Wakuu tayari makamanda ameishaingia katika viwanja vya Nyamalango. Sasa ni utambulisho, katibu wa mkoa wa chama Mushumbushi anawatambulisha jukwaa kuu. Wenje, Highless, mbunge wa ukerewe, mzee Sylivester mwenyekiti wa baraza la wadhamini, mayor na naibu wake wa jiji la Mwanza, madiwani na viongozi wa SAUT. Sasa prof Mlambiti anamwaga cheche...anawaasa vijana kutolala, kupigania haki zao. Anasema ameingia CHADEMA kwasababu wanauongozi thabiti wasio na woga, anaongeza kwamba umasikini umezidi umekithiri tangu JK aingie madarakani. Thamani ya shs imeshuka....