Mnyika,
Binafsi napenda kukupongeza kwa jukumu hili jipya na gumu kwako. Kwa muda sasa umekuwa mtendaji mzuri, mwadilifu na mkweli katika wadhifa wako kabla ya hapo.
Ninachopenda kukuasa ni kuwa karibu zaidi na mawazo ya wananchi, wanachama na makada katika kujenga chama chetu. Nina matumaini sana na wewd na ni imani yangu kwamba utakiinua chama chetu juu zaidi. Katika utendaji kazi wako utakutana na hoja nyingi chafu, zenye lengo la kukupotezea muda na heshima yako, daima simama imara na kuwa muwazi ukikwepa kwa hali na mali kutumika kama mpotoshaji mkuu na mpindishaji wa malengo na sera za chama.
Katika kipindi hiki mijadala ni mingi mno itaibuliwa mingine ikiwa na lengo la kukukwamisha wewe binafsi na chama, nakusihi songa mbele na daima toa kauli sahihi ili kuepuka malumbano yasiyo lazima ya ndani ya chama.
Utakutana na makundi na mitazamo tofauti, yenye kulenga maslahi binafsi hasa itakayoishia kukishushia chama, nakuomba usiwe mwepesi wa kujibj kila jambo litakaloelekezwa chadema, hii itakuwa busara kuu na iliyotukuka kwako na kwa uongozi uliokukasimu wadhifa huo.
Chama kwetu sisk makada, kitakusikiliza kama msemaji mkuu na mjuvi wa kila jambo na kwa hakika wewe sasa u daraja baina yetu na chama.
Mungu akusaidie, mungu anisaidie na mungu awasaidie watanzania wote wapenda mabadiliko popote walipo.
Ni mimi,
Pangu Pakavu
Nakusalimia.
Utakuwa ni uteuzi mzuri na makini kwani kurugenzi yetu ya habari na uenezi haikuwa active kiasi kinachotakiwa.
Ili afanye kazi zake vizuri zaidi na kwa uhakika inabidi wampunguzie majukumu ya ukurugenzi wa mambo ya nje.
Na kuanzia sasa wale watunga propaganda dhidi ya chadema wamepata kiboko yao, JJ amekuja kuwashika!