Hata kama Dr Slaa angekuwa ni mzaliwa au mkazi wa Igunga, tayari ana majukumu muhimu zaidi kuliko kuliongoza jimbo la Igunga au kuwa mbunge wa jimbo lolote lile. Dr Slaa hana uchu wa madaraka kiasi hicho, ni kiongozi shupavu mwenye uwezo na nia ya kweli ya kuleta maendeleo Tanzania. Makamanda wa CDM waliopo bungeni cheche zao zinatosha kuwasha moto nadhani wote mnashuhudia, Dr Slaa aendelee tu na kuuchochea moto wa mabadiliko kupitia elimu ya uraia tena yenye hamasa kwa wananchi nchi nzima.
Miaka minne iliyosalia ni muda tosha kwa CDM kuhakikisha wananchi wamehamasika vya kutosha kuing'oa CCM kwenye utawala wa nchi hii. Kwa mwendo huu, wabunge 2015 majority watakuwa wapinzani!