Dr. Slaa: Sitakula sahani moja na mafisadi

Dr. Slaa: Sitakula sahani moja na mafisadi

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
12,279
Reaction score
38,855
Kufuatia uvumi kuwa Edward Lowassa waziri mkuu aliyeng'oka kwa kashfa za ufisadi kutaka kuhamia UKAWA, Dr. Willbrod Slaa katibu mkuu wa CHADEMA amesema kuwa hayupo tayari kula sahani moja na mafisadi.

Akijibu tuhuma hizo Dr. Slaa amesema wazi kuwa CHADEMA na UKAWA hawapo tayari kupokea mafisadi kwani itakuwa ni kinyume kabisa na dhamira ya UKAWA ya kuwatumikia watanzania wanaotegemea mabadiliko makubwa.

"Watanzania wapo tayari kwa mabadiliko na wameonyesha nia ya dhati kutuunga mkono, hatupo tayari kuchafuka na mafisadi" amesema Dr. Slaa

Kutokana na hali halisi ilivyo mdani ya CCM, chama hicho kinatarajiwa kukumbwa na mgogoro mkubwa kutokana na msuguano mkali wa makundi mawili makubwa yanayowania urais huku kundi hasimu na Lowassa likiungwa mkono na rais Kikwete.

Lowassa tayari ametoa hotuba huku akiainisha vipaumbele vyake ambavyo vinaenda kinyume kabisa na ilani ya CCM mwaka 2015-2020 jambo linalohashiria kuwa ndani ya chama hicho hali si shwari.
 
porojo zako kayasema wapi hayo? mnajitahidi sana kuzuia lichama lenu lisipasuke sio?mimba imefika mizi tisa lazima mtoto atoke hai au mfu.......
 
Mbona umeleta habari isiyo na chanzo? Hayo maneno kayasema akiwa wapi? Tuwekee chanzo tuone.
 
hata kujikopesha na kujiuzia mali za umma ni ufisadi,kukiuka miiko ya imani yako kwa tamaa za kimwili ni ufisadi pia
 
Lowasa ameshaweka wazi asiyemtaka ndani ya ccm aondoke yeye hawezi kuondoka ccm anategemea atakuwa mgombea wa uraisi
Ccm lazima mtambue ikulu siyo pango mafisadi wala wodi ya wagonjwa.
VOTE FOR UKAWA.
 
Lowasa ameshaweka wazi asiyemtaka ndani ya ccm aondoke yeye hawezi kuondoka ccm anategemea atakuwa mgombea wa uraisi
Ccm lazima mtambue ikulu siyo pango mafisadi wala wodi ya wagonjwa.
VOTE FOR UKAWA.
Pale mbwa anapotaka kumfukuza Mwenye Nyumba ,,,,,ni taabu sana
 
Ina Maana wewe na mahakama zetu, ww una akili sana, mahakama zilitoa ufafanuzi na uamuzi kuwa Josephine tayari aliachana na mumewe, mzee mzima anayejua kulea kachukua, hakuna kosa, naamini sana mahakama zetu hasa kuu, slaa ni rais mtarajiwa ndo maana kila anapotoa hoja mbadala CCM wanaichukua
 
lowasa hawezi toka ccm kamwe. na amesema anayetaka kutoka na atoke.

Hata Zitto alisema hatoki Chadema. Lowasa akiendelea kuikosoa serikali atafukuzwa chama na ndiyo ccm itaimarika. Chadema sasa iko juu zaidi baada ya Zitto kufukuzwa.
 
Tunakujua vizuri Kamanda. We sema lini tukusindikize kuchukua form ya kuchukua dola...
 
Dr. Slaa ni FISADI MZINIFU...

Kapora mke wa mtu, na kamtelekeza mke wake Rose kamili, na watoto alio zaa nao...Dr. Slaa hafai, mchafu na hafai kuwa kiongozi sbb familia yake kaitelekeza, na Rose kamili hadi leo analaani, haamini babu wa makamo ya Slaa, kuacha familia ikiteseka, ana roho mbaya sana hiki kibabu...Upadre ulimshinda sbb ya hii tabia chafuu...!!!

CCM hawezi itoa madarakani, anaota nn, au wakati anaongea alikuwa na mzinifu mwenzake J...

Slaa sio kiongozi, hata kanisa lilimfukuza, hafai... kanisa la RC ndio mahala maadili ya ukweli yaliko...kama kanisa lilimshindwa, nani atamweza..!!? atuondolee usiku hapa...!!!
 
Duh hii wala haitaji Dr kulisema mbona dhahiri kabisa kushiriki na fisadi na kujifua.

Kwani hata kujua hili inahitaji akili ya PHD?
 
Ina Maana wewe na mahakama zetu, ww una akili sana, mahakama zilitoa ufafanuzi na uamuzi kuwa Josephine tayari aliachana na mumewe, mzee mzima anayejua kulea kachukua, hakuna kosa, naamini sana mahakama zetu hasa kuu, slaa ni rais mtarajiwa ndo maana kila anapotoa hoja mbadala CCM wanaichukua

BUGORORA:

Kwa nyongeza ni kwamba suala kuoa na kuolewa kwa mtu yeyote sio issue ya kitaifa. Taifa letu halijashindwa kuendelea kwa miaka 50 kwa sababu watu wameoana na kuachana au kwa sababu fulani kamfumania fulani. Lakini ni ukweli wa mchana kweupe kuwa nchi imeshindwa kupiga hatua kwenda mbele sababu ya mafisadi.
 
Back
Top Bottom