Nampongeza Dr Slaa kwa kusikika baada ya kujificha kwa muda mrefu. Nimefuatialia majibu yake, but kinachonitatanisha ni kwamba, huyu dr hana sera mpya. Kwanini kila akiongea popote lazima atoe reference za EPA na Ufisadi?
Huu ni muda muafaka kwake kubadilika.
Wananchi tunahitaji kupata mapya kutoka kwake. Tunahitaji kusikia juhudi anazozifanya na chama chake kuleta maisha bora kwa kila mtanzania.
Nafasi ya chama kufanya zaidi hutolewa na wananchi na chama hakina uwezo wa kuinyakua. Kama umekiri kuwa kwa kiasi fulani wamefanikiwa na unaamini wanahitajika kufanya zaidi, suala sahihi la wewe kufanya ni kuunga mkono yale yaliyofikiwa ili ridhaa ya wananchi ipatikane, wapewe dola na waweze kufanya hiyo zaidi unayoitaka.
Kuna tofauti kubwa kati ya kukosoa na kuponda. Usipoijua hiyo tofauti utagombana na mama mkwe wako. Mayage ameconclude kwenye makala yake kuwa solution ni kuanzishwa chama kingine, huu ni ukosoaji? Yawezekana huna nia mbaya ktk comments zako, lkn yaelekea huna akili pia. Ni nini unachohitaji wewe kama mwananchi, siasa za kubwabwaja majukwaani na kusubiri uchaguzi au chama kilicho active wakati wote kikiwatumikia wananchi?
Uanaharakati ndio hasa msingi wa mabadiliko chanya ktk mataifa ya kidemokrasia. Ndio njia ya kupata haki toka kwa watawala dhalimu. Shida yetu watanzania ni uoga wa mabadiliko. Badilika kimtazamo, acha uoga na unga mkono harakati hizi za CHADEMA. Tanzania haitakuwa huru kwa uwakilishi wa wabunge wanaoorodhesha msululu wa matatizo ya majimbo yao halafu wamalizie kwa 'naunga hoja mkono kwa 100%'.
Na kama shida yako ni yale yanayohubiriwa majukwaani na CHADEMA, labda nikuulize: Ulitaka wajadili nini zaidi ya yale yanayotukwamisha tusiendelee?
Kuna kingine kinachotukwamisha zaidi ya ufisadi, mikataba mibovu, wizi wa rasilimali, uwajibikaji mdogo, kujuana na kufumbiana macho tunapokosea?
Ni vyema wananchi tukaaacha upuuzi, hizi nguvu za kuisakama CHADEMA tungeielekeza kwenye kuisakama serikali iwachukulie hatua wanaotufilisi. Kama tutagoma kushiriki harakati na kukaa tusubiri kuanzishwa kwa chama kitakacholeta maajabu kwa kukaa ofisini na kukomesha mabaya haya, basi hatutakuwa na tofauti na Mayage anayewaza kwa kutumia tumbo.
Wako ktk kupinga mambo ya kijinga na ukosoaji usio na mashiko,
Shizukan
Nyie CHADEMA ni watu gani msiotaka kukosolewa???? Mayage katika makala yake aliwakosoa na kuwataka mfanye vizuri zaidi lakini mmeigeuza makala yake kuwa ugomvi kana kwamba amewatukana matusi ya nguoni. Ni nyie mnaolalamika hali ya nchi kwa sasa na kuhoji kama kweli Rais ana washauri. Nyie mnaukataa ushauri wa Mayage, je huyo Padri wenu aliyeasi akiingia Ikulu atamsikiliza nani?
kwani mayage mayage ni nani?? Ata atushauri tuwe na utitili wa vyama?? Hizi ni njaa tu zinawasumbua, kujipendekeza pia wanatumiwa na mafisadi, dr slaa tunamuelewa na kumkubali sana ivi mayage mayage amesikia matokeo ya uchaguzi uko mbeya vijijini?? Aaah kama hajui basi ajue tumechukua kijiji uko, natmai km anadhani anacapacity ya kutosha basi aanzishe icho chama aone mziki wake o/w aache mdomo anabwabwaja tu uyo.. Masab...li pia tokoilake lake....siku zote chadema tunasema ni chama makini chenye viongozi mahiri katika kujenga hoja, dr ndiye mwasisi wa mapambono dhidi ya ufisadi na chama chetu kitaendelea kusimamia ukweli huu huyu mwandishi anatakiwa atambue kuwa watanzania wanatambua kuwa chadema ndiyo mkombozi wa uchumi wa tanzania na tanzania tunayoitaka (tanzania we want)
siku utakapo acha kubwabwaja mashudu pia pumbalini chadema wataacha kulalamika hovyo!!!!!!!!!!!!!!!
dr slaa badili mifani... you can go deeper than that kwa ku refer hata nje ya tz
Ni vizuri kafanya hivyo!
Sijalisoma bado la yaelekea anajibu kwa kuonyesha postive achievements za CHADEMA na hilo ni kosa!
Mayage kasema chama kina nafasi wafanye zaidi ya walivyofanya sasa! Sasa inaonekana watu hawapendi kukosolewa, hili nalo ni mapungufu ya kiuongozi! Ndo maana Dr Slaa naye hafai kuwa kiongozi wa nchii hii!
Haya ni maoni yangu kama mwana CHADEMA, unafiki kwangu hauna nafasi!!!
thank you very much dr. ninaamini hakuna executive leader wa ccm aliye na uwezowako na pia ambaye angejali kunijibu.MTM
Kwa manufaa yako na wana JF Serikali yako imekabwa na wahisani kuhusiana issues hizo unazotaka Dr Slaa asizizungumzie. Kwa taarifa yako mambo hayo yote ndiyo kwanza yamepamba moto. Kikao kati ya serikali ya JMT na wahisani cha 24.6.2011 kilitoa action plan ya utekelezaji wa ufuatiliaji wa madeni ya EPA.
Taarifa ya sasa ni kuwa makumpuni kadhaa kama Ndovu Soaps,Bora Hotels and Appartments,Venus Hotels B.V.Holdings, VB Associates Kagoda Agricultre wamerudisha asilimia 100 fedha zilizofisadiwa. Jumla yote ni 70,725,425,541.39. Makampuni 13 hayajurudisha chochote.Kikao cha Troika kilitakiwa kukaa Taarifa ya kinachoendelea. Kwa taarifa ya wanaJF hata misaada inayopewa JMT iko conditioned kwenye matokeo ya EPA. Ndio maana narudia No Research no Right to speak.
Watanzania kweli wa ajabu, Wazungu wanafuatilia uwizi nchini kwetu sisi tunapiga porojo zisizo na tija. Alafu unaongelea maendeleo wakati hata hizo zilizorudi hujui zilirudishwa wapi. Maybe wanaobisha ni mafisadi au beneficiaries wa ufisadi.
Ahsante Dr. Slaa, majibu yako yanajitosheleza,yenye hekima na yenye uchunguzi wa kina.MTM

yana hekima with wrong assumptions...Ahsante Dr. Slaa, majibu yako yanajitosheleza,yenye hekima na yenye uchunguzi wa kina.