Ndugu waislaamu, na Watanzania wote kwa ujumla,
Awali yote napenda kutoa salaam za pekee kwa ndugu zetu Waislaamu ambao wanaungana na wenzao wa Dunia nzima kusherehekea sikukuu ya Eid baada ya kumalizia Mfungo Mtukufu wa Mwezi wa Ramadhan. Ni Imani yangu kuwa kutokana na Mfungo huo kila Muislam amepata Rehema zinazoambatana na Mfungo huo Mtukufu, lakini pia Nina Imani Taifa letu katika ujumla wake limenufaika na Rehema na Baraka za Mfungo huo Mtukufu. Tunamshukuru Mwenyeenzi Mungu kwa kila mmoja aliyejaliwa kufunga kumalizia Mfungo vizuri na kutekeleza nguzo hii muhimu katika Imani ya ki-Islamu.
Ninawatakia pia Watanzania wenzangu wote tuungane na ndugu zetu Waislamu kuungana kwa Upendo wa Mwenyeenzi Mungu katika kusherehekea sikukuu hii kwa Amani na Upendo Kama ilivyo desturi ya Watanzania. Kwa utamaduni wa kitanzania, tumezoea kusherehekea Sikukuu pamoja Kama ndugu, marafiki, majirani na jamii kwa ujumla. Hiki ni kipindi ambapo watoto wetu hutoka Mitaani wakicheza na kufurahia pamoja. Watoto wakila na kucheza pamoja kusherehekea sikukuu mbali mbali .
Ni Imani yangu kuwa sikukuu hii ya Eid itazidi kutuunganisha Watanzania kwa Upendo mkubwa na mshikamano, itatuleta pamoja kutafakari rehema za Mwenyeenzi Mungu na kutafuta namna ya kuondoa Tofauti zetu ndogondogo tukizingatia kuwa sisi sote ni viumbe wa Mwenyenzi Mungu! Ni kipindi cha kuonyesha Upendo wetu kwa wote wenye kuhitaji zaidi na kipindi cha kurejesha Amani na matumaini kwa walio katika hatari ya kukata tamaa katika maisha yao ya kila siku.
Nawatakia wote Heri ya Eid el Fitr.
Idd Mbarak!
Dr. W.P.Slaa
Good dr. Slaa
safi sana dkt slaa

Mnafiki sana huyu mzee, cdm na waislamu wapi na wapi?

Huyu Mzee hana undugu wa kweli na waislamu, kwahiyo hizi salamu zake ni za kinafiki!
Mkuu, kikwete mtu wa watu yule, inashangaza kuona leo slaa anawapenda waislamu wakati kwenye chama wanawatimua hovyo, au ndo gia za kutaka support ya UKAWA?Kalale huko msukule weye. Kimekuuma slaa kuwapenda waislamu sio. Wakati kikwete huwa anawatakia wakristo salam kwenye sikukuu zao kwani yeye anahusiano na wakristo. Una akili fupi kabisa. Kwanza inaonesha wewe ni mdini naturally
asante rais mtarajiwa
Huyu Mzee hana undugu wa kweli na waislamu, kwahiyo hizi salamu zake ni za kinafiki!
c.c the big show,faithfox
pisha wewe rais anaongea na waislam na watz wote
wapeni nafasi waislamu ndani ya chama ili tuwe na imani na myasemayo otherwise hii ni sawa na kumpaka mtoto uji mdomoni wakati umeunywa wewealafu wewe msalani ni mkristo nenda kanisani ukaombewe upone na huo udini wako ukuishe msukule weye