Elections 2010 Dr Slaa ni Presidential Material wa Kweli

Mo-TOWN

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,721
515
Sikuwahi kubahatika kuhudhuria mkutano wowote wa mgombe urais kwa chama cha CHADEMA Dr Wilbrod Slaa. Kupitia ITV nimepata fursa nzuri sana kuweza kumsikiliza akinadi sera za CHADEMA na mustakabari wa nchi hususani ktk nyanja ya kiuchumi na kisiasa.

Ukweli ni nimefarijika sana kuwa huyu bwana ni Presidential Material. I am impressed, ameongelea maswala ambayo ni strategic kwa maendeleo ya nchi. Kwa mfano ukubwa wa serikali na marekebisho ktk mifumo ya kiutawala ambayo inapelekea viongozi kutowajibika kwa wananchi. :thumb:
 
Huyo ndo rais wetu mbadala, kazi kwako ndugu kuwaambia na wengine. Tunaomba uwe mjumbe kwa watu wenye mioyo migumu hawa wapo wengi sana hawataki kusikia, na wanahisi ni mtu wa aina ya ajabu. lakini ni kama ulivyomsikia anazungumzia mambo ya maendeleo ya kweli tu.
Lakini nasikitika kwa kuwa wapo watu wengi wanaosema serfa zake hazitekelezeki na hata akichaguliwa naye ataweza kuwa mbaya zaidi ya JK
Tafadhali tuwe wajumbe kwa mtu mmoja mmoja waelewe.

Watanzania wengi hawaelewi sera nzuri alizonazo wanafikiri ni kama wale wa ccm kutafuta KULA badala ya KURA
Sambaza sifa hizi za Slaa kwa wengine tafadhali
 
Ndugu yangu ndio maana akina kikwete na chama chao waligundua mapema kuwa Dr. slaa wakijaribu kujibizana nae kwenye midahalo atawalaza chani. Ndio maana wakaamua kujitoa kabisa ili waendelee kuwadanganya watanzania kwenye majikwaa ambako hawana nafasi ya kuwauliza maswali. Watanzania tukishindwa kuitumia nafasi adimi ya kumchagua dr. Slaa kuwa raisi wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa tanzania itatuchukua miaka mingine kibao kumpata mtu kama Dr. slaa
 
Tumeshapanda juu ya mlima na nchi ya ahadi iko mbele yetu. Hatuna budi kufika huko kwani Musa wetu Dk. Slaa yuko mbele yetu. Tusikubali kuendelea na utumwa ndani ya nchi yetu wenyewe chini ya ukoloni, ufedhuli na ujambazi wa CCM. Tuwahamasishe na kuwaelimisha mama zetu na dada zetu ambao mara nyingi wanatuangusha kwa kuendelea kuwapigia kura mabeberu ya CCM. Tukishindwa tarehe 31/10 kufanya maamuzi magumu kwa kuinusuru nchi yetu Mungu aliyoipendelea hata mawe iko siku yatakuha kuongea na kutusuta kwa upumbavu wetu kwa kushindwa kutambua kilicho bora. La sivyo tuwe tayari kubaki na umaskini wetu hadi YESU atakaporudi.
 
Naminia wenzagu. nasikitika atakosa kura yangu ila nimewacha wadau wanafanya mambo. Mungu awaongoze waTZ.
 
Nimewahi kuhudhuria mkutano mmoja wa kampeni wa Dr. Slaa na nikalinganisha na mikutano ya kampeni ya JK. kupitia Tv nikagundua tofauti kubwa sana.
1. Dr. Slaa anazungumzia masuala yake kwa kutaja vitu vya msingi na vichache sana bila kusoma mahali popote. JK. ninaona anazungumza vitu vitu ambavyo huwezi kujua kipi ni cha msingi. Mf. Dr. Slaa anaweza kuzungumzia juu ya uboreshaji wa huduma ya afya na Elimu na akaeleza kwa kifupi sababu ya serikali kufanya hivyo, namna ya kutekeleza hilo na muda wa kutekeleza. lakini ndugu Jk. akifika mahali akikuta Hospitali ambayo ina hadhi ya Hospitali Wilaya anaahidi kuwa hiyo itakuwa Hospitali ya Mkoa au ya rufaa.

Ukweli ulio wazi ni kuwa ama Jk anawaona Watanzania ni mbumbumbu au yeye ni mbumbumbu. Haiingii akilini kwa mfano kutuambia Hospitali fulani itakuwa Hospitali teule, wakati Dispensari imeshindwa kutoa huduma kama dispensari. Jk kama kiongozi wa serikali iliyopo madarakani anajua wazi kuwa haina maana kuipa Hospitali hadhi ya kuwa Hospitali kama hujaandaa madaktari wa kutoa huduma hiyo.

2. Uwezo wa Dr. Slaa ni mkubwa sana kuelewa kwamba wananchi wanahitaji nini na yeye kama mgombea anawaambia hilo tena kwa ufasaha na kwa hoja inayokubalika. Jk. haelewi kabisa watu wanatarajia nini kutoka kwake. Mfano: watu hawahitaji mgombea kuzungumzia ujenzi wa barabara inayojengwa wakati watu wanaiona kwa macho. Vile vile watu hawataki mgombea kuzungumzia vitu vinavyofanyika ambavyo vimetengewa bajeti ya serikali. Bajeti ya serikali inapitishwa mwaka hadi mwaka na wabunge wanahusika navo hvyo haina maana ya mgomea kuweka kwenye ahadi yake.

3. Dr. Slaa huwa anaweza kusema vitu anavyotaka kuwaambia wapiga kura bila kuhangaika kurejea kumbukumbu (data) zilizoandikwa. Jk. wakati mwingine husoma hutuba zake utafikiri anawasilisha hoja bungeni. Mgombea urais tena anayemalizia kipindi anashindwa hata kutambua kuwa wananchi hawahitaji uwingi wa ahadi na tarakimu nyingi bila sababu za msingi.

Natoa pole kwa Jk kwa kushindwa kujibu maswali ya msingi yaliyo katika vichwa vya wapiga kura na badla yake kuhangaika kuahidi vitu vingi kama ununuzi wa meli, viwanja vya ndege nk. vitu hivyo si hoja za kutosha kwamba wanachi wakuchague. Kitu cha ajabu ni kuwa itakuwaje endapo wagombea wengine nao wataahidi vitu kama hivyo? je, tumchague yule atakaye ahidi vitu vingi? JK akumbuke hata kama anaahidi mf. kujenga uwanja wa ndege ni wananchi ndiyo wanaojenga kwa kodi zao siyo yeye. Kutoka kwake watu wanataka dira na upeo alionao katika kuwaongoza wananchi.
 
Dr. Slaa amethibitisha kwa watanzania waliokuwa na shaka juu ya uwezo wake, kilichobaki ni sisi kumpa kura nyingi za kutosha kumuweka kwenye jumba la magogoni ili atubadilishie nchi hii kwani miaka 50 ya hawa ccm imethibisha wameshindwa.
 
Back
Top Bottom