DR SLAA UMEKUWAJE TENAAAA?????
hakuna ubishi kwamba Dr Slaa amefanya kazi kubwa kuijenga Chadema, pamoja na viongozi wengine Kina Mbowe, Lisu, Mnyika na wengineo wengi.
Na Dr Slaa aelewe pia kuwa kuna wengine walimpisha yeye kugombea uraisi kwa Chadema hapo kabla kwasababu walijua alikuwa na ushawishi mkubwa kuliko wao. vyama vingine vingi wanaogombea uraisi ni wenyeviti, Mfano CUF lipumba amegombania mara kadhaa; inamaana Mbowe hakutanguliza ubinafsi kung'ang'ania kugombea uraisi bali awepo anayegombea mwenye ushawishi ili chama kikue. na hilo Limefanikiwa
Sasa amekuja mwenye ushawishi Zaidi ndio maana Ukawa kwa ujumla wakaona wasimame nyuma ya Lowassa kimkakati kupata kura za Ukawa pamoja Na CCM wengine wanaopenda mabadiliko.
Sasa Chuki za Slaa zinatokana na Nini? kwanini Dr Slaa asitangulize kwanza maslahi ya Taifa kuiondoa kwanza CCM halafu mengine baadae?
Mbona yeye walimpisha?
Ushauri wangu kwa Dr Slaa, wananchi wanataka mabadiliko, Asaidie kupata mabadiliko hayo hata kama yeye binafsi hamuafiki Lowassa lakini tulio wengi tunaona fursa ni kubwa kwa Lowassa kuliko kwa Slaa na huo ni ukweli
Dr Slaa asingeweza kumshinda Dr Magufuli hata bila goli la Mkono. CCM wanalijua hilo, Ukawa wanalijua hilo, Dr Slaa mwenyewe nalijua hilo na wananchi wote tunalijua hilo.
DR Slaa usiwasaliti watanzania kisa kumfurahisha Mama Mushumbusi,
Dr Slaa ungana na watanzania wenzako kuleta mabadiliko katika mfumo wa uongozi wa Nchi ulioharibiwa na CCM. hilo ndio jukumu letu kama taifa kwa sasa.
Vinginevyo sifa zote ulizojijengea kwa miaka mingi zitapukutika, na Chadema pia kitaathirika.
Mwanafalsafa mmoja wa kichina aliwahi kusema nanukuu "YULE ANAYETOKA KWENDA KULIPA KISASI KWA MWENZAKE, KWANZA ACHIMBE MAKABURI MAWILI"
mwisho wa kunukuu