Dr Slaa kulakiwa Kigoma kwa Maandamano.

Status
Not open for further replies.

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA mkoa wa Kigoma kinaandaa mapokezi makubwa siku ya Alhamisi tarehe 8.12 wakati Katibu Mkuu wake Dr Wilbroad Slaa atakapowasili kwa ziara ya siku nane.

Katika manispaa ya hapa Kigoma matawi mbalimbali yameanza maandalizi ya kumpokea kiongozi huyo baada ya kupokea taarifa rasmi za ujio wa kiongozi huyo.

Viongozi kadhaa wa matawi wakizungumza wamesema wanataka kumpokea Dr Slaa kwa maandamano makubwa kama ishara ya imani ya wanachama wa Chadema Kigoma kwa uongozi wa chama chao.

Pia wamesema lengo lingine la maandamano hayo ni kuonyesha kwamba wanaheshimu maamuzi ya Kamati Kuu na kwamba wanaKigoma wanakipenda chama na siyo watu binafsi.

Dr Slaa anaanza ziara ya siku 8 mkoani Kigoma kuanzia tarehe 5.12 hadi tarehe 13.12 ambapo anatarajiwa kutembelea majimbo yote.


-------------------------

TAMKO LA KIKAO CHA MKOA – CHADEMA
PAMOJA NA BAADHI YA VIONGOZI WA MAJIMBO NA HII NI TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI




  1. Kikao kilichofanyika ofisi ya Mkoa Ujiji kilibeba AGENDA ya Kujadili na Kuboresha ujio wa ziara ya Katibu Mkuu (T) Dr. P. Slaa Mkoani Kigoma 5/12/2013


- Ambapo atatembelea majimbo yote 8 ya mkoa Kigoma kwa mikutano si chini ya miwili kwa kila jimbo na baadae mkutano wa mwisho, jioni Mkutano ufanyike makao Makuu ya Jimbo. Lengo likiwa kuangalia uhai wa chama.- Mambo makuu na muhimu yalizingatiwa- Usalama kwa Kiongozi huyo kufutia sakata la Maamuzi ya kamati kuu dhidi ya Mhe.Zitto na mapokeo ya wanachama wetu.
- Kutoa taarifa rasmi kwa majimbo na kupokea hali ilivyo au inavyoonekana katika maeneo yao.-Baada ya Tafakuri ya kina na ya Hekima na Busara pevu katika ujio huo iliazimiwa ifuatavyo
i. Mkoa uliomba Taifa lihairishe na kusogeza mbele tarehe ya ziara hiyo muhimu kwa mkoa wetu, ili Mkoa kama ngazi ya chini ya Kanda na Taifa uwezekwenda katika majimbo hayo na kuwaelimisha wanachama na wapenzi wetu juu ya kuheshimu na kuwa na nidhamu na maamuzi yatolewayo na ngazi ya juu yetu. Hata kama yanamaumivu ….katiba yetu ifuatwe katika kutatua tatizo – Maoni ya Wengi Mkoani na Viongozi wa Chama ni kuudhiwa na maamuzi ya k/kuu ambayo dhahiri yalilenga kumilika Zitto – Kisiasa.
ii. Mkoa ulitishika na vitisho baada ya kupokea taarifa toka kwa baadhi ya viongozi wa majimbo ya mkoa kwa hali ya usalama si nzuri kwa ujio wa kiongozi wetu Dr. Slaa kufika Kigoma kwa kipindi hiki wakati wanachama na wapenzi wakitafakari na kwa kauli tofauti zisizolenga kuwepo usalama.

iii. Kwa hekima ya kikao kilijiridhisha kwa kupata maoni toka katika majimbo 6 kuwa hali ni mbaya kabisa wakishauri Katibu mkuu asogeze mbele ziara yake kupisha mtafaruku huu na kwa usalama wa Chadema na viongozi wake Kitaifa.

iv. Hivyo Mkoa kupitia kikao hicho kuwa ni bora kuzuia kuliko kutibu, tayari sintofahamu zimeonekana, viongozi na hasa wa majimbo kutofautiana mitazamo ni HATARI katika hali hiyo. Mkoa ulijiridhisha usalama hautakuwepo kwa ujumla hata kama baadhi ya majimbo yakisema wao wapo salama tu.
v. HOFU/TAHADHARI - Endapo hali haitokuwa salama Mungu apishe mbali.
Mkoa hautokwepa lawama na Uzembe wa makusudi kwani wajibu wa ngazi ya chini ni kutoa ushauri kwa ngazi ya juu. Hivyo mkoa unatoa ushauri kwa Makao Makuu (T) Chadema kusogeza mbele ziara hiyo hadi hali itulie na mkoa upite majimboni kujiridhisha na usalama kwa viongozi wake na hasa wa Taifa.

LENGO KUU: NI KUHAKIKISHA CHADEMA TUNAPITA SALAMA KATIKA WAKATI HUU MGUMU KWETU – CHADEMA


Asanteni




ALHAJ. JAFARI KASISIKO MSAFIRI WAMALWA

M/KITI MKOA 01/DEC.2013 KATIBU MKOA
0756439200 0786448443
0714439200 0756448442




CHADEMA MKOA KIGOMA


 
Naona babu atachoka kabla hata ya huo uchaguzi wenyewe 2015 kwa safari, manake badala ya M4C sasa ni safari za kuzunguka nchi nzima kujieleza kwa nini wamemfukuza Zitto na Kitila

Wewe mwenyewe kutoka UK ulikuwa wa kwanza kusajili defence ya Zitto. Wee inakuhusu nini? Wewe ni CCM safari za CDM zinakuhusu nini?
 
Naona babu atachoka kabla hata ya huo uchaguzi wenyewe 2015 kwa safari, manake badala ya M4C sasa ni safari za kuzunguka nchi nzima kujieleza kwa nini wamemfukuza Zitto na Kitila

pole xana bwana lukos, jiandae kuzikosa buku 7 baada ya 2015.
 
WanaKigoma ni watu wa mabadiliko, wanamshangaa Zitto fedha zinamfanya auze utu wake

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
quote_icon.png
By Chris Lukosi
Naona babu atachoka kabla hata ya huo uchaguzi wenyewe 2015 kwa safari, manake badala ya M4C sasa ni safari za kuzunguka nchi nzima kujieleza kwa nini wamemfukuza Zitto na Kitila

Kafie mbali huko.......................
 
Status
Not open for further replies.
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom