CCM isingekwapua Mablioni ya EPA, leo hii praise team wangekuwa Lindi wanalima Mbaazi

jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
10,239
2,000
*Na Christopher Cyrilo*

ILIKUWEPO NCCR, IKAWEPO CUF, ILA CHADEMA NI TOFAUTI.
Sehemu ya 1

Mwaka 1995, sisi watoto wa enzi hizo tulikuwa na kawimbo flani hivi, tunaimba;
'Mkapaaa, Mkapa ana kikwapa'
'Mremaaaa, Mrema ana kilema'.

Watoto wa Tanga utawaweza kwa vituko?

Kulikuwa na mpambano wa kufa mtu kwenye uchaguzi mkuu wa kwanza uliohusisha vyama vingi Tanzania. NCCR Mageuzi ikiongozwa na Augustino Mrema aliyekuwa akiwakilisha chama chake kwenye nafasi ya Urais dhidi ya Benjamin Mkapa wa CCM. Mrema alichachafya sana na chama chake cha NCCR Mageuzi - lakini chama kilipoteza nguvu miaka michache iliyofuata.

Mwaka 2000 ikawa zamu ya CUF ya Ibrahim Lipumba. Kama ilivyo ada kwa watawala wa Afrika, mabavu mengi yalitumika kuidhibiti CUF hadi kufikia mauaji ya raia kule Zanzibar - doa la utawala wa Benjamin Mkapa kama aliyokiri mwenyewe siku chache zilizopita. CUF ilikuwa na nguvu kubwa iliyotishia uwepo wa CCM madarakani. Tunaambiwa majeshi yalitumiwa kuharibu kura, na kupandikiza hofu kwa raia ali mradi CCM inufaike. Omar Mahita aliyekuwa mkuu wa jeshi la polisi enzi hizo aliratibu uhuni wa kuonesha visu vyenye nembo ya CUF mbele ya vyombo vya habari siku moja kabla ya uchaguzi- eti kwamba CUF walipanga kuchinja watu!

CUF ilisingiziwa udini, CUF ilisingiziwa ugaidi, CUF ilifanyiwa fitina nyingi zikiwemo kuwarubuni viongozi wake na hatimaye leo CUF kimekuwa chama kisicho na mvuto tena.

NGUVU YA CHADEMA
Wimbi la Chadema liliibuka ghafla kipindi cha kwanza cha Rais Kikwete - aliyeingizwa madarakani kwa sababu ya mvuto wake, na kwa msaada wa propaganda za Rostam Aziz na kampeni kubwa zilizofadhiliwa kwa wizi wa fedha za EPA. Sakata la EPA ndilo lilomuibua Mh. Zitto Kabwe, ambaye atakumbukwa kama mmoja wa vijana machachari waliopanda mbegu ya siasa za upinzani kwa vijana wengi nchini. Dr. Wilbroad Slaa pia alifanya kazi kubwa kama Katibu mkuu wa Chama, na zaidi Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe aliyekuwa nyuma ya mafanikio ya siasa za Upinzani tangu wakati huo.

Uchaguzi wa Mwaka 2010 ulikuwa wa aina yake. Jakaya Kikwete alichanganyikiwa hadi akawa anaahidi madaraja kwenye maeneo tambarare yasiyo na mto wala maziwa wala bahari.

Aliyekuwa mgombea wa Chadema, Dr. Wilbroad Slaa alikuwa na mvuto wa aina yake, aliungwa mkono na watanzania wengi na hata kusababisha hali ya kuchachawa ndani ya CCM. Serikali ya Kikwete ikaendeleza kasumba ya kutumia vyombo vya dola kudhibiti wapinzani. Raia wakauawa Arusha, Mbeya, Mwanza, Mara, Iringa, Dar es salaam nk - kwa vitendo vya jeshi la polisi. Imekuwa kawaida kwa CCM kutumia mabavu hata kusababisha mauaji kwa raia wa Tanzania pale inapoona hatari ya kupoteza dola.

Kipindi cha pili cha Urais wa Jakaya kilikuwa kigumu zaidi. Viyoyozi vya jengo la bunge havikuwasaidia mawaziri wa Jakaya Kikwete kila aliposimama Tundu Lissu, au Peter Msigwa, au John Mnyika, au Halima Mdee, Godbless Lema nk.waliyweta kwa joto. Kashfa za ufisadi zilichafua sana serikali ya Kikwete, akawa anapangua baraza la mawaziri kila mara. Chadema ikazidi kuungwa mkono na watanzania wengi zaidi- na sasa wasomi wengi na baadhi ya viongozi wa vyombo vya dola wakaanza kuielewa Chadema. Hoja za Chadema zikaanza kupewa kipaumbele na Serikali ya Jakaya, mfano, kuanzisha mchakato wa katiba mpya. Ilifika kipindi kukawa na msemo kuwa Chadema inaongoza nchi kwa kutumia Rais wa CCM.

UKAWA - ulikuwa tishio kubwa kwa utawala wa CCM kwenye uchaguzi wa 2015. Watia nia karibu wote wa CCM hawakuwa na nguvu ndani na nje ya Chama chao, ukimuondoa Lowasa ambaye alikuwa hatakiwi. Watu wakasema chama kinamfia Jakaya mikononi. Yaliyotokea ni historia ambayo haitafutika siku za karibuni.

KUIUA CHADEMA
Rais Magufuli, baada ya kupewa na watu wenye nguvu, akajenga imani kuwa adui wakubwa wa maendeleo ya nchi yetu ni 'siasa'. Akapiga marufuku siasa. Hakuridhika, akaanza kuvishughulikia 'vyama vya siasa'. Hakujifunza, akaanza kushughulika na 'wanasiasa wa upinzani' - kazi anayofanya hadi leo. Wanasiasa wengi kama si wote wanaoshughulikiwa na Serikali ya Magufuli wanatoka CHADEMA, kana kwamba amedhamiria kuiua CHADEMA kabla ya 2020. Hawezi.

Kuna tofauti kubwa kati ya CHADEMA na vyama vingine vilivyokuwa na nguvu kabla ya CHADEMA kwa namna vilivyojengwa. NCCR ya mwaka 1995 ilipata nguvu kutokana na shahuku ya watu kutamani mageuzi. Pia, Mrema alikuwa na ushawishi kutokana na uwezo mkubwa alioonesha akiwa waziri wa mambo ya ndani wakati mkapa hakuwa akijulikana sana kwa watanzania wa kawaida. Zaidi ya hapo, NCCR ilikuwa na viongozi wachache wenye uwezo na ushawishi kwa jamii, na kubwa kuliko yote haikuwa na watu wanaoweza kubadili mbinu za siasa ili kuendana na hila na figisu za CCM.

CUF nayo ilidumaa kwa 'kukubali' kusingiziwa udini. CCM ikafanikiwa kuharibu taswira ya CUF kwa kuisingizia udini na bahati mbaya viongozi wa CUF nawo walishindwa kucheza na hiyo propaganda chafu. Kama sio UKAWA mwaka 2015 CUF ingekuwa na wabunge wachache zaidi.

Chadema kwa upande wake imeruka vihunzi vingi vya hila za CCM. Kwamba ni chama cha wachaga -imeshindikana. Chama Cha wakatoliki - imeshindikana. Chama Cha wakristo- imeshindikana. Chama cha kigaidi-imeshindikana. Kwa aibu kubwa, CCM imeshindwa kukibatiza Chadema jina lisilofaa.
Hayo yote ni kwa sababu Chama kilisukwa kisomi, na wanasiasa wengi waliopewa nafasi za uongozi ni 'wanadamu wenye akili za kisasa' wasioamini kwenye matabaka ya watu.
Wakati CCM bado wanafanya siasa za kijamaa zinazojali zaidi 'usisi', Chadema imejikita kwenye hoja na sera zinazojali maendeleo jumuishi katika ulimwengu mpya. Kwa sababu hiyo, Chadema inaungwa mkono na watu wenye akili - wasomi huru na wale wasiosoma lakini wana akili. Na hapo kwenye kuungwa mkono ni suala la hiari yao hao wanaounga mkono Chadema na sio kulazimishana na kutishana kama CCM.

Pia, Kuna tofauti ya kimtazamo kwa wananchi ilivyokuwa wakati wa NCCR, CUF na wakati huu CHADEMA ikiwa na nguvu. Nguvu ya NCCR na CUF ilitokana na wafuasi wao zaidi, lakini nguvu ya CHADEMA inatokana na mambo mawili makubwa, moja ni hilo la wingi wa wafuasi na pili ni chuki kubwa ya wananchi kwa CCM na Serikali. Chuki kubwa kiasi kwamba 'idadi ya kutosha' ya wananchi wanamtamania kifo kiongozi wao. Mbaya zaidi, hakuna ishara ya kujifunza kwa hilo.

Wapo wananchi wengi wanaochukia serikali ya CCM na sio wanachama au wafuasi wa CHADEMA, lakini serikali ya CCM haiwezi kuwatofautisha watu hao na CHADEMA - ambao wanaongezeka kila siku kutokana na matendo ya hovyo ya serikali ya CCM. Kwa kupambana na CHADEMA kwa mbinu za kisiasa za hovyo, serikali ya CCM inazidi kuchukiwa na kundi hilo la watu, na kwa sababu ya akili finyu - kundi hilo linatazamwa Kama CHADEMA, na hali hiyo pia inachangia nguvu ya CHADEMA.

Kuna sababu nyingine kubwa inayoipa CHADEMA uhai wa muda mrefu - nayo ni mizizi ya Chama. Programu ya CHADEMA NI MSINGI imekifanya chama kukita mizizi hadi kwenye vichochoro vya nchi. Huko kwenye misingi wanachama wanajipangia, wanajisimamia, wanajiongoza bila kutegemea usimamizi wa makao makuu ya Chama. Kwa mtindo huo, Chadema kimeshakuwa chama Cha watu na sio cha viongozi. Kuwafanyia hujuma viongozi wa Chama hakuwezi kuua chama...wapo wengi wanaoweza kurithi na kuongoza chama.

Chadema ni familia. Vijana wengi wa Chadema wanatendeana kama ndugu, ukiacha wachache wenye akili za ki-CCM. Jambo hilo ni hazina kubwa kwa Chama kwa sababu mahusiano ya wanachama yanajengwa na kitu zaidi ya siasa - na kushirikiana kwenye mambo ya nje ya siasa, kwa hiyo wanachama wanabaki pamoja hata kwenye mitikisiko ya kisiasa. Katika mazingira kama haya, kutaka kukiua Chadema ni kujitafutia maradhi ya moyo, ni kujitafutia msongo wa mawazo - uje kufa bure.
Itaendelea...
 

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,571
2,000
Asante sana kwa bandiko zuri!

Nimependa sana pale unaposema 'wananchi wengi wametokea kuichukia CCM na matendo yanayofanywa na serikali lakini serikali wala chama hawaonekani kujifunza kitu halafu wanawachukulia wote wanaoichukia CCM au serikali kwamba ni CHADEMA!

Juzi juzi tulikuwa tunapiga stori na mmoja wa wasimamizi wa uchaguzi huu unaotarajiwa wa serikali za mitaa.

Katika maongezi likajitokeza swala la hawa waliosusia uchaguzi kama wako sahihi na ni kweli wagombea walijaza fomu vibaya!?

Nilipoonekana kupinga hoja zake, ghafla akabadilika na kusema "Chadema utawajua tu"! Nilishangaa Sana nikamuuliza swali kwamba kwa hiyo kila anayetofautiana mtazamo na yanayofanywa na serikali ni CHADEMA?
 

jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
10,239
2,000
Uncle Jei Jei,

Ukitofautiana na serikali wewe ni CHADEMA, kwahiyo zaidi ya watu MILIONI 30 ni CHADEMA , maana CCM haikubaliki kabisa ila inalazimisha kwa kutumia tools za mkoloni.
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,612
2,000
Mie nimefurahi sana kusikia Mkapa kaweka hili hadharani!!

Kuna siku niliwahi kusema hapa kwamba JPM afunge mdomo wake kwa sababu hajui ameingiaje ingiaje madarakani!!!

CCM kila unavyofika Uchaguzi Mkuu lazima waibe pesa za wananchi! Mkapa kaiba za EPA kumwingiza JK na JK nae kaiba za Escrow kumwingiza JPM.

Tusubirie wizi mwingine wa kutisha ifikapo 2023/2024.
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,717
2,000
Mie nimefurahi sana kusikia Mkapa kaweka hili hadharani!!

Kuna siku niliwahi kusema hapa kwamba JPM afunge mdomo wake kwa sababu hajui ameingiaje ingiaje madarakani!!!

CCM kila unavyofika Uchaguzi Mkuu lazima waibe pesa za wananchi! Mkapa kaiba za EPA kumwingiza JK na JK nae kaiba za Escrow kumwingiza JPM.

Tusubirie wizi mwingine wa kutisha ifikapo 2023/2024.

Kwa kutokuwa na uhakika wa 2020 tayari wameshakwiba tayari zile T1.5 ambazo kumbe ni 2.4t.
Hakuna uhakika kabisa wa uchaguzi ujao ndio maana kampeni zimeanza mapema. Kaanza kujikomba kwa wasanii akidhani watamsaidia wakati ni kundi lililo dharauliwa sana kwa wakati huu.
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,612
2,000
Kwa kutokuwa na uhakika wa 2020 tayari wameshakwiba tayari zile T1.5 ambazo kumbe ni 2.4t.
Hakuna uhakika kabisa wa uchaguzi ujao ndio maana kampeni zimeanza mapema. Kaanza kujikomba kwa wasanii akidhani watamsaidia wakati ni kundi lililo dharauliwa sana kwa wakati huu.
Yaani Genge la CCM ni moja ya magenge hatari kabisa kuwahi kutokea duniani! Na tena heri ya wakati wa JK ilikuwa watu wakiiba tu, tunajua lakini huu ufichi wa sasa, watu watapasuka vichwa wizi utakapoanza kuwekwa hadharani hapo 2026.

Itakuwa kama wakati wa Mkapa... huku mitaani anaimba yeye ni Mr. Clean kumbe wanapiga matukio ya kufa mtu kimya kimya!!
 

Mkendo

JF-Expert Member
Oct 14, 2013
2,847
2,000
Hawawezi kuzishinda Nguvu za wakati,pamoja ma mabomu na virungu.

Upinzani wa kweli upo mioyoni .
 

kidyongo

Senior Member
Oct 21, 2018
128
250
Sawa,kwa kuwa chadema inakybalika nadhani hawatasusia uchaguzi wa serikali za mitaa,wekeni mpira Kati tucheze sasa why mpira kwapani yakheee?
 

mtume wawatu

JF-Expert Member
Oct 30, 2016
614
1,000
Mkuu wewe ukweni unajiweka kizibo cha wine!?
Hajanielewa. Mwandishi wa bandiko kashindwa kuonesha udhaifu wa chadema. Na hiki ndicho kitakachoua chama hiki. Lolote linalotokea kukikosoa hiki chama linaonwa kama usaliti kumbe ni kwa maslahi ya ustawi wa chama.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom