Dr Slaa kanikumbusha siku Mwangosi anauawa!!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,305
33,924
Siku Daudi Mwangosi anauawa ni wakati huo mimi nilikuwa ni Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Iringa. Nakumbuka siku ile nilikuwa na mazungumzo mafupi na Mwangosi pale kwenye Hoteli ya M.R kuhusu kunipatia kitabu cha " The Shackled Continent" kilichoandikwa na Robert Guest ambacho alikuwa ameazimwa na rafiki yetu mwingine Andrew Mwakibete. Masaa machache baadaye ililetwa taarifa kwamba Mwangosi kauawa.

Lakini jana yake mimi na Benson Kigaila Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa CHADEMA, tulikuwa kwa RPC kupeleka taarifa kwake kwamba Katibu Mkuu hakubaliani na kuzuiwa kwa mkutano wake wa Nyololo ambao ulikuwa umefuata sheria zote ikiwamo kutoa "Notice" kwa Ma-OCD wa wilaya zote itakapofanyika mikutano hiyo, na mimi kama Katibu wa Mkoa nilimwandikia RPC taarifa ya mikutano hiyo nikiambatanisha na ratiba yake.

RPC alisema kwamba kwa kuwa kuna zoezi la Sensa linaendelea basi mikutano hiyo ikifanyika italivuruga zoezi hilo. Slaa aligoma kukubaliana na sababu hizo na kutoa mfano wa shughuli za kisiasa zilizokuwa zinaendelea Zanzibar kama uhalali wa CHADEMA na yenyewe kuendelea na mikutano hiyo.

Mimi nikiwa Katibu wa Mkoa sikuwahi kuomba kibali (Na wala sheria haisemi hivyo) cha kufanya mikutano ya ndani kwa kuwa haifanyiki usiku. Lakini ni DK. Slaa mwenyewe ndiye alikuwa anasisitiza kwamba sheria haitutaki kuomba kibali bali ni kutoa taarifa na mikutano ya ndani haihitaji kuomba kibali.

Leo Slaa kanikumbusha siku ambayo ilimchukua Rafiki yangu ambaye tulikuwa tuna baraza letu la kujadiliana na kubadilishana mawazo. Nakumbuka picha yake akitokea kwenye Mgahawa wa Zanjabil Mkabala na Hoteli ya M.R akiwa na Kamera yake mkononi na begi dogo kalining'iniza begani tayari kwa safari ya kwenda Nyololo. Alipouawa hadi nikatamani ningejua ningemzuia asiende Nyololo.

Ni kwa nini Slaa hakwenda Nyololo na kama waandishi wa habari walikwenda Nyololo ilitarajiwa iandikwe habari ya nani wakati Mwenye mkutano mwenyewe hakuwepo. Jee wakati wana CHADEMA wengine wanakwenda Nyololo Dr.Slaa alijua kwamba mkutano ule ulikuwa umezuiwa na kama alijua ni kwa nini alilazimisha ukafanyike?

R.I.P Daudi Mwangosi

CC:
Dr. Willibrod Slaa
 
Kwanini umekumbuka leo baada ya Slaa kuondoka CDM?
Unaelewa maana ya kukumbuka? Ni lazima kuwe na mambo mawili. La kwanza ni lazima tukio liwe limetokea zamani na la pili lazima kuwe na tukio ama wazo linahusianisha na tukio lile la zamani na wakati uliopo ili kuamsha hisia!
 
Sawa.

Leo Dr. Slaa ni adui wa CDM na mzee Lowasa na kipenzi cha wana CDM.

Siasa na UNAFIKI damudamu milele.
 
Siku Daudi Mwangosi anauawa ni wakati huo mimi nilikuwa ni Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Iringa. Nakumbuka siku ile nilikuwa na mazungumzo mafupi na Mwangosi pale kwenye Hoteli ya M.R kuhusu kunipatia kitabu cha " The Shackled Continent" kilichoandikwa na Robert Guest ambacho alikuwa ameazimwa na rafiki yetu mwingine Andrew Mwakibete. Masaa machache baadaye ililetwa taarifa kwamba Mwangosi kauawa.

Lakini jana yake mimi na Benson Kigaila Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa CHADEMA, tulikuwa kwa RPC kupeleka taarifa kwake kwamba Katibu Mkuu hakubaliani na kuzuiwa kwa mkutano wake wa Nyololo ambao ulikuwa umefuata sheria zote ikiwamo kutoa "Notice" kwa Ma-OCD wa wilaya zote itakapofanyika mikutano hiyo, na mimi kama Katibu wa Mkoa nilimwandikia RPC taarifa ya mikutano hiyo nikiambatanisha na ratiba yake.

RPC alisema kwamba kwa kuwa kuna zoezi la Sensa linaendelea basi mikutano hiyo ikifanyika italivuruga zoezi hilo. Slaa aligoma kukubaliana na sababu hizo na kutoa mfano wa shughuli za kisiasa zilizokuwa zinaendelea Zanzibar kama uhalali wa CHADEMA na yenyewe kuendelea na mikutano hiyo.

Mimi nikiwa Katibu wa Mkoa sikuwahi kuomba kibali (Na wala sheria haisemi hivyo) cha kufanya mikutano ya ndani kwa kuwa haifanyiki usiku. Lakini ni DK. Slaa mwenyewe ndiye alikuwa anasisitiza kwamba sheria haitutaki kuomba kibali bali ni kutoa taarifa na mikutano ya ndani haihitaji kuomba kibali.

Leo Slaa kanikumbusha siku ambayo ilimchukua Rafiki yangu ambaye tulikuwa tuna baraza letu la kujadiliana na kubadilishana mawazo. Nakumbuka picha yake akitokea kwenye Mgahawa wa Zanjabil Mkabala na Hoteli ya M.R akiwa na Kamera yake mkononi na begi dogo kalining'iniza begani tayari kwa safari ya kwenda Nyololo. Alipouawa hadi nikatamani ningejua ningemzuia asiende Nyololo.

Ni kwa nini Slaa hakwenda Nyololo na kama waandishi wa habari walikwenda Nyololo ilitarajiwa iandikwe habari ya nani wakati Mwenye mkutano mwenyewe hakuwepo. Jee wakati wana CHADEMA wengine wanakwenda Nyololo Dr.Slaa alijua kwamba mkutano ule ulikuwa umezuiwa na kama alijua ni kwa nini alilazimisha ukafanyike?

R.I.P Daudi Mwangosi

CC:
Dr. Willibrod Slaa
Jesuit.......

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Dr Slaa ana upande wake sasa naona asiseme hana chama ni bora akaeleweka yuko wapi moja kwa moja.

Hii ni mara ya pili nasoma maandiko yake la kwanza ni lile kama sijakosea lilikuwa ni la kukubaliana kutokukubaliana.

Pesa tamu bhana keshafyata vilivyo na ameungana na wale wazee wa kusifu tu.

Kila nikionaga picha ya mwangosi na yule askari mpiga bomu roho inaniuma sana.
 
Back
Top Bottom