Dr Slaa atoa salamu za Mwaka mpya...

Dr Slaa atoa salamu za Mwaka mpya...

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa amelaani ubadhirifu na wizi wa mali ya umma unaoendelea serikalini.

Akihutubia waumini wapatao 70,000 katika mkesha wa mwaka mpya kwenye viwanja vya Kanisa la Ufufuo na Uzima vilivyopo Kawe, kiongozi huyo amesema maovu mbalimbali yanayotokea ni kwa sababu ya watu kumsahau Mwenyezi Mungu na kumgeukia Shetani.

Dr Slaa amesema ni aibu kubwa kwa Taifa kukumbwa na kashfa mbalimbali zikiwemo wizi wa Fedha za Escrow,Meremeta,Epa nk.

Kiongozi huyo mwenye ushawishi mkubwa nchini alialikwa na Kiongozi wa Kanisa hilo Mchungaji Josephat Gwajima kuwa mgeni Rasmi katika mkesha huo wa mwaka mpya.

Katibu Mkuu huyo pia alitumia nafasi hiyo kuwatakia Watanzania heri na baraka tele katika mwaka huu mpya wa 2015 wenye changamoto mbalimbali.

Hotuba ya Dr Slaa anayetarajiwa na wengi kuwa Rais wa Awamu ya Tano iliwapa hisia kali maelfu ya waumini hao na kukuta wakimshangilia kupita kiasi kila baada ya maneno machache.
 
Tuwekeeni video yake na sisi tuliombali tufaidike
 
10675702_10152943439914339_199039496563984524_n.jpg
 
!...Cc: Msalani, Ritz, Faizafoxy, Simiyu Yetu Etc. Tunasubiri Hapa Matusi Yenu
 
Slaa anatoa salamu kanisani slaa ni mdini sana
 
Hongera sana Dr Slaa. Karibuni vijana wa Mwigulu kwa matusi kama mnavyotakiwa kufanya mara tu mlionapo jina la Dr Slaa kwenye mitandao.

Wanachanganyikiwa na mapepo yanapanda likitajwa jina la Dr Slaa.
 
Haoni aibu madhambi yote haya aliyonayo hata kuongea mbele za watu.
 
Back
Top Bottom