Dr. Slaa ni mtanzania wa kweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa ni mtanzania wa kweli

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Felixonfellix, Sep 3, 2010.

 1. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Binafsi nimeipenda,
  Haya nawe endelea!!!!!

  MTANZANIA YEYOTE MZALENDO WA KWELI, MWENYE AKILI TIMAMU, ASIYE NA MTINDIO WA UBONGO, WALA MTUMWA WA HILA CHAFU, WALA UDUMAVU WA KIAKILI, TENA ASIYE NA UTANDO WA BUIBUI WALA TONGOTONGO ZA UFISADI MACHONI, WALA ASIYE MZEMBE WA KUFIKIRI, ANAALIKWA ASOME KWA UANGALIFU NA AZINGATIE MAKALA HII NA AWASHIRIKISHE NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI ZAKE POPOTE PALE WALIPO..

  DR SLAA YES WE CAN! HUYU NI MTANZANIA WA PILI BAADA YA NYERERE KUCHUKIA UFISADI KWA VITENDO. NI MTANZANIA WA PILI KUCHUKIA UMASKINI WA WATANZANIA KWA VITENDO. NI DR. SLAA ALIYESIMAMA NA KUTAJA MAJINA YA WALA RUSHWA NA MAFISADI. AKATAKA WALE WANAOPINGA WAMPELEKE MAHAKAMANI. HAKUNA ALIYETHUBUTU KUJITOKEZA KUMPELEKA MAHAKAMANI.

  NI DR. SLAA ALIYESIMAMA BUNGENI KUOMBA POSHO ZA WABUNGE KUPUNGZWA KUZIELEKEZA ZAIDI KWA WATANZANIA MASKINI. NI DR SLAA ALIYESIMAMA BILA WOGA KUNYOSHA VIDOLE KWA MATUMIZI MABAYA YA OFISI ZA UMMA. NI DR SLAA AMEKUWA MTANZANIA BAADA YA NYERERE KUTOA HOJA ZA NGUVU ZINAZOMLENGA KUMKOMBOA MTANZANIA MASKINI. MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA YAKO WAPI? AJIRA MILIONI MOJA ZIKO WAPI? HEBU MWENYE MBAVU ZA KUJIBU SWALI HILI AJIBU BILA UNAFIKI!

  NI DR SLAA ANAYEWEZA KUDHIBITI MATUMIZI MABAYA YA OFISI ZA UMMA. NI DR SLAA ANAYEWEZA KUWAPA ELIMU YA BURE WATOTO WETU PALE MLIMANI. ACHANA NA LONGOLONGO ZA CCM KUWATOZA USHURU WATOTO. WAULIZENI MAJUKWAANI WAO NYERERE ALIWATOZA ADA ? KAMA SI KUTAKA WATANZANIA WAENDELEE KUWA MAMBUMBUMBU NI NINI? KAMA SI KUTAKA WATANZANIA TUENDELEEE KUWA WATUMWA NI NINI?

  NI DR. SLAA ANAYEONGELEA TRENI YA UMEME KWENDA KIGOMA, DODOMA , TABORA, NA MWANZA.. WAULIZE MPANGO WAO CCM KAMA SI KUWAPA WAHINDI WANAOLETA MABEHEWA AMBAYO MABABU ZETU WALITUMIA WAKATI WA UKOLONI. SASA WAHINDI WANABAKI KUTUDANGANYA NA BAJAJI WAKATI VYUMA CHAKAVU VYA RELI SASA VINATUMIKA KUJENGA VYOO. HAWA HAWATUTAKII MEMA. HAWANA TOFAUTI NA AKINA CARL PETERS.

  NI DR SLAA ANAYEONGELEA MFUMKO WA BEI -NANI HAJAJUA DOLA LEO HII NI SAWA NA TSH 1500. UCHUMI UNADIDIMIA KWA KASI. AHADI NYINGINE ZA UONGO LUKUKI ZINATOLEWA TENA, WAKATI ZILE TULIZOAHIDIWA MWAKA 2005, HATA MOJA HAIJATEKELEZWA. WATANZANIA WALIO WENGI NA HASA WA VIJIJINI, WAMELALA USINGIZI. WANAFUMBULIWA MACHO, LAKINI WAMESINZIA BADO! WANATABASAMU, WANACHEKELEA NA KURIDHIKA NA VITISHETI VYA KIJANI NA VIKOFIA ZA NJANO. WAMEKWISHAZOEA SHIDA KIASI KWAMBA WANADHANI NI SEHEMU YA MAISHA YAO . EE MWENYEZI MUNGU, TUNUSURU NA HILI BALAA...

  NI DR.SLAA ANAWEZA KUZUIA WIZI WA MATRILION YA PESA KUTOKA MIGODI YETU YA BUZWAGI, GEITA, BULYANKULU, BUHEMBA, NYAMONGO, TULAWAKA, NZEGA NA TANZANITE. CCM WAMESHINDWA KWA SABABU NI WASHIRKA WAKUBWA NA WAMERUHUSU WIZI HUO. NI DR SLAA ANAEWEZA KUWALIPA WAFANYAKAZI ZAIDI YA SHILINGI 350.000 ACHANA NA CCM AMBAYO IMESHINDWA KUSIMAMIA MALIASILI AMBAZO ZINGELIWAPA WAFANYAKAZI KIMA CHA CHINI KINACHOKIDHI MAHITAJI YAO.

  NI DR.SLAA ANAYEWEZA KUSIMAMIA MASHIRIKA YA UMMA KULETA TIJA ACHANA NA CCM WANAOFYONZA MICHANGO YETU KULE, KWANI HAYA MASHIRIKA YAMESHINDWA NINI KUWAJENGEA NYUMBA WANACHAMA WAKE? MBONA KWINGINE YAMEWEZA?
  NI DR.SLAA ANAYEWEZA KUONGOZA NCHI BILA WOGA, KWA UTAWALA WA KWELI WA SHERIA BILA KUWAONEA WATU WALA BILA KULIPIZA VISASI. NI DR. SLAA AMBAYE AMEPANGA KUBADILI KATIBA ILI RAIS AFUATE MATAKWA YA WALIO MWAJIRI AMBAO NI WANANCHI. WAULIZE CCM HATA KAMA MTU KAIBA ANAPEWA MDA ARUDISHE PESA. HIVI INAINGIA AKILINI KWELI? UTAWALA WA SHERIA UKO WAPI?
  NAOMBA NIWAPE HEKO ITV KWA KUTUREJESHE KWENYE HOTUBA ZA MWALIMU. KATIKA HOTUBA YAKE MOJA ALISEMA WAZIRI MMOJA KULE UINGEREZA ALIANDIKWA KIDOGO TU GAZETINI JUU YA KASHFA, YULE WAZIRI ALIJIUZULU NA WAZIRI MKUU HATA HAKUMJIBU BALI ALITEUA MTU MWINGINE.

  CCM HAWAWEZI HAYO? ETI WANATAKA USHAHIDI. NANI KAWAMBIA RUSHWA TULE WAWILI HARAFU TUTOE VIELELEZO? TUNAIONA RUSHWA KWA MATOKEO YAKE. MATENGENEZO YA BARABARA YA BILION 200, BAADA YA SIKU MBILI IMEHARIBIKA. KWANINI USIMFUKUZE WAZIRI NA KATIBU WAKE WA WIZARA KWANZA ? CCM HAWAWEZI! ETI WANATAKA
  VIELELEZO!

  NI DR SLAA ANAYEWEZA KUFANYA HAYO. SI TUMEONA MNAZI MMOJA ALIVYOWATAJA MAFISADI WOTE! HAPO AKIWA NI MBUNGE TU! JE AKIWA RAIS SI WATAKIMBIA NCHI? JAMANI NAWAMBIA TUMPE MIAKA MITANO TU AWAKURUPUSHE MUONE MOTO UTAKAVYOWAKA..

  TUTAPATA DAWA, TUTAPATA SHULE ZA BURE, TUTAPATA MADAWATI. JAMANI HIVI KWELI KARNE YA LEO WATOTO WANASOMA WAMEKAA CHINI? WE MUST BE SERIOUS! HIVI KWELI DUNIA YA LEO WATU WANAVULIWA NGUO NJIANI KWENDA MWANZA, SHINYANAGA, TABORA, KIGOMA, MBEYA, LINDI NA MTWARA KWA SABABU YA USAFIRI WA MALORI?

  NANI ASIYE JUA MADAKTARI WETU WENGI BINGWA WAPO BOTSWANA KWA SABABU YA MAISHA DUNI TANZANIA NA HIVI KWENDA KUTAFUTA MAISHA BORA WAKATI HAPA KWETU WANANCHI MASKINI WANAKUFA BILA MADAWA? NANI ASIYEJUA MATATIZO YA UMEME, MAJI, MAKAZI, MARADHI, YANAVYOTUTESA? NANI ASIYEJUA WAKULIMA WETU WASIVYOKUWA NA MASOKO YA MAZAO YAO ? NANI ASIEJUA ASILIMIA 85 YA WATANZANIA WANATUMIA VIBATARI AU MAKOROBOI KAMA MWANGA? NANI ASIEJUA TUNAVYONYONYWA NA HAWA WAKOLONI WALIOKUJA KUCHUKUA KILA KITU??

  JAMANI WAFANYAKAZI, WAKULIMA, NA WANAFUNZI, KWA NINI MNALALA USINGIZI? KWA NINI MNAPIGA MIAYO YA NJAA WAKATI MAGHALA YETU YAMEJAA NAFAKA? NI AKILI GANI HII? NCHI YETU INAZO RASLIMALI ZA KUTUTOSHA, LAKINI WANAOZIFAIDI NI VIBAKA WACHACHE. MTALALA HADI LINI?

  NI DR SLAA MZALENDO WA KWELI, NA SIO KWA AJILI YA SIFA, ANAWEZA KUTUVUSHA TULIPO. NCHI HII NI MASKINI NA UMASKINI WENYEWE NI WA KUJITAKIA. TANZANIA NI TAJIRI TUNA KILA KITU - MITO , MAZIWA, NATIONAL PARKS, MIGODI, MAZAO YA MISITU, NA KILA AINA YA UTAJIRI. LAKINI TUKO MASKINI WA KUTUPWA! NAONA
  HURUMA NA UMASKINI WA KIFIKRA WA WATANZANIA.

  HIVI KUNA MTU HAJUI MAPOLISI WANALALA KWENYE VIBANDA VYA MABATI? HIVI KUNA AMBAO HAWAJUI MAPOLISI WATENDAJI WANALIPWA LAKI MOJA? WAMEKOSA NINI HAWA? NI AJABU! PAMOJA NA LAKI YAO MOJA UTAKUTA BADO WANATUMIKA KUWANYANYASA WATETEZI WAO. HATA MAASKARI AMKENI HIYO LAKI MOJA YENU HAINA TIJA HADI MRUBUNIWE KUWANYANYASA WAPINZANI AMBAO KIMSINGI WANAWATETEA NINYI! HIVI MAASKARI MNAYO MACHO YA KUONA? JAMANI TUACHE WOGA INAWEZEKANA! MBONA KENYA WAMEWEZA? MBONA MALAWI WAMEWEZA?MBONA ZIMBABWE WAMEWEZA? MBONA GHANA WAMEWEZA? KUFANYA MABADILIKO SAHIHI, INAWEZAKANA NA NAFASI NI HII TUITUMIE.


  TUMTUME DR SLAA ATUKURUPUSHIE WEZI WOTE NA ATUWEKEE KATIBA SAWA. HUO NDIO MSINGI WA YOTE. NI DR. SLAA ASIYEOGOPA KUWEPO NA MGOMBEA BINAFSI. CCM HILI HAWALIWEZI. WAMELIPINGA HADI MAHAKAMANI. WANATAKA WAO TU NDIO WAENDELEE KUTUTAWALA NA KUTUNYONYA.

  JAMANI 2010 HAKUNA KUDANGANYIKA! ENOUGH IS ENOUGH. ACHENI KUDANGANYIKA. WAKATI NDIO HUU. WATANZANIA MSIPOAMUA SASA, MTAMLAUMU NANI TENA? NAWATAMANI WATU WA KULE MARA -HAKUNA KURA INAIBIWA. ZOTE ZINASIMAMIWA. TUKIBADILIKA INAWEZEKANA, TENA NI RAHISI. PELEKE UJUMBE HUU KWA MARAFIKI, NDUGU, JAMAA, BABU NA BIBI YAKO KULE KIJIJI AMBAKO WANADHANI BADO NYERERE NDIYE RAIS WA NCHI HII. PELEKA UJUMBE HUU HARAKA KWA SIMU KAMA IPO, AU KWA NJIA YA POSTA, MRADI TU WALE JAMAA WALIOCHOKA KUISHI WASIIKWAPUE BARUA WAKIDHANI NI HELA..
   
 2. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,375
  Likes Received: 3,138
  Trophy Points: 280
  Rais mwafaka kwa wakati mwafaka.......dr.slaa ndiyo chaguo la wengi kwa sasa
   
 3. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,501
  Likes Received: 1,226
  Trophy Points: 280
  slaa the best,slaa the great, slaa for the future and prosperity of our nation go slaa go
   
 4. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  yes Dr.Slaa kwa mabadiliko ya kweli na ustawi wa taifa letu
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mmmh Felixonfelix uandishi wa herufi kubwa kwa taratibu za mtandao wa intaneti kunamaanisha una 'shout' .....are you shouting at us? :confused2:
   
 6. Wa Mjengoni

  Wa Mjengoni JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nukuu toka mwanzililishi wa thread...."WAMEKWISHAZOEA SHIDA KIASI KWAMBA WANADHANI NI SEHEMU YA MAISHA YAO . EE MWENYEZI MUNGU, TUNUSURU NA HILI BALAA.."

  Sasa ukiondoa la wizi wa kura, hili ndilo linayotumaliza Watanzania. Sio kwamba hakuna watu wenye dhamira ya dhati kabisa toka moyoni kutukomboa. Watanzania wengi masikini wameshaona wao ni wa hivyo hivyo tu, wanashindwa kuhusisha maisha yao ya kila siku na serikali iliyopo madarakani, vitu hivi ni mtu na mwanae, wao hawajui. Mungu atusaidie sana kwa hili.
   
Loading...