DR. SHEIN nani kakwambia kuwa ICC ina uwezo wa kuhoji uchaguzi?

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
Alichokisema Dr. Shein ni sahihi kabisa kua ICC haina uwezo wa kuhoji uchaguzi kwasababu ICC haishughuliki na mambo ya matokeo ya uchaguzi, ICC ni mahakama inayoshughulika na makosa ya kihalifu (human rights violation), sasa tumulize Dr. Shein Je na hili pia ICC hawana uwezo wa kumuhoji?

Inawezekana Dr. Shein kwasababu anajua kua kaingia madarakani kwa njia za wizi ndio maana kila anaposhtakiwa anadhani anashtakiwa kwa kosa la wizi tu na labda hajui kua CUF haikumshtaki yeye na wenzake kwasababu ya wizi bali wamemshtaki kwa vitendo vya uvunjifu wa haki za binadam walioufanya.

Sasa ni vyema Dr. Shein akatambua kwamba ICC haitomhoji kashindaje uchaguzi bali itamuhoji kwa nini amevunja haki za binadam? Kwa nini aliwaamrisha mazombi wakapige watu wasiokua na hatia? Haya ndio mambo wanayoshughulikia ICC.

Dr. Shein kudhani kua ICC itahoji uchaguzi ni hofu yake inayotokana na kushindwa kuamini kua atafika 2020 bila ya kufikwa na chochote ikiwemo hiyo kuhojiwa kwa uhalali wa serikali yake na ukweli ni kwamba Dr. Shein ameshahojiwa na ataendelea kuhojiwa mara kadhaa kuhusu uhalali wa serikali yake lakini kwa ICC Dr. Shein asijipange kujibu swali hilo bali ajipange kujibu kwa nini alivunja haki za binadam au na hilo alilifanya kwa mujibu wa katiba? Je katiba yetu imeruhusu uvunjaji wa haki za binadam?

Kujinasibu na kujigamba kwa Dr. Shein ni ishara inayoonyesha kushindwa na kuashiria kua bila ya shaka lipo jambo kwasababu kama maneno ya wapinzani ni uzushi na uongo kwa nini anapoteza mda kujibu hoja za kizushi si angewaacha viongozi hao wa upinzani wakadanganya watu wao yeye akaendelea na serikali yake tu?

Kibaya zaidi kinachoonekana kwa Dr. Shein ni kama vile hakuwahi kupita shule hata siku moja pamoja na udokta wake, mtu unapohoji na kudai kua mataifa ya nje hayawezi kukuondosha madarakani kwasababu ya sheria zako za ndani wakati umevunja sheria na makubaliano ya kimataifa hii inaonyesha ni kiasi gani kichwani hamna kitu.

Ivi Dr. Shein anadhani hao waliovamiwa na nchi za magharibi (western countries) wote walitaka kufanyiwa hivyo? Na je anadhani hao nao hawakua majabari na kusema kua hakuna anaeweza kuwaingilia katika mambo yao ya ndani? Nadhani Dr. Shein na CCM wenzake wangejifunza kuisoma dunia na siasa za ki-magharibi (international politics) ndipo halafu wakatoa jeuri.

Basi haya na mfano wa haya ndio utakayohojiwa na ICC kama unataka tukupe taarifa za ndani, sasa kama una la kujibu jiandae ila haya ni madogo tu makubwa utajionea mwenyeo.

The initial statement from one among the ICC lawyer said that told their colleagues during the meeting with Maalim Seif Sharif Hamad at the corridor bargain in ICC offices the lawyer said "During the registration period which ended in Unguja in April 2005, pro-CCM militia, nicknamed Janjaweed, in collaboration with security forces harassed people waiting to register, burnt and looted homes, beat people up and committed many random acts of violence with the intention of increasing insecurity and discouraging people from registering. In some cases, people were arrested and held until the registration exercise finished in their areas.

Between November 2004 and May 2005, the human rights abuses associated with registration were: Death 30, Serious Injuries 73, Rapes 1, Arrest without Charges 47, House Burnt 14, Business Properties BUrnt 2.

In addition to that CUF repeesentative and ICC lawyer have many things to add in human rights abuses in Tanzania/Zanzibar. For examples:
The Police arrested without charge and without explanation, the former CUF candidate for Donge in 2000, Hafidh Juma Ali.

At Fujoni Kiombamvua registration centre, the police officer in charge of the centre, ARCS for Mfenesini Station, known by as Maridadi, interfered in the registration process by forcing non-Zanzibaris (Mainlanders) to be registered by force and at one incident tore papers containing particulars that were being collected by a CUF agent at the center.

At all registration centres of Donge constituency, minors were registered. The exercise was forcefully supervised by Ali Juma Shamhuna then and later was Minister in Zanzibar Government. A police officer with number E 704 executed this plan by forcing the registration of minors at Donge Kipande and Donge mchangani centers which are both located within Donge Mwanda Primary School Centre. The exercise was also assisted by a Donge kindergarten teacher, Ms Riziki Abdullah Juma. Among the minors registered at this centre were two brothers, Makame Khamis Askari (12 years of age) and Bakari Khamis Bakari (14 years of age). The second of these is still in the PER as of November 1, 2005.

At Mahonda registration Centre, Donge constituency, the police officer in charge, Sergent Mohamed Khamis, (number Z 2009) hijacked the registration process by giving orders as to who should and should not register. He ordered all CUF members and supporters out of the centre after receiving instructions and directives from CCM members camping outside the centre.

Those CCM members giving such instructions from outside the ceentre were Samira Abdalla Mali, Asha Haji Suleiman, Ali Maabad, and Amour Ali Kidogo. At the same centre, minors were registered by force on the instructions of Police and the SHEHA. Among the minors registered were Maryam Chum Seif, Maryam Massoud, Rehema Massoud, Mboje Haji Silima, Mkasi Ali Vuai, and Khadija Hamad. At least two of them are registered in the PVR given to CUF after the elections on October 30.

Also, at Mahonda registration centre (Donge constituency) and Kilombero A and B registration centre (Kitope constituency), all people origin were prevented from registering even if they were born in the area or had been residents for more than 30 year.

Dr. Shein huko hutoenda kuhojiwa uchaguzi baba wala usijali ila narejea kukwambia kua haya ni madogo tu mengine tunayahifadhi.

Sisi CUF kwa sasa chetu kimya. Time will tell.

Written by
Abdalla Dadi.
 
Wa kwanza anayetakiwa kuitwa na ICC ni yule aliyahamasisha watu kuchoma Mikarafuu ya wasiomuunga mkono, kuchoma Boti na nyumba za wasiomuunga mkono na kumshabikia, kuwatisha wananchi wasitoke kumchagua wamtakaye kwa kuwawekea alama nyekundu kwenye makazi yao, aliyehamasisha wafanyabiashara wanachama na wapenzi wake wasihudumie wanachama na wapenzi wasio upande wake.
 
Endeleeni kujitekenya na kucheka wenyewe. Shein ndio Rais wa Zanzibar mpka 2020. cuf endeleeni kuwadanganya wale wapemba wasio na shule.
 
Hizi kesi za ICC nazo hua zinaenda kwa muda mrefu mpaka basi, yaani hadi leo walalamikaji bado wako kwenye mchakato wa kuitengeneza kesi tu. First hearing inaweza kufanywa Dr. akiwa kamaliza miaka yake 5.
 
Unaongelea vitu vingine vya 2004 na 2005.. unamhusishaje na vitu ambavyo vimefanyika na yeye hakuwepo?
 
Umemaliza vizuri....chenu kimya na time will telll n that time will tell ni kujiandaa na uchaguzi 2020 no otherwise.
 
Back
Top Bottom