Hiz thread nyingine bana, zimekaa kama zipo shule ya Vidudu..........
Ukisoma heading unaona mzinga wa habari na ndani unakuta PUMBA.
Mbona hata vidole vyako wewe mwenye vinapishana, sasa itakuwa watu wawili?
Hata Laptop zangu zinapishana, itakuwa Kikwete na Slaa?
Ningelikuwa Mod basi habari kama hizi nazifungia palepale hadi zitakapoandikwa na kuwa na Kichwa, kifua, tumbo na miguu.
Tukijua TOFAUTI zao kama TAIFA zitatusaidia nini? Kumbuka hapa tunajadili zaidi UTAIFA. Hizo za ana dini gani au ni Dr gani sisi hatujali sana. Tumeona akina Chenge na Degree zao za Havard, ndiyo wanafisadi taifa hili. Akina Prof. Mahalu wamekomba hela za nchi hii. Hivyo basi sasa tunaweka UTAIFA mbele na kuangalia kwanza mtu kalisaidia vipi taifa hili na si Dini yake, jina lake, elimu yake.......