Dr Slaa kulakiwa Kigoma kwa Maandamano.

Status
Not open for further replies.

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA mkoa wa Kigoma kinaandaa mapokezi makubwa siku ya Alhamisi tarehe 8.12 wakati Katibu Mkuu wake Dr Wilbroad Slaa atakapowasili kwa ziara ya siku nane.

Katika manispaa ya hapa Kigoma matawi mbalimbali yameanza maandalizi ya kumpokea kiongozi huyo baada ya kupokea taarifa rasmi za ujio wa kiongozi huyo.

Viongozi kadhaa wa matawi wakizungumza wamesema wanataka kumpokea Dr Slaa kwa maandamano makubwa kama ishara ya imani ya wanachama wa Chadema Kigoma kwa uongozi wa chama chao.

Pia wamesema lengo lingine la maandamano hayo ni kuonyesha kwamba wanaheshimu maamuzi ya Kamati Kuu na kwamba wanaKigoma wanakipenda chama na siyo watu binafsi.

Dr Slaa anaanza ziara ya siku 8 mkoani Kigoma kuanzia tarehe 5.12 hadi tarehe 13.12 ambapo anatarajiwa kutembelea majimbo yote.

-------------------------

Naona babu atachoka kabla hata ya huo uchaguzi wenyewe 2015 kwa safari, manake badala ya M4C sasa ni safari za kuzunguka nchi nzima kujieleza kwa nini wamemfukuza Zitto na Kitila

Wewe mwenyewe kutoka UK ulikuwa wa kwanza kusajili defence ya Zitto. Wee inakuhusu nini? Wewe ni CCM safari za CDM zinakuhusu nini?
 
Naona babu atachoka kabla hata ya huo uchaguzi wenyewe 2015 kwa safari, manake badala ya M4C sasa ni safari za kuzunguka nchi nzima kujieleza kwa nini wamemfukuza Zitto na Kitila

pole xana bwana lukos, jiandae kuzikosa buku 7 baada ya 2015.
 
WanaKigoma ni watu wa mabadiliko, wanamshangaa Zitto fedha zinamfanya auze utu wake

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
By Chris Lukosi

Naona babu atachoka kabla hata ya huo uchaguzi wenyewe 2015 kwa safari, manake badala ya M4C sasa ni safari za kuzunguka nchi nzima kujieleza kwa nini wamemfukuza Zitto na Kitila

Kafie mbali huko.......................
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…