Dr. Slaa kupanda kizimbani leo

Dr. Slaa kupanda kizimbani leo

kyalankota

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2014
Posts
2,594
Reaction score
1,463
Moshi. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibroad Slaa, leo anatarajiwa kupanda kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Hai kutoa ushahidi katika kesi ya jinai inayomkabili kijana aliyejifanya Jaji Mkuu mstaafu Barnabas Samatta.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Hai, Dennis Mpelembwa alisema jana kuwa Dk Slaa amethibitisha kuitikia wito huo wa Mahakama.

Katika ushahidi uliotolewa mahakamani, Dk Slaa akiwa Mtendaji Mkuu wa Chadema, ndiye anayedaiwa kushughulikia suala la mshtakiwa kutaka kuwatapeli viongozi wa Chadema.

Tayari Jaji Samatta na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wamekwishatoa ushahidi wao katika kesi hiyo inayoendeshwa na mawakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Katika ushahidi wake, Jaji Samatta alikana kumfahamu mshtakiwa Abeid Adam Abeid (22) na kwamba namba ya simu iliyotumiwa kujitambulisha kwa Dk Slaa na Lema kuwa ni Jaji Samatta siyo yake.

Kwa upande wake, Lema alidai mshtakiwa huyo alimtumia meseji mbalimbali akijitambulisha kwake kuwa ni Jaji Samatta na kwamba angemsaidia katika rufaa yake ya kuvuliwa ubunge ya mwaka 2012.

Upande wa mashtaka, ukiongozwa na Wakili wa Takukuru, Susan Kimaro ulidai mshtakiwa alitenda kosa hilo kati ya Aprili na Mei 2012. Mtuhumiwa alikana mashtaka hayo na leo upande wa mashtaka unatarajiwa kufunga ushahidi wao baada ya Dk Slaa na shahidi mwingine ambaye hajatajwa, kutoa ushahidi wao.

Chanzo:Mwananchi
 
Kwanini asikamatwe pia kuhusu ile kesi yake ya kuiba mke wa mtu?
 
Kwanini asikamatwe pia kuhusu ile kesi yake ya kuiba mke wa mtu?

vijana wa ccm huwa mnanifuraisha sana mlivyo wajinga!
Lakini mbona mkiambiwa mumtaje mume wa huyo mke hamumtaji?? Tuwaeleweje sasa??
 
Dah! Mie nilidhani anafikisha mahakamani na Mahimbo kwa kumpora mke wake!
 
lini ulisikia mwanamke anaibiwa?mwanamke kama hakupendi basi....hawang'ang'aniwi,uking'ang'ania umeumia.....

Mkuu we achana nao hao maana mwisho watatupeleka kwenye mambo ya Babu Seya bure.
 
Mi nilidhani ni ile kesi aliyofunguliwa na Rose Kamili ya kutelekeza watoto bila matunzo yoyote
 
Aiseee..., midubwasha ya ccm inachekesa kweli, Yaani mtu mzima na akili zako timamu huku dushelele linasimama unasiamama mbele za kadamnasi eti unalalamika kuibiwa Mke..??!!!

What a joke...!!! We utakuwa shoga si bure ningekuwa mimi napiga kimya, Ni aibu kupindukia kwa mwanamume rijali kulalamika kuibiwa mwanamke.

Ni sawa na mwanamume kusimama mbele ya wakwe zako UCHI na lipododo lako huku dushee ikiwa imesimama..!!! aibu sana.

BACK TANGANYIKA
 
Ushauri wa bure.Mtoa mada jifunze kuandika vizuri. Ungeamdika "Dr. Slaa kutoa ushahidi mahakamani" na sio "Dr. Slaa kupanda kizimbani" take that!!


BP
 
Back
Top Bottom