Dr Slaa: Tupo Makini kuliko CCM, Usalama wa Taifa....

Dr Slaa: Tupo Makini kuliko CCM, Usalama wa Taifa....

Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (CCM), ambaye alianza kwa kuwatuhumu viongozi wa Chadema, wamekuwa wakipanga kuua watu na wakati huo huo wakitaka wananchi wawape ridhaa ya kuongoza nchi.

Alisema pamoja na viongozi hao kuwa na tabia hiyo, wamekuwa wa kwanza kulalamika juu ya vitendo vyao na kwamba tabia hiyo ni sawa na mchawi ambaye akiroga mtu na kumuua, anakuwa wa kwanza kulia akionyesha uchungu alionao juu ya marehemu.



"Mheshimiwa Spika, kuna jambo ambalo limekuwa likiandikwa na kulalamikiwa na watu, kwamba ugaidi ugaidi. Katika jambo hili nawaomba Watanzania wasikilize kwa makini, kuna jambo lilitokea na jambo hili ni jambo la kigaidi, limeandikwa sana na kwa masikitiko linapotoshwa, yaani watu wanapotosha mpaka mambo yanayohusu maisha ya watu.

"Eti wanasema usalama wa taifa, mara wanasema polisi wanatesa watu, katika hili wala msihangaike na kwenye jambo hili hakuna polisi wala usalama wa taifa. Jambo la mkanda, aliyerekoki huo mkanda yuko tayari kusema kokote, aliyeniletea huo mkanda yuko tayari kusema kokote na mimi niko tayari kwenda kokote hata kama ni mbinguni.

"Chadema walipanga kuteka na kuua na huyu mwandishi walipanga kumuua eti wanadai picha ilitengenezwa, sasa kwa taarifa yenu hata pale alipokuwa anaongea, (akimaanisha Lwakatare), aliandika hata ile karatasi ninayo, ni hii hapa, fingerprint ni ya kwake, mwandiko ni wa kwake na vyote alivyokuwa anafanyia kazi vimepatikana na alisema atatoa ushahidi na mimi niko tayari kutoa ushahidi kokote iwe ni hapa na hata mbinguni nitakwenda," alisema Mwigulu akionyesha karatasi hiyo na kuongeza.

"Eti Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe), anasema anayewasiliana na gaidi eti naye aunganishwe na ugaidi, hebu fikirieni, yule aliyekuwa akipanga njama ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, kama ni viongozi, amewasiliana na viongozi gani kama siyo wakubwa zake ambao wamemwagiza kufanya hayo tena?

"Jitihada zinazoonyeshwa ambazo ni za kumtetea mtu hata kabla hajafika mahakamani, inadhihirisha ule ulikuwa ni mpango wa chama.

"Kwa kauli hii, ambayo ameandika kiongozi wa upinzani, viongozi wanaowasiliana nao waunganishwe katika kesi ya ugaidi kuanzia leo wakamatwe na polisi, hapa simuoni kiongozi wa Kambi ya Upinzani, labda wameshamkamata," alisema Mwigulu.

Katika mazungumzo yake, Mwigulu ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, alitaka Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, akamatwe kwa kuwa alihusika kumtetea Lwakatare.

Kwa mujibu wa Mwigulu, aliyekuwa akipanga njama za ugaidi huo ni mwanachama wa Chadema na kwamba fedha zilizotumika katika kufanikisha mpango huo, ni za chama hicho.

"Mnasubiri nini polisi, mtu ameshaomba kuunganishwa mwenyewe katika kesi?"

"Mkishapanga maovu mnawahi kwenda kutetea kama vile mchawi ambaye akishaua, anawahi kwenda kulia na kugalagala msibani. Mimi kwenye hili suala la mauaji, nawaomba Chadema mfanye vitu viwili, kwanza kimbieni haraka zaidi kwenye makanisa ama misikiti mliyokaribu nayo ili mkatubu kuwa mmepanga kuwauwa watu wasio na hatia.

"Baada ya kuomba toba, mrudi kutubu kwa wananchi, yaani mnataka uongozi halafu unawaza kuuwa watu, look at you," alisema.
 
Back
Top Bottom