Dr.slaa alia na ardhi na vituo bandia Arumeru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr.slaa alia na ardhi na vituo bandia Arumeru

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by PISTO LERO, Mar 23, 2012.

 1. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Dk Slaa na ardhi

  Katikamikutano ya jana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alimshambuliaNaibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Gudluck Ole Medeye kwambaanahusika na kukodisha shamba la Valesca lililo Jimbo la Arumeru Mashariki kwawawekezaji kwa bei ya kutupa.

  Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Ngabobo, Ngurdoto naSakila, Dk Slaa alisema ni aibu mawaziri wa Serikali ya CCM kuomba kura katikaJimbo la Arumeru Mashariki huku wakiwa ni waasisi wa mpango wa kugawa ardhi yaumma kwa walowezi wa kizungu.

  Alisema Naibu Waziri huyo, ambaye ni mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi,kabla ya kukubali kutolewa shamba hilo lenye zaidi ya ekari 400 ambalo Serikaliitapata kiasi cha Sh2.4 milioni tu kwa mwaka walipaswa kuwakumbuka wananchi.

  “Hivi kweli nyie wananchi wa Meru hamuhitaji ardhi hii na mngeshindwa kulipa Sh6000kwa ekari moja ili muweze kulima, kama alivyouziwa mzungu? ”alihoji Dk Slaa.

  Aliwataka wakazi wa jimbo hilo, kukubali mabadiliko sasa kwa kuchagua mbunge waupinzani ili aweze kuhoji ardhi ya Meru ambayo kiasi kikubwa kimegawanywa kwawalowezi kutoka nje ya nchi.

  Vituo bandia

  Wakati hayo yakiendelea, tuhuma kwamba kuna vituo 55 vya bandia vilivyoandaliwakwa lengo la kutumika kuiba kura kwenye uchaguzi huo, zinaonekana kugonganishavichwa vya maofisa wa uchaguzi.

  Tuhuma hizo ni zile zilizotolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaajuzi kwamba kuna vituo 55 bandia 55 vya kupigia kura katika uchaguzi huo mdogomadai ambayo yalikanushwa na Msimamzi wa Uchaguzi wa Arumeru Mashariki, TrasiasKagenzi.

  Juzi Kagenzi alipozungumza na waandishi wa habari alisema vituo halali ambavyoanavitambua ni 327 tu na hakukuwa na kituo ambacho kimeongezwa na kwamba hatakama ikitokea hivyo, itakuwa ni baada ya majadiliano na vyama vyote shiriki.

  “Vituo vilivyopo ni 327 pekee, na kama ikitokea kituo kinakuwa na watu zaidi ya500 ndipo kunaweza kuongezeka, lakini historia inajionesha kila uchaguzi mdogounapofanyika idadi ya wapigakura inapungua,”alisema Kagenzi.

  Lakini jana Kagenzi alikiri kuwapo kwa kasoro kwenye orodha ya vituo hivyo nakwamba alikuwa anawasiliana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ili kuwezeshakufanyika kwa marekebisho.

  Maeleo ya Kagenzi yanatokana na ushahidi ambao gazeti hili liliupata kwa kuonaorodha ya vituo hivyo, ambayo ilikuwa ikionyesha takwimu mbili tofauti za idadiya vituo vya kupigia kura.

  Katika orodha hiyo, safu ya idadi ya vituo vya kupigia kura katika kata 17 zajimbo hilo ilikuwa ikionyesha vituo 327, wakati safu ya mwisho ya orodha hiyohiyo ilikuwa ikionyesha kuwapo kwa jumla ya vituo 382, likiwa ni ongezeko lavituo 55.

  Waraka wa orodha hiyo unaonyesha kuwa katika Kata ya Akheri kutakuwa na vituo20 idadi ambayo inayofautiana na iliyotolewa na tume ambavyo ni vituo 18.

  Kata nyingine ambazo vituo hivyo vinaonekana kuongezwa ni Kikatiti vituo 22badala ya 18, Kata ya Kikwe vituo 12 badala ya halali 11, Kata ya Kingori vituo29 badala ya halali 26 na Kata ya Leguruki vituo 23 badala ya halali 20.

  Kata nyingine ni Makiba vituo 21 badla ya halali 18, Majiya chai 24 badala ya29 halali, Maroroni vituo 21 badala ya 17 halali, Mbuguni vituo 25 badala yahalali 21,Nkoarsambu vituo 10 badala ya 8 vinavyohitajika na Kata yaNgarenanyuki ambako vimeongezwa vituo sita kutoka halali 20 hadi 26.

  Orodha hiyo ambayo Kagenzi alithibitisha kwamba ilikuwa na makosa pia inakasoro katika Kata za Nkoaranga ambako vituo vimeongezwa kutoka halali 17 hadi22, Pori kutoka vituo halali 16 hadi 20, Nkwandua kutoka vituo 22 hadi kufikia25 na Kata ya Seela - Sing’isi vituo hivyo viliongezwa kutoka halali 12 hadi15.

  Kata nyingine ni Songoro nyumbani kwa Mgombea wa Chadema, Joshua Nassari vipovituo 15 na hakuna kilichoongezeka huku Kata ya Usa River ilikuwa na vituo 36,lakini vimeongezeka vitano na kufikia 41.

  Kagenzi alisema alipowasiliana na idara ya teknolojia ya habari ya NEC kuhusukasoro hizo walimwambia kwamba orodha ya awali haikuwa toleo la mwisho nakwamba wangefanya marekebisho ya kuondoa kasoro hizo.

  “Wameniambia kwamba hiyo orodha ilikuwa ni working draft tu (rasimu yakufanyiwa kazi), kwahiyo nimeomba hiyo orodha kamili ya mwisho, wakishanitumianitaisambaza kwa vyama husika,”alisema Kagenzi jana.

  Baadaye msimamizi huyo wa uchaguzi alisema wataalamu kutoka NEC walitarajiwakuwasili Arumeru jana mchana kwa ajili ya kurekebisha kasoro hizo pamoja nakufanya maandalizi mengine kwa ajili ya uchaguzi huo mdogo.

  Hata hivyo, kauli ya Kagenzi ilikuwa ikipishana na ile iliyotolewa naMkurugenzi wa Uchaguzi, Julius Mallaba ambaye awali alisema hakukuwa na vituovya nyongeza kama ilivyodaiwa na Dk Slaa.

  Baada ya kuelezwa kuhusu orodha hiyo ya tume, Mallaba alisema: “Basi kama ikohivyo nitawasiliana na wahusika ili tuone hatua waliyofikia katika kurekebishakasoro hizo”.

  Dk Slaa alisema hali kama hii waliibaini katika Jimbo la Igunga mara baada yamatokeo kutangazwa na baada ya kufuatilia walikuta vituo hewa ambapo vilikuwana kura kati ya 160 na 280.

  GAZETI LA MWANANCH

   
 2. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Makamanda msilale, bado mapambano.
   
 3. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  bravo the real dk.
   
 4. monongo

  monongo JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 370
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Jamani makamanda msilale,kama mnavyojua siku zote shetani huwa halali , kadhalika magamba ni mashetani ya kijani yenyewe siku zote yana waza jinsi ya kuiba kura na fedha za walala hoi.magamba hayana huruma hata kidogo.
   
 5. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Sijui katiki hilo vituo hewa Jaji Lubuva atajiteteaje.
   
 6. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Takataka wakubwa!! Mnajifanya eti mmekosea. Safari hii mmeshikwa pabaya. Makamanda msilale na Mungu awe nanyi. Lazima haki ipatikane. CCM ni kifo tu kinasubiri. Huyo Mkuu wa NEC atasemaje hili??
   
 7. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ukiisha ona Slaa anaanza kulalamika hivyo ujue ameisha jua kuwa atashindwa, hapa anatafuta sababu tu
   
 8. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Sio kulalamika ww.. Ni fact na mpaka Tume wenyewe wamekiri ni kweli kuna vituo hewa ambavyo hawajui vilikotoka..! Magamba mmekamatika sasa.. Hakuna pa kutokea..
   
Loading...