Hivi na wewe ni mchuuzi wa huo upuuzi kwamba eti mbunge afanye siasa jimboni kwake tu? fine, umetolea mfano wa Mbowe. Mbowe ni mwenyekiti wa chama cha siasa chenye nguvu hapa nchini, bungeni anapewa hadhi inayoendana na ya Waziri Mkuu, ambaye ni Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni. sasa huyo kwa mujibu wa katiba, ambayo inahakikisha uhuru wa kujumuika na uhuru wa kueleza mawazo kwa mtu yeyote, lakini kwake Mbowe, kwa mujibu wa sheria ya vyama vingi, amehakikishiwa uhuru wa kufanya kazi ya siasa katika mipaka ya Jamhuri ya Muungano, ikiwa ni pamoja na Zanzibar. unakumbuka kwamba sheria yetu inalazimisha kwamba chama cha siasa lazima kiwe na sura ya muungano. sasa hiyo amri ya kuzuia wanasiasa wasifanye kazi yao, eti watakwamisha wale waliochaguliwa kutekeleza majukumu yao, inasimama katika vifungu gani vya katiba, na sheria ipi?
Ni kwamba, chama chenu kinatetemeka sana kusikia mtu wa upinzani anaunguruma mtaani. kama siyo hivyo kwa nini mnawazuia? mna yepi ya kuficha? na mko tayari kuvunja sheria na kutumia ubabe?