Dr. Slaa ajifunze kwa kutazama ziara za Kinana

The Intelligent

JF-Expert Member
Dec 27, 2013
2,459
818
Ukitazama ziara ya katibu wa CCM inayoendelea kwenye baadhi ya mikoa, utaona kuna mengi ya kujifunza kwa viongozi wa CHADEMA.

Binafsi sio mpenzi wa siasa za chama, lakini huwa napenda kuona namna vyama vinavyoshindana kwa hoja, ziara ya kinana imeonesha kurejesha matumaini ya wa-tz kwa CCM.

Nilichokiona kikubwa kwa kinana ni namna anavyogusa maisha ya watu anaowatembelea(hata kama kwa ahadi hewa), wananchi wana matatizo ya ardhi, maji, kilimo nk. hili Kinana amelijua mapema, Slaa jifunze hapo.
 
Duhu -- umenigaragaza ndugu yangu - sina mbavu. Yaani unataka Dr wetu wa ukweli awe analia lia tu kama Kinana kwa madudu yanayofanywa na serikali ya CCM kwa wananchi?
 
Haha ajifunze kulaghai wananchi? Eti ataongeza ruzuku kwa hospital ya Dareda labda serkal ni mali ya babake
 
Slaa ameishiwa hoja hata ukimsikiliza kwasasa ni kama amejikatia tamaa, huwezi kumlingani Kinana na babu Slaa.

nikweli uwezi linganisha fisadi na mzalendo babu kinana hana usafi wowote 2namjua tangu akiwa mbunge wa arusha hasafishiki hata kwa jiki.
 
Haha ajifunze kulaghai wananchi? Eti ataongeza ruzuku kwa hospital ya Dareda labda serkal ni mali ya babake

Mkuu Helper, slaa ni bingwa wa kupiga propaganda ila hamwezi kinana, yule mzee anajua kuwazunguka watu hadi wanakaa sawa! ukimtazama huwezi kuamini kama ndiye anashutumiwa ku-deal na pembe za ndovu.
Nasema tena slaa ajitazame upya, atumie kipaji chake cha kujenga hoja ndio anaweza kumtoa kamasi mzee kinana, vinginevyo ataishia kunawa wakati mwenzake anamalizia kula.
 
Last edited by a moderator:

ziara za kinana hazina tija zaidi ya ulaghai kwa watz wasiojielewa,Hivi ulishajiuliza ni kwa nini hizo porojo zake za kuwa katiba haiwezi kuleta maendeleo anazitoa kwa watu mbumbumbu tu? Maeneo yenye watu wanaojitambua kama hapa Mwanza hawezi kutoa huo uharo wake!
 
Ukitazama ziara ya katibu wa CCM inayoendelea kwenye baadhi ya mikoa, utaona kuna mengi ya kujifunza kwa viongozi wa CHADEMA.

Binafsi sio mpenzi wa siasa za chama, lakini huwa napenda kuona namna vyama vinavyoshindana kwa hoja, ziara ya kinana imeonesha kurejesha matumaini ya wa-tz kwa CCM.

Nilichokiona kikubwa kwa kinana ni namna anavyogusa maisha ya watu anaowatembelea(hata kama kwa ahadi hewa), wananchi wana matatizo ya ardhi, maji, kilimo nk. hili Kinana amelijua mapema, Slaa jifunze hapo.

CDM HAINA HELA YA KUNUNULIA WALI WATU WOTE KWENYE MKUTANO na KUWAPA SARE .
 
Ukitazama ziara ya katibu wa CCM inayoendelea kwenye baadhi ya mikoa, utaona kuna mengi ya kujifunza kwa viongozi wa CHADEMA.

Binafsi sio mpenzi wa siasa za chama, lakini huwa napenda kuona namna vyama vinavyoshindana kwa hoja, ziara ya kinana imeonesha kurejesha matumaini ya wa-tz kwa CCM.

Nilichokiona kikubwa kwa kinana ni namna anavyogusa maisha ya watu anaowatembelea(hata kama kwa ahadi hewa), wananchi wana matatizo ya ardhi, maji, kilimo nk. hili Kinana amelijua mapema, Slaa jifunze hapo.
Soma maelezo yako vizuri halafu jitathimin je? Kweli wewe sio mpenzi wa siasa za vyama?kuuficha unafiki ni kazi ngumu sana hasa kama huna mazoea ya kuwa mnafiki.
 
yaani aige mifano ya ziara za kinana zinazotusababishia garama zisizokuwa na maana kwenye nchi hii? ajabu hii.
garama anazotumia kinana si ajabu zingejenga nyumba za walimu zaidi ya 100. huu upuuzi huu, unakera sana.
watu wanafikiria siasa tu badala ya maisha ya watu.
 
Umetoroka Mirembe mleta mada?Ajifunze kuwaita Mawaziri wa chama chake "mzigo" bila kuwa na nguvu ya ushawiahi ya kuwaondoa?

Kuitetea CCM lzm uwe na akili "fyatu"kama ya huyu jamaa
 
Back
Top Bottom