Dr Slaa awaanika Kikwete na CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Slaa awaanika Kikwete na CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Serayamajimbo, Dec 5, 2009.

 1. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #1
  Dec 5, 2009
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na Edward Kinabo na Janet Josiah

  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa Rais Jakaya Kikwete ameshiriki moja kwa moja kuvuruga uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji uliofanyika nchini kote hivi karibuni na kwamba kipo mbioni kumshitaki na serikali yake katika jumuiya ya kimataifa.

  Hayo yalisemwa jana na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willbrod Slaa, alipokuwa akitoa taarifa ya maamuzi ya kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho, mbele ya waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana.

  Dk. Slaa alisema Kamati Kuu ya chama hicho iliyokutana Desemba 2 hadi 3 jijini Dar es Salaam, ilijadili na kubaini kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji ulifanyika kwa utaratibu ambao ni wa kihuni na ni aibu kwa taifa na serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwani ulikwenda kinyume na kanuni za msingi za kidemokrasia na haki za binadamu, hivyo kutokuwa huru wala wa haki.

  “Tuna ushahidi wa kutosha wa mizengwe iliyofanyika na mbaya zaidi mkuu wa nchi, Rais Kikwete naye alishiriki moja kwa moja kwenye uhuni huo. Nina ushahidi wa maagizo yaliyotolewa na Kikwete mwenyewe kule Karatu. Siku mbili kabla ya uchaguzi, aliyekuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Karatu aliondolewa ghafla na kupelekwa mkurugenzi mpya ili akaisaidie CCM ishinde, kwa maagizo ya Kikwete mwenyewe.

  “Tutapiga kelele mpaka dunia nzima isikie, tutaendesha kampeni ya kuiambia jumuiya ya kimataifa ijue kuwa Tanzania hakuna demokrasia. Wajue kuwa hakukuwa na uchaguzi, kilichofanyika kwa kiasi kikubwa kilikuwa ni uhuni tu,” alisema Dk. Slaa.

  Akitoa mfano wa sehemu ya kile alichokiita uhuni, alisema wagombea wa CHADEMA katika wilaya 10 walienguliwa kwa sababu tu wasimamizi walilazimisha wagombea hao wateuliwe na ngazi ya chini kabisa ya chama hicho iitwayo msingi, ilhali kwa katiba ya chama hicho, msingi si ngazi ya uteuzi wa wagombea.

  Hata hivyo, alisema pamoja na uchaguzi huo kufanyika katika mazingira ya hovyo hovyo, kikanuni na kiusimamizi, bado CHADEMA imefanya vizuri zaidi katika uchaguzi huo ikilinganishwa na uchaguzi wa mwaka 2004, hali inayoashiria kuwa wanachama wake wanaongezeka na chama hicho kinakubalika.

  Aidha, alisema Kamati Kuu ya chama hicho imelaani hatua ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutangaza matokeo bungeni kabla ya kuwa na taarifa yenye matokeo kamili ya uchaguzi nchi nzima na kuielezea hatua hiyo kuwa ililenga kulipotosha Bunge na kuwapotosha wananchi kama sehemu ya propaganda za Serikali ya CCM kutaka kuonyesha kwamba inakubalika na Watanzania.

  “Hivyo Kamati Kuu inayatilia shaka matokeo ambayo yanaendelea kujumuishwa hivi sasa kwani yanaweza kubadilishwa kuendana na matokeo ambayo Waziri Mkuu alishayatangaza bungeni kabla ya kupokea matokeo ya nchi nzima,” alisema Dk. Slaa.

  Aliitaka serikali kuweka hadharani matokeo yote ikiwemo kwa kuyaweka katika tovuti ya serikali, kituo kwa kituo ili umma uweze kuyapitia na kuyajadili.

  Katika hatua nyingine, Dk. Slaa alisema tangu kupitishwa kwa sheria mpya ya vyama vya siasa 2009 inayomruhusu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukagua mahesabu ya vyama vya siasa, bado ameshindwa kuanza ukaguzi kwa sababu ya kuiogopa CCM, kwani ndicho kinachotumia vibaya fedha zake, ambazo ni nyingi kuliko za chama chochote cha siasa nchini.

  Alitoa mfano kuwa mwaka jana kuwa jumla ya sh bilioni 13 zilizotumika katika vyama vya siasa zilibainika kuwa hazikutolewa vielelezo vyovyote, hali inayoonyesha dhahiri kuwa chama kilichotumia fedha hizo bila kutoa vielelezo ni CCM kwani ndicho kinachopokea fedha nyingi.

  “Kwa bilioni hizo 13 unaweza kuona ni chama gani kilichotumia fedha zake bila kuwasilisha vielelezo, maana ukichukua fedha za CHADEMA na CUF hata ziwe za mwaka mzima, bado haziwezi kuzidi bilioni 1.5,” alisema Dk. Slaa.

  Alisema CHADEMA ipo tayari kukaguliwa na CAG kwani inasimamia uwazi na uadilifu na wabunge wa chama hicho ndio walioanzisha wazo la kutaka vyama vyote vya siasa vikaguliwe na mkaguzi huyo.

  Kwa upande mwingine, alisema kamati kuu ya chama hicho iliazimia kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kwa wadhifa wake, aendelee kuwa mtia saini kama sehemu za usimamizi wa kifedha uliopo kwenye taratibu za fedha za chama zilizopitishwa na vikao vya juu, licha ya shutuma zilizoelekezwa kwake na waliokuwa maofisa wa chama hicho, David Kafulila na Danda Juju hivi karibuni.

  Alisema pia CHADEMA itaendelea kuwakopa na kuwalipa wanachama wake mbalimbali kila inapobidi kwani ruzuku ya chama hicho kwa mwezi bado haitoshi kuendesha harakati za kisiasa na kuwataka wote wanaokituhumu chama hicho kwa kumlipa Mbowe madeni yake wakome, kwani chama hicho hakipo tayari kuamuliwa na watu wa nje jinsi ya kujiendesha.

  “Tutaendelea kulipa madeni ya Ndesamburo, Mbowe na ya mwanachama yeyote yule anayekikopesha chama. Hakuna mtu wa kutuamulia jinsi ya kutuendeshea chama chetu. Anayeona kuwa CHADEMA kuna ufujaji wa fedha aeleze akiwa na ushahidi.

  “Mwenye jeuri aeleze milioni 35 wanazosema zimetafunwa zilitoka wapi, kwa namba ngapi, tarehe gani na kwenda kwa mtu gani mwenye akaunti namba gani. Waseme kama Dk. Slaa nilivyosema wakati nilipoelezea jinsi fedha za Deep Green, Kagoda, Meremeta nakadhalika, zilivyoibwa Benki Kuu,” alisema Dk. Slaa.

  Akigusia mfumo wa uanachama na uchangishaji fedha kwa njia ya kieletroniki (E-membership), alisema tayari huduma hiyo imeshaanza kwa wateja wa mitandao ya Zain na Vodacom na kinachotakiwa ni kwa mtumiaji kutuma ujumbe mfupi (sms) wenye neno CHADEMA kwenda namba 15710.

  Chama hicho wiki ijayo kitaanza kufanya mikutano yake ya kujiimarisha, almaarufu Operesheni Sangara, itakayoanzia mkoani Shinyanga na kuenea nchi nzima, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwakani.

  Wakati huo huo, chama hicho kimelaani taarifa ya uamuzi wa serikali kwa kushirikiana na Baraza la Wadhamini wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wa kukataa kuongeza mkataba wa aliyekuwa Mhadhiri Mwandamizi chuoni hapo na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Profesa Mwesiga Baregu.

  Dk. Slaa alisema uamuzi huo una dalili za kumkomoa kutokana na msimamo wake thabiti wa kuikosoa serikali, kutetea umma na kuunga mkono CHADEMA.

  “Kamati kuu imelazimika kuamini hivyo kwa kuzingatia hali ya kisiasa nchini wakati maamuzi hayo yanafanyika, huku kukiwa na uhaba wa wahadhiri waandamizi kama yeye katika chuo hicho,” alisema Dk. Slaa. Alisema kilichomtokea Profesa Baregu ndicho kilichotokea kwa Dk. Masumbuko Lamwai, aliyekuwa kiongozi ndani ya Chama cha NCCR-Mageuzi ambaye aliamua kurudi CCM. Aidha, Dk. Slaa alisema CHADEMA imepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini na mmoja wa waasisi wa chama hicho, Kanali mstaafu Geofrey Marealle aliyefariki dunia juzi.
   
 2. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  hivi Dr Slaa ni Dr wa nini vile?, alifanya PHD wapi tena vile?, na ali research kitu gani vile?.....i wish niione thesis yake, maana jamaa anaonekana ni genious sana...
   
 3. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Watu waliosoma theology huwa ni vichwa. Wako deep sana. Haswa Catholic theology. PhD zao zinakuwa mara nyingi za Philosophy (sijui sasa ndio inakuwaje manake tayari PhD = Doctor of Philosophy)
   
 4. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #4
  Dec 6, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  PhD maana yake ni Permanent hand Damage! Huyu mheshimiwa PhD yake ilikuwa iana husu mambo ya siasa, literally, alikuwa permanently damaged kwenye politics ndo maana aliachana na upadri na kuungana na siasa (ambayo ndo inalipa kwa sasa bongo! teh teh..)[FONT=&quot][/FONT]
   
 5. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Divinity?
   
 6. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ,  Oh, yeah
  Thanks
   
 7. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #7
  Dec 6, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  I guess you meant head mkuu
   
Loading...