Dr. Slaa aibuka kutoka Canada, Asema wanaomponda Magufuli ni Mafisadi

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
20160323_043409.jpg

DK. Slaa atabaki katika kumbukumbu ya watanzania kama mpambanaji shupavu wa vita dhidi ya ufisadi Mungu azidi kumpa afya njema.
 
Hivi Maisha yake huko yanagharimiwa na nani huyu mwanasiasa shupavu?
Zinagharamiwa na walewale waliofadhili ziara zake ulaya na Marekani kutangaza Chama na kueleza ulimwengu kinachoendelea Tanzania. Aliwaambia kipindi anafanya hizo ziara hamkuwahi kuhoji ingawa ilijulikana si kwa fedha za chama ....sasa leo mnapata wapi nguvu za kuhoji akiwa nje ya chama?
 
Basi sawa....
 
Hatufanani kimaisha hata kdogo hatufanani style yakutafuta maisha kila mtu anastyle yake.dr slaa baada ya upadre alishakuwa na life style yake na alikuwa anakaa mara kwa mara Italy na Germany na ukumbuke vzuri wafadhili wengi wa cdm yy ndye cordinator. afu kingne hichi anachofanya Magufuli cyo mliokuwa mnalilia CDM siku zote?
 
20160323_043409.jpg

DK. Slaa atabaki katika kumbukumbu ya watanzania kama mpapmbani shupavu wa vita dhidi ya ufisadi Mungu azidi kumpa afya njema.
Kwanini akakimbia uwanja wa mapambano na kwenda mafichoni? Mpambanaji shupavu mkweli na mahiri hupambana mpaka dakika ya mwisho .....anayasema haya sasa baada ya kusaidiwa kugomboa nyumba yake....huyu kakimbia asili yake atatangatanga chini ya ardhi mpaka mwisho...!
 
Aisifiae mvua imemnyea, lazima amsifie magufuli kwani ccm ndio imemuwezesha kufunga ndoa ughaibuni, kufanya fungate ughaibuni, kupata fedha za kupiga pamba kali yeye na mkewe, utakuwa juha kuacha kuwatetea waliokufadhili yote haya.
 
Hiyo Habari ya Dr hapo
juu vichwa vidogo vinajipinga !
Mimi bado Ntaendelea kuheshimu KAzi yake tu !

lakini siyo hiki kinacholetwaga kila wakati Na hiki kgaeti !

Ila Ufisadi Ujue una sura nyingi Dr Slaa !!
Mapambano ya kuleta
Mbadiliko ya Kifkra 'Kisera Kisheria yawe mfumo rasmi ndani ya Taifa leo yanaendea !

Kama sio Mimi Mtoto
atamalizia , mjukuu wangu hadi kieleweke!

Lakini ndani ya Ccm
Sahau !!
Hakuna MTU hata mmoja anayeweza akiwa kule !!!

zaidi kutipia majipu !!

mpaka sasa wameshashindwa mwaka bado !

Hakuna kulala
 
Atueleza kwanza anaishi Ulaya kwa gharama ya nani?Je, anaishi huko kwa support ya ule mzigo aliopewa Afrika kusini?
Ungeanza kudiscuss alichoongea na sio maisha yake hayatuhusu, yule hakuwa mtumishi wa serikali maisha yake hayatuhusu siamini kama anatumia kodi yetu., maneno aliyoyasema unayaonaje? hilo ndo lina tija na mstakabali wa Taifa letu.
 
Dr. Slaa ni Mwanasiasa pekee Tanzania ambae aliweza kupambana na ufisadi kwa nia safi, ni kiongozi alieongelewa ufisadi bila unafiki, Ningependa sana Slaa aungane na Zitto ni wao tu hapa Tanzania wanaweza unda chama kinachopiga ufisadi bila ya wao hakunan wengine ninao waona wanapambana na ufisadi katika vyama vya upinzani.
 
Sitaki kukuamini kwani huyo slaa mwenyewe anajua kuwa ccm hakuna mtu safi? Alafu kama kweli ni mwanasiasa anayepinga ufisadi mbona ana support kazi ya magufuli wakati anajua kamrudisha wizarani fisadi wa escow? Hebu acheni kuongea vitu ambavyo hamvijui
 
Vipi ajazungumzia ya Zanzibar mwana siasa huyu anayejifanya mzalendo kwani aoni maelfu ya watanzania wenzake wamenyimwa haki yao ya msingi kupata Kiongozi waliyemchagua
 
Chadema inahitaji damu mpya. Kama si migogoro leo Zitto, Mnyika , Kafulila, Kitila Mkumbo , Msando , Tundu Lissu , Joshua Nassari , Makene, Ben Saanane n.k ndio wangekuwa machine za kuendesha harakati mpya kwa umoja wao .....Hawa vijana wamegawanywa na ma mentor wao , propaganda za CCM na mapungufu yao ya ubinafsi ....hiki kizazi kimepotea na sasa ipo kazi ya kujenga kizazi kipya kisicho na makandokando haya ....kwasasa hakuna Chama chenye njia bora ya kuibua vijana safi ....labda JPM afanye hivyo akipewa uenyekiti wa CCM ....
 
Atueleza kwanza anaishi Ulaya kwa gharama ya nani?Je, anaishi huko kwa support ya ule mzigo aliopewa Afrika kusini?
Usijitoe ufahamu...

Anza kwanza kumhoji mwana UKAWA mwenzenu Seif anaishi kwa gharama za nani pale hitelin
 
Sitaki kukuamini kwani huyo slaa mwenyewe anajua kuwa ccm hakuna mtu safi? Alafu kama kweli ni mwanasiasa anayepinga ufisadi mbona ana support kazi ya magufuli wakati anajua kamrudisha wizarani fisadi wa escow? Hebu acheni kuongea vitu ambavyo hamvijui
Yes anajua kama baadhi ya wanachama wa CCM NI MAFISADI na alisimama Mwembe Yanga kutupa orodha ya mafisadi woote, Na sote tunawajua ila hapo HAKUSIFIA CCM KUWA NI WASAFI BALI AMESEMA WANAOMPIGA MAGUFULI NI MAFISADI, Kwahiyo kama uko CCM, uko C.U.F. au ART Wazalendo Mathali unampinga Magufuli basi wewe fisadi au mrija wako ushakatwa, MJEFUNZE KUSOMA NA KUELEWEA KABLA YA KUANZA KUKURUPUKA NA MACOMMENT YA KUMPONDA mtu, Halafu muache tabia ya kila jambo kuliongelea kisiasa, SASA HIVI HATUTAKI SIASA Na Ukawa mkiendelea hivyo 2020 tutawasahau sabab wananchi wanaona A unawalazimisha waone B Watawashtukia nakuwaona hamna nia njema kwao, mana mengi anayofanay Magufuli mlisema ni ilani yenu, lakin hapo hapo mnajisahau pia mnaponda, kuna hatari ya 2020 tukawasahau.
 
Back
Top Bottom