Dr. Slaa athibitisha EPA ni ya Mkapa Arumeru. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa athibitisha EPA ni ya Mkapa Arumeru.

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Losambo, Apr 4, 2012.

 1. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  WanaJF katika kufunga kampeni za jimbo la Arumeru Dr. W. P. Slaa alizungumzia kashfa kubwa sana juu ya rais mstaafu Benjamin W. Mkapa alisema wapinzani ni vifaranga!!!! Kauli hiyo ilikuwa ni kejeli na dharau kwa wapinzani jambo ambalo Dr. W. P.Slaa aliona asilifumbie macho na kuamua kumlipua katika mkutano uliofanyika USA kabla ya kwenda kuhitisha kampeni katika viwanja vya Patandi USA ambapo ilikuwa ni funiko bovu kwa jinsi watu walivyoitikia wito.

  Hebu msikilize Dr. Slaa akimkaanga BWM.  Namshauri Mkapa kuachana na siasa ambazo hazina tija kwake hasa ukizingatia siyo kiongozi aliyekuwa msafi sana alipokuwa Ikulu yetu.

  Nawakilisha.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  WanaJF katika kufunga kampeni za jimbo la Arumeru Dr. W. P. Slaa alizungumzia kashfa kubwa sana juu ya rais mstaafu Benjamin W. Mkapa baada ya yeye kuwananga wapinzani kuwa vifaranga!!!! Kauli hiyo ilikuwa ni kejeli na dharau kwa wapinzani jambo ambalo Dr. W. P.Slaa aliona asilifumbie macho na kuamua kumlipua katika mkutano uliofanyika USA kabla ya kwenda kuhitisha kampeni katika viwanja vya Patandi Tengeru ambapo ilikuwa ni funiko bovu kwa jinsi watu walivyoitikia wito.

  Habari hii haikupata coverage kubwa lakini kama kawaida wanaJF tunajuzana, hatunyimani.

  Hebu msikilize Dr. Slaa akimkaanga BWM.  Namshauri Mkapa kuachana na siasa ambazo hazina tija kwake hasa ukizingatia siyo kiongozi aliyekuwa msafi sana alipokuwa Ikulu yetu. Akikaa kimya mchango wake katika taifa hili unaweza kuendelea kuheshimika.

  Nawakilisha.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  Mkapa ni fisadi hilo halina ubishi,nakumbuka kauli ya JK akimtetea Mkapa alisema TUKIANZA KUWASHITAKI MARAIS WASTAAFU BASI VIONGOZI HASA MARAIS WATAKUA WANANG'ANG'ANIA KUKAA MADARAKANI MILELE!!!
   
 4. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mwambie Slaa aende Mahakamani
   
 5. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mkapa ndiyo anatakiwa aende mahakamani kwa kudhalilishwa kuwa ni fisadi halafu huko ndiko kitaeleweka.
   
 6. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,652
  Likes Received: 21,867
  Trophy Points: 280
  Kwani yeye ni DPP?
   
 7. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Akafanye nini?
   
 8. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kwani kasema amedhalilishwa?

  Kama ana ushahidi kwanini asiupeleke mahakamani?

  Kwa katiba ya nchi inasemaje kuhusu mtu kumshitaki mwingine? inasema mpaka upitie kwa dpp?
   
 9. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #9
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Akashitaki kama anaona kuna kosana ana ushahidi
   
 10. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #10
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  JK aliposema wezi walioia EPA warudishe fedha zetu alikuwa mjinga? Nchi tatizo kubwa ni kubebana ndiko kunakotuhangaisha hata kama kitu kitu kipo wazi. Au unataka Lusinde atoke Mtera aje akueleze na hilo?
   
 11. T

  Taso JF-Expert Member

  #11
  Apr 4, 2012
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,649
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Kampuni ya Mr. and Mrs. Benjamin Mkapa, "TanPower Resources Limited, S.L.P 15 Luthuli Street, Dar-es-Salaam, ambayo ni Ikulu yetu."

  Nilidhani Ikulu iko mtaa wa Magogoni. Nafahamu anwani za marais wengine za 10 Downing Street na 1600 Pennsylvania Ave, n.k. lakini ya Ikulu ya nchi yangu mwenyewe siijui, aibu, you know? Nadhani tatizo ni poor media, hawaandiki vitu hivi. Sasa sijui hilo S.L.P 15 Luthuli Street ni plot namba ngapi.
   
 12. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #12
  Apr 4, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ipo siku wezi wote na wahujumu wa mali za nchi watafikishwa mahakamani, kwa hilo hakuna ubishi. Kwa sasa hivi bado hawajafikishwa kwa vile utawala wa sasa pamoja na vyombo vya dola vinawalinda. Pindi itakapokuja serikali yenye uongozi bora na yenye kufuata maadili, lazima watafikishwa mahakamani. Jambo hili ni lazima, hata kama itakuwa imepita miaka mingi. Kumbuka kesi ya Pinochet wa Chile na wengine. Wanaotuhumiwa kwa wizi, hujuma na mauaji, kaeni chonjo
   
 13. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #13
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Na hicho ndicho kinachowatia wazimu watawala wengi wa nchi za kiafrika. Wanapokuwa Ikulu hawawatumikii wananchi kwa usafi bali kwa ubinafsi. Kasumba hii isipoachwa, demokrasia ipo mashakani sana. Sauti ya watu kupitia masanduku ya kura inaweza kufunikwa au kupotezwa.
   
 14. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #14
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Jf siku haizi habari za video wanazihujumu
   
 15. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #15
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kivipi mkuu sijakuelewa?
   
 16. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #16
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Kwani ni kazi yake kushitaki au wako wenye hiyo kazi? Sheria unaijua wewe?
   
 17. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #17
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  basi awapelekee ushahid
   
 18. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #18
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Yule mwanaharakati aliyejitolea kupeleka ushahidi kwa Feleshi msheufanyia kazi au kazi yenu ni kulilia ushahidi ili mchakachue?
   
Loading...