figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,484
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduiz Dr Ali Mohmaed Shein amesema serikali
inaunga mkono matumizi ya mitandao ya kijamii na haina mpango wa kuyazuia ingawa mitandao hiyo iwe yenye kuleta faida na maendeleo kwa wananchi.
Dr Shein ametoa msimamo huo wakati akizungumza na wananchi na wadau wa sekta ya sheria nchini katika kilele cha siku ya sheria kwa Zanzibar, sherehe ziliozofanyika katika bustani za Victoria ambapo
amesema mitandao ina faida kubwa ingawa amesisitiza umuhimu wa kufuatwa kwa sheria za nchi pamoja na kuwepo kwa uhuru wa mwananchi kupata habari.
Mapema jaji mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu ameiomba serikali kuangalia mahakama kwa undani zaidi kuhusu bajeti kwa vile mahakama inakwama katika utekelezaji wake huku mwanasheria mkuu wa Zanzibar Said Hassan Mzee amesema sheria mpya za mitandao za Cyber Crime zilipitishwa na bunge sasa zinafanya kazi Zanzibar, naye katibu wa chama cha wanasheria Zanzibar Omar Said Shaabn alielza matatizo ya sheria za mitandao na utekelezaji wa sheria.
Sherehe hizo za siku ya sheria Zanzibar ambazo kauli mbiu ya mwaka huu ni matumizi mabaya ya mitandaio ya kijamii yanaweza kuwa chanzo cha uvunjani wa sheria na amani ya nchi.
Chanzo: ITV