Dr. Slaa aikana akaunti ya Twitter, asema imegushiwa

Dr. Slaa aikana akaunti ya Twitter, asema imegushiwa

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,255
Reaction score
8,027
Katibu mkuu wa CHADEMA ambaye yuko mapumzikoni kwa sasa Dr Slaa amekanusha vikali akaunti ya Twitter ambayo imekua ikimzushia mambo mbali mbali! Akaunti hiyo iliyokosewa hata jina lake amesema ni feki na hajawahi kua na akaunti ya Twitter.

My take:
Wadau humu JF tuwapuuze wazushi hawa wanaojaribu kutengeneza taswira mbovu ya UKAWA.

=================================

Dar es Salaam. Wakati kukiwa na taarifa zinazosambaa mtandaoni zikimuhusisha Dk Willibrod Slaa na akaunti ambayo imekuwa ikitoa msimamo wake wa kujitenga na shughuli za siasa pamoja na Ukawa, katibu huyo mkuu wa Chadema amekanusha taarifa hizo akisema hajawahi kuwa na akaunti ya twitter.

Hii ni mara ya pili kwa Dk Slaa kuzungumza na gazeti hili, lakini akikatakaa kufafanua mambo mbalimbali yanayohusu sakata lake na Chadema, akiahidi kuwa kufanya hivyo baadaye, huku akiweka bayana kuwa hajawahi kuwa na akaunti ya twitter.

Dk Slaa, aliyekuwa anatajwa kuwa mgombea urais wa Chadema, hajaonekana hadharani katika matukio makubwa ya kichama tangu Chadema na Ukawa walipomkaribisha waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa na kumteua kuwa mgombea urais anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja huo.

Mara ya mwisho kuonekana kwenye shughuli za chama hicho ni katika kikao cha Kamati Kuu wakati Lowassa alikaribishwa kufanya majadiliano na kujibu hoja za wajumbe.

Lakini baada ya hapo Dk Slaa hakuonekana wakati wa kutambulishwa kwa Lowassa kwa waandishi wa habari, tukio la kuchukua na kurudisha fomu za urais ndani ya chama na tukio la juzi la kuchukua fomu za urais kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Wakati hayo yakiendelea, kuna akaunti ya twitter yenye jina la "Dr Willibrord Slaa" ambayo imekuwa ikitoa kauli mfululizo zikiwa na ujumbe mbalimbali unaoendana na mazingira aliyomo sasa mwanasiasa huyo.

Agosti 10, kulitumwa ujumbe zaidi mara 10, mmojawapo ukijaribu kuwaaminisha watu kuwa hiyo ni akaunti halisi ya Dk Slaa.

"Ndugu zangu Watanzania, hii ni akaunti yangu rasmi, bila shaka yoyote na naomba ninachoandika hapa kifikishwe kwa Watanzania popote walipo," unasema ujumbe huo.

Taarifa nyingine zilizotumwa kwenye akaunti hiyo ya twitter ni pamoja na ile iliyoeleza kuwa Dk Slaa ameomba ulinzi kutoka nchi na mashirika ya kimataifa na atazungumza kupitia runinga na redio pindi atakapopata ulinzi.

Akizungumza na gazeti hili jana, Dk Slaa alisema hajawahi kutuma taarifa yoyote kwenye mitandao ya kijamii.

"Sijawahi ku-operate (kuendesha) kitu chochote kwenye akaunti ya twitter, sina akaunti kama hiyo," alisema Dk Slaa.

Mbali na kukanusha kumiliki na kuendesha akaunti hiyo, Dk Slaa alirudia kauli yake ya wiki iliyopita kuwa atatoa msimamo wake muda muafaka utakapofika, baada ya kuulizwa swali kuhusu hatma yake ndani ya Chadema na kisiasa kwa ujumla.

"Subira yavuta heri, sasa ili uipate hiyo heri unatakiwa kuvumilia. Kwa hiyo wakati ukifika nitazungumza tu na Watanzania," alisema.

Alipoulizwa ni wapi alipo kwa sasa, alisema yupo Dar es Salaam anapumzika, lakini akasisitiza kuwa ipo siku ataweka wazi mustakabali wake kisiasa.

Dk Slaa alisema yeye na mke wake Josephine Mushumbusi wanatarajia kusafiri kwenda nje ya nchi katika siku chache zijazo, ingawa hakuweka wazi nchi anayotarajia kuitembelea, lakini akasema atarejea baada ya wiki moja.

Chanzo: Mwananchi
 
Ahsante baba Dr. Slaa. Tunaendelea kukuombea hatimaye urejee kwenye mapambano
 
Gazeti gani ili tujue kama linasema ukweli au uzushi.
 
Hii sheria ya kwenye mtandao itakuwa inawafunga watu siyo, kama mtu anaweza kuanzisha account kwa jina la mtu mwingine na kutukana sii hatari sana?
 
Kama amesema hajawahi kuwa acount twitter ile iliyobadilishwa jina na kupewa jina lLowassa ilikuwa feki pia.
 
Wenyetabia ya kumlisha maneno wataendelea kuumbuka wanadhan Dr Slaa anaweza hamia chama chakichawi chakina liz 1 kinacho elekea ukingon!
 
Wenyetabia ya kumlisha maneno wataendelea kuumbuka wanadhan Dr Slaa anaweza hamia chama chakichawi chakina liz 1 kinacho elekea ukingon!
Unadhani atabakia kwenye saccoss?
Nimeuliza source ya gazeti sijapewa...
 
Acha uzushi, akaunt ni ya kwake Dr. Slaa. Kwani bavich name ukawa fans shida yenu ni nini? Yeye kesha sema nyekundu siyo njano. Kwaheri.
 
Tweet from Dr Willibrord Slaa (@willibrordslaa) - Dr Willibrord Slaa (@willibrordslaa) tweeted at 7:07 AM on Wed, Aug 12, 2015:Mwananchi leo Agosti 12 "Dr Slaa aikana Twitter account". Si kweli, wanaongopa. Sijazungumza na gazeti hilo wala mwandishi Florence Majani.
 
Acha uzushi, akaunt ni ya kwake Dr. Slaa. Kwani bavich name ukawa fans shida yenu ni nini? Yeye kesha sema nyekundu siyo njano. Kwaheri.

Usiwe na ubishi mkuu! Watafute waandishi wa gazeti uwaulize
 
Kumekuwepo na twitter account ambayo imekuwa iki-tweet vitu controversy kwa kutumia jina la Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willbroad Slaa.

Kwa muda sasa imekuwa ikisababisha usumbufu kwa watu wengi hasa watumiaji wa mitandao ya kijamii, kwa vitu inavyoandika na kusambaza ambavyo havina uhusiano wala hadhi ya Katibu Mkuu Dk. Slaa wala CHADEMA.

Tunapenda kusisitiza kwa mara nyingine kuwa kwa sasa Dk. Slaa hana twitter account ama anayoiendesha mwenyewe au inayoendeshwa na mtu mwingine kama ilivyowahi kutokea huko nyuma.

Ukiangalia kwa makini jina la Katibu Mkuu linalotumika kwenye twitter account hiyo LIMEKOSEWA. Hii pekee inaweza kuwa sababu kubwa kabisa kuonesha kuwa account hiyo ni fake na wanayoitumia wanafanya hivyo kwa malengo yasiyokuwa chanya kwa nafasi ya Katibu Mkuu na mabadiliko kwa ujumla hasa kuwakanganya watu.

Tayari hatua stahiki zinafanyika kumaliza usumbufu huo kabisa.

Tumaini Makene
Mkuu wa Habari na Mawasiliano - CHADEMA
 
Hongera Dr Slaa tuko pamoja endelea kupumzika mbele kwa mbele karibu sana.
 
Baba hapo umewapa zauso wanao jiegemezaga kwa wenzao ili wasukumwe kwa nyuma maana wao pekee hawajiwezi kila siku mh Dr Slaa wanamlishaga miji maneno wakizan ktb mkuu anaweza hamia ktk chama cha kina liz 1 nabado kimya kingi kinamshindo na usimuone kobe kainama. Utukufu wa mwisho utaushinda ule wamwanzo time will tell ccm hoyiiiiiiii
 
Back
Top Bottom