote kule maana cc adui yetu ni ccm wala cyo mtu mmoja mmoja acha aende na umaarufu wake kwisha huwezi mlazimisha nae atakuwa alitaka urais tu huu ndo ibinasfi ambao hatutaki huwezi kaa na wenzio mkakibaliana tunamtakia kila la heri huko aendako

Kumbukeni Dr Slaa ndiye kakipigania chadema miaka mingi kwa shida na raha leo mnamdharau ghafla!! Mungu atawahukumu.
 
Huwa sina tabia ya kuweka topic yoyote kwenye jukwaa hili na pia hata nikiweka ni kwa mambo ya kawaida tu, ila leo nimelazimika kuandika ujumbe huu na kuuweka humu jukwaani, kwani ninaamini kwa dhati ya moyo wangu kuwa hii ndiyo njia pekee kwa mtu wa kawaida kama mimi ya kuwasiliana nawe binafsi.

Lengo langu hasa Dr. Slaa si kukushinikiza wala kukusumbua, najuwa ama una mambo mengi au umeamua kupunzika tu au vyovyote vile iwavyo, ila mimi binafsi na ninajuwa tuko watu wengi wenye mfano kama wangu ambao hatuelewi kile kinachoendelea kwako zaidi ya kusoma magazeti na mitandao hii ya kijamii ambavyo vyote hivyo haviwezi aminika kwa asilimia zote.

Hivyo kwa heshima nakuomba sana, kama ukiona vema na busara, ujitokeze hadharani na kutoa msimamo wako juu ya haya tunayoyasikia, maana wapo wanaosema umeamua kujiondoa ndani ya chadema, wapo wanaodai umeamua kupunzika tu na watu hao wanadai unataka kuachana kabisa na siasa na kwamba unataka kwenda Nchi nyingine kupumzika, na wapo wanaodai upo ndsni ya CHADEMA na unaendelea na kazi zako kama kawaida, hayo yote sisi watu wa kawaids tu, na ambao tunakuheshimu sana na kukutegemea sana na ambao tumejiandikisha kwa makusudi ili kupigia kura chadema baada ya kuridhika na uongozi wako na siasa zako, tunashindwa kuamua la kufanya.

Kwa ujumbe huu mzee wangu NAKUOMBA SANA TENA SANA!! jitokeze binafsi na kutoa msimamo wako juu ya hili ili sisi wengine pia tuamue la kufanya kwani wewe ndiyo dira yangu.

Samahani sana kama ujumbe huu utakuudhi au kukusabishia usumbufu wowote ule ila nia yangu ni kusikia KAULI yako iwe dira ya maamuzi yangu.

AHSANTE.
 
Sitaki kuamini kwa namna yoyote Ile kuwa Dr Slaa aliyepigania mabadiliko na mageuzi miaka 20 leo anaweza kuwavunja moyo wapiganaji wenzake hata kama wameshindwa kuelewana kwenye masuala kadhaa. Wanaomshauri kastaafu Siasa ni wale wenye malengo ya kumwangamiza kabisa na kumtumia kama daraja la wao kupita katika kipindi hiki kigumu kwao, Namshauri Dr Slaa asikubali kabisa kuwa daraja la utawala wa ccm kwa gharama yoyote Ile. Watanzania tutakukumbuka daima kama utafanya uamuzi wa kujali maslahi ya taifa na CHADEMA.

Nadhani nyie mliomkaribisha Lowassa ndio mmemvunja moyo.
 
Napata shida sana kuamini haya maneno kama kweli yanatoka kwa Dr hasa hiyo sentesi ya mwisho inayoishia na neno yakome!

Ila kama ni yeye basi tunaomba heri ila please and please Dr tunaomba usitudishe nyuma tena kwa miaka kadhaa hapa tulipo ni mahali pazuri sana kwa mustakabali wa taifa letu na vizazi vijavyo, tunaomba tuwe sehemu ya historia nzuri kwa taifa hili.

Huu ni wakati ambao adui yetu mkubwa tumeshamfahamu na kinachohitajika na umoja na mshikamano wa siku chache kutokea leo taifa hili lifunguliwe minyororo tuliyofungwa kwa miaka 50 iliyopita.

Naamini watanzania tumeteseka vya kutosha na tumemuomba Mungu pamoja mara nyingi tukiomba atunusuru kama taifa nadhani hii ni nafasi pekee aliyotupatia kwa kipindi hichi tulichokuwa nacho tusipowatoa sasa hivi tuwe pia tayari pia kuwavumilia miaka mingine 50 ya watoto wetu kukalia mawe shuleni,
Mama wajawazito kulala watatu mpka wanne kwenye hospitali zilizopo hapahapa mjini, sasa nashindwa kuelewa huko vijijini hali ipoje
Tunaokuomba eeh Mwenyezi Mungu atunusuru
 
Ni wiki inakaribia sasa kila mtu slaa kasema kasema ninachojua hajawahi kuongea na yeyote labda mbowe na wenzake wa kamati kuu so tumuache aseme mwenyewe anaondoka au anaunga mkono ccm kuondoka tuache viherehere
 
Kumbukeni Dr Slaa ndiye kakipigania chadema miaka mingi kwa shida na raha leo mnamdharau ghafla!! Mungu atawahukumu.
Dr Slaa amekwazwa akakwazika. Ufisadi ni mbaya sana. Maskini Padre wa watu. Heshima aliyokuwanayo imeporomoka poroooooooo
 
Tusipo kuwa makini ccm watatuvuruga mbaya Sana Mimi naomba tofauti ya dk na dr dkt
 
Back
Top Bottom