Dr. Salim Ahmed Salim akutana na waandishi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Salim Ahmed Salim akutana na waandishi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Halisi, Oct 25, 2009.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Dr. Salim Ahmed Salim, amekutana na Waandishi wa habari nyumbani kwake Dar es Salaam, pamoja na kujibu maswali ya waandishi wa habari, alitoa taarifa ifuatayo.


  MKUTANO NA VYOMBO VYA HABARI

  JUMAPILI TAREHE 25. 10. 2009
  585 MSASANI, PENINSULA


  Mabibi na Mabwana.
  Habari za asubuhi
  Nawashukuru nyote kwa kuja kwenu.

  Mtakumbuka kuwa mapema mwaka huu, Bodi ya Taasisi ya Mo Ibrahim, ambayo mimi ni mjumbe mmoja wapo, ilitoa uamuzi wa kufanya sherehe za kutunuku Tuzo ya Mafanikio ya Uongozi Bora Barani Afrika, hapa Dar es Salaam.

  Kutokana na uamuzi wa Kamati ya Tuzo ya Mo Ibrahim mapema mwezi huu wa kutomtunukia yeyote Tuzo hiyo, hapatakuwa na sherehe ya kutoa Tuzo kama ilivyopangwa hapo awali. Hata hivyo, tumeamua kuitumia nafasi hii kutilia mkazo umuhimu wa Uongozi Bora barani Afrika. Kufuatia uamuzi huo, matukio muhimu mawili yameandaliwa. Tukio la kwanza litakalofanyika jioni tarehe 14 Novemba, 2009 ni la kiutamaduni ambalo, licha ya shughuli nyinginezo, watakaohudhuria wataweza kushuhudia michango ya wasanii mahiri kama Yossou N'Dour na Angelique Kidjo, tukio ambalo litatangazwa moja kwa moja katika radio na runinga mbalimbali barani Afrika. Sherehe hizo zitahudhuriwa na watu mashuhuri waliotoa mchango mkubwa kwa bara la Afrika pamoja na mamia ya watanzania na wageni mbali mbali kutoka pande zote za dunia.

  Aidha, tukio hilo litatoa kipaumbele kuhusu nafasi, majukumu na wajibu wa vijana barani Afrika hivi sasa na katika siku za usoni.

  Tukio la pili ambalo linazinduliwa kwa mara ya kwanza kabisa na Taasisi ya Mo Ibrahim, litakuwa ni Jukwaa (mbonge) ambalo litakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo Viongozi, Maofisa wakuu wa serikali, Wafanyabiashara, Wanaharakati, Wasomi, Wanafunzi na Vijana kutoka nchi mbali mbali barani Afrika, ili kujadiliana mada mbalimbali zinazohusu fursa na mambo muhimu ya maendeleo. Jukwaa litafanyika siku ya Jumapili, tarehe 15 Novemba 2009. Kimsingi, lengo la jukwaa hilo ni kujadili na kuweka bayana fikra na mtazamo wa pamoja wa jinsi ya kushughulikia masuala ya maendeleo kwa siku za usoni.

  Jukwaa hilo litakuwa na Mada kuu Tatu zitakazojadiliwa katika vipindi vifuatavyo:

  Mjadala wa mada ya kwanza, utahusu Haki na Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani (Climate Change and Climate Justice). Mwenyekiti atakuwa Rais Mstaafu Festus Mogae wa Botswana. Rais Mogae ni Mtunikiwa wa Tuzo ya Taasisi ya Mo Ibrahim kwa mwaka 2008, na ni miongoni mwa wawakilishi wanne maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki-moon, kuhusiana na masuala ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa.

  Mjadala wa mada ya pili, utahusu Kilimo na Usalama wa Chakula (Agriculture and Food Security). Mwenyekiti wa mjadala huo atakuwa Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Bwana Kofi Annan. Bw. Annan ni Mwenyikiti wa Bodi ya Mshikamano wa Mapinduzi ya Kijani katika Afrika – AGRA.

  Mjadala wa mada ya tatu, utahusu Ushirikiano wa Kikanda wa Kiuchumi (Regional Economic Intergration) ambao Mwenyekiti wake ni Bwana Abdoulie Janneh. Bwana Janneh ni Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Uchumi ya Afrika ya Umoja wa Mataifa.

  Mkutano huu utakuwa ni Muhimu, utakaowaleta watu kutoka sehemu zote za Afrika. Wadau wote hawa wanakuja pamoja wakati ambapo kwa upande mmoja kuna maendeleo ya jumla katika bara la Afrika lakini kwa upande mwingine kuna vikwazo vya kutia wasiwasi katika baadhi ya nchi na hivyo kujenga umuhimu wa wadau na taasisi mbalimbali kukutana na kutafuta ufumbuzi na changamoto ambazo zinakabiliwa barani la Afrika. Kwa kufanya hivyo, tutaendeleza mjadala na mazungumzo kuhusu changamoto za msingi ambazo zinakabili bara la Afrika. Taasisi ya Mo Ibrahim inaamini kuwa ili kutoa mchango madhubuti katika juhudi za kuendeleza uongozi bora katika Afrika, taasisi haina budi kusaidia kufanikisha mijadala na mazungumzo mbalimbali yanoyohusu changamoto za msingi za muda mrefu zinazolikabili bara letu.

  Baada ya kueleza hayo, ninapenda kutoa ufafanuzi kuhusu kazi moja kubwa ya Taasisi ya Mo Ibrahim, kazi ambayo tunaiona kuwa muhimu zaidi kuliko Tuzo yenyewe. Kazi hiyo ni ile kazi ambayo tathmini yake huwa ni mojawapo ya vigezo muhimu katika uamuzi wa kupatikana kwa TUZO. Ninakusudia kueleza Vigezo vya Taasisi ya Mo Ibrahim kuhusu Uongozi Bora barani Afrika (Ibrahim Index on African Governance), chombo maridhawa katika juhudi za kuendeleza uongozi katika Afrika. Tarehe 5 Oktoba mwaka huu tulitangaza vigezo hivyo huko Cape Town, Afrika ya Kusini. Vigezo hivyo ni vipimo kamili vya kupimia usawa katika uongozi. Ni kipimo cha uongozi bora ambacho hutoa taarifa na kuwawezesha wananchi kuendesha serikali na taasisi zao kwa kuwajibika. Hivyo vigezo vilivyoandaliwa na Taasisi ya Mo Ibrahim ni pamoja na michango ya watafiti maarufu, taasisi, na ule mchango wa Kamati ya Ushauri ambayo inajumlisha Wasomi wa Afrika na Watafiti. Vinalenga kuchachua mjadala kwa njia makini inayoweka misingi imara katika uongozi bora katika Afrika.

  Vigezo vya Taasisi ya Mo Ibrahim hupima pia kwa kiasi gani huduma zinawafikia wananchi kupitia serikali na asasi zisizo za serikali. Vigezo vya Mo Ibrahim vimezingatia misingi mikuu minne kama ifuatavyo:

  1.Usalama na Utawala wa Sheria
  2.Ushirikishaji na Haki za Binadamu
  3.Fursai na Uchumi Endelevu
  4.Maendeleo ya Watu

  Tathmini ya Taasisi ya Mo Ibarahim hupima utawala bora kwa kutumia vigezo 84 ambavyo hukusanywa kwa hali ya kutosheleza inayohusisha taarifa na takwimu (data) ambazo zinatathmini uongozi bora barani Afrika.
  Vigezo vinahusisha:

  • Usalama wa mtu Binafsi
  • Utoaji wa Elimu na Ubora wa Elimu yenyewe
  • Haki za Watu (Civil Liberties)
  • Ubora wa Miundombinu
  • Uhuru wa Mahakama
  Vigezo vimegawanywa tena katika sehemu ndogo ndogo (Sub-categories) kumi na tatu zikiwemo:-

  • Usalama wa mtu Binafsi
  • Utawala wa Sheria
  • Haki za Binadamu
  • (Usawa) wa Jinsia
  • Menejimenti ya Uchumi
  • Mazingira na Maendeleo ya Vijijini
  • Elimu
  Sasa ningependa kugusia suala la TUZO. Kama mnavyojua, Kamati ya Tuzo haikuweza kuteua mshindi mwaka huu. Kwa niaba ya Bodi ya Taasisi ya Mo Ibrahim, Rais mstaafu wa Botswana Ndugu Kitumire Masire alisoma tamko la Kamati ya Tuzo kama ifuatavyo:

  "Taasisi ya Mo Ibrahim iko mstari wa mbele kusaidia uongozi wa Afrika ili kusukuma mbele hali ya Uchumi na Ustawi wa jamii wa watu wa Afrika. Lengo la Taasisi ni kuendeleza na kuinua uongozi bora na kutambua umahiri katika uongozi wa Afrika. Kamati ya Tuzo inatambua maendelea yaliyofikiwa katika baadhi ya nchi za Afrika kuhusiana na uongozi bora na wakati huo huo kuzingatia matatizo yaliyopo katika baadhi ya nchi. Mwaka huu Kamati ya Tuzo iliwazingatia baadhi ya viongozi wenye sifa na kuheshimika (Credible) lakini baada ya kuzingatia kwa undani na umakini Kamati haikuweza kuchagua mshindi."

  Muundo wa Kamati ya Tuzo unajumlisha viongozi mashuhuri duniani ambao wanaamini kwa dhati kuisadia Afrika katika mapambano yake katika maeneo mbali mbali. Kamati hiyo ipo chini ya mwenyekiti aliyepokea Tuzo ya Amani ya Nobel, Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan. Wajumbe wengine wa Kamati hiyo ya Tuzo ni pamoja na Marti Ahtisaari, Rais Mstaafu wa Finland ambaye pia ni Mtunukiwa wa Tuzo ya Nobel, Mohamed El Baradei, ambaye ni Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki na Mtunukiwa wa Tuzo ya Nobel; Mary Robinson, Rais Mstaafu wa Ireland na Kamishna Mkuu wa zamani wa Umoja wa Matifa wa Haki za Binadamu; Aicha Bah Diallo, Waziri wa Elimu Mstaafu wa Guinea na Mkurugenzi Mkuu Msaidizi Mstaafu wa UNESCO pamoja na Mama Graca Machel, Kiongozi mashuhuri wa harakati za Haki na misaada ya kibinadamu na Mtetezi mkubwa wa Haki za Maendeleo ya Watoto.

  Mimi kama mmoja wapo wa wajumbe wa kamati hiyo ya TUZO, ningependa kusisitiza tu kuhusu maamuzi hayo na kauli iliyotolewa. Mtakapoanza kuuliza maswali ni vema niwajulisheni waziwazi kwamba sitajibu maswali yeyote yale kuhusu mwenendo wa majadiliano ya Kamati ya Tuzo. Kifungu cha 11 cha hadidu za rejea kinasema:

  "Majadiliano na viambatisho vyovyote vya Kamati ya Tuzo ni SIRI KUU. Mjumbe yeyote wa kamati ya TUZO haruhusiwi kutoa siri ya mwelekeo wa mazungumzo au matokeo ya kutofaulu kwa mtu yeyote yule na wakati wowote ule."

  Hata hivyo, kama mjumbe wa Bodi ya Taasisi, ningependa nitoe maono machache:
  Kwanza kabisa, Wajumbe wa kamati ya Tuzo huzingatia itikadi ya Tuzo na hufanya kazi kwa mujibu wa kanuni na miongozo iliyowekwa. Wanafanya hivyo kwa misingi ya uhuru, uaminifu na bila upendeleo. Pili, katika kumchagua mshindi, Bodi hutegemea kwamba Kamati ya Tuzo itatia maanani mambo kadhaa yakiwemo: Utendaji wa nchi kama ulivyopimwa kwa kutumia Vigezo vya Taasisi ya Mo Ibrahim pamoja na chambuzi nyingine zinazoheshimika na kukubalika. Viongozi wanaostahili ni watendaji wakuu wa nchi au Serikali waliostaafu, ambao wamepata madaraka kwa njia ya uchaguzi huru na halali na kustaafu katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita; baada ya kuitumikia nchi kwa mujibu wa Katiba kama ilivyoainishwa wakati alipochukua madaraka. Kwa mujibu wa maelezo haya, kipindi kinachozungumziwa hapa ni kile cha mwaka 2006, 2007 na 2008.

  Mabibi na Mabwana, Wanahabari,
  Sasa niko tayari kujibu maswali yenu.

  oooooooooooooooooooooooooooooooo

  English Version:

  Statement to the Media by Dr. Salim Ahmed Salim on the Events by Mo Ibrahim which will take place on 14 – 15 November, 2009 in Dar es Salaam
  At 585 Msasani Peninsula, Masaki, Dar es Salaam
  Sunday 25 October, 2009

  Ladies and Gentlemen: Good morning.
  Thank you for coming today.

  As you are aware, early this year, the Board of the Mo Ibrahim Foundation, of which I am a member, took a decision to hold the ceremony of awarding the Ibrahim Prize for Achievement in African Leadership here in Dar es Salaam.

  Given that the Prize Committee took a decision earlier this month not to award the Ibrahim Prize this year, we will not be holding a Prize ceremony as originally planned. We will nonetheless use the occasion to highlight the importance of governance in our continent. In this connection, two major events will take place; the first is a cultural celebration in the evening of Saturday 14 November that will feature contributions from African icons such as Youssou N'Dour and Angelique Kidjo. Broadcast live across Africa, this event will be attended by many of Africa's finest daughters and sons. The event will also highlight the important role that young Africans are playing and will play in the future of our continent. Let me just mention that this particular event will proceed as originally planned with invited guests from different parts of the world as well as Tanzanians.

  The second event is an exciting new initiative of the Mo Ibrahim Foundation which will be launched for the first time in Dar es Salaam. On November 15, the Foundation has organised a forum in which African stakeholders will gather to discuss key issues and opportunities for progress. The aim of the forum is to articulate shared aspirations and a common vision for the future around these issues.

  The forum will consist of three consecutive sessions:

  First, Climate change and climate justice chaired by Former President Festus Mogae of Botswana. President Mogae, who is a laureate of the Mo Ibrahim Prize is one of United Nations Secretary-General, Ban Ki-moon's four special envoys on climate change.

  Second, Agriculture and food security, chaired by the former Secretary General of the United Nations Mr. Kofi Annan. Mr Annan is Chairman of the Board of the Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA).

  Third, Regional Economic Integration, chaired by Mr. Abdoulie Janneh. Mr Abdoulie Janneh is the Executive Secretary of the United Nations Economic Commission for Africa.

  This will be an important gathering of people from all over the continent. At a time when, despite overall progress in Africa, we are seeing worrying setbacks in some countries, it is vital that African stakeholders and institutions come together to look for a way forward in some of the major challenges facing the African continent. If we can help foster debate and dialogue on the key long term challenges facing the continent, the Foundation will have contributed a great deal to furthering good governance in Africa.

  At this juncture let me outline one other major activity of the Foundation: work which we consider to be even more important than the Prize and whose evaluation is one of the significant inputs in determining the winner of the Prize, I am, of course, referring to the Ibrahim index of African Governance, a very important tool in the efforts to improve governance across the continent. On 5 October this year we launched the Index in Cape Town, South Africa. The Index is a comprehensive ranking of African countries according to governance quality. It aims to be Africa's leading assessment of governance that informs and empowers citizens to hold their governments and public institutions to account. Thus the Index which is prepared by the Mo Ibrahim Foundation with input of able researchers and various institutions and effectively assisted by an Advisory Committee comprising of mostly African academics and researchers aims to stimulate debate in a constructive way and establish a framework for good governance in Africa.

  The Ibrahim Index measures the delivery of public goods and services to citizens by government and non-state actors. The Ibrahim Index uses indicators across four main pillars:

  1.Safety and Rule of Law
  2.Participation and Human Rights
  3.Sustainable Economic Opportunity
  4.Human Development

  The Ibrahim Index assesses governance against 84 criteria, making it the most comprehensive collection of qualitative and quantitative data that measures governance in Africa.
  Criteria include:

  • Personal Safety
  • Education Provision and Quality
  • Civil Liberties
  • Quality of Infrastructure
  • Judicial Independence
  The criteria are divided into four main categories and 13 sub-categories which include:

  • Personal Safety
  • Rule of Law
  • Rights
  • Gender
  • Economic Management
  • Environment and the Rural Sector
  • Education
  Now let me turn to the issue of the Prize. As you know, the Prize Committee decided not to award the Ibrahim Prize this year. President Masire on behalf of the Board read out the statement of the Prize Committee which reads as follows:

  "The Mo Ibrahim Foundation is committed to supporting great African leadership that will improve the economic and social prospects of the people of Africa. The Foundation's focus is the promotion of good governance in Africa and the recognition of excellence in African leadership. The Prize Committee noted the progress made on governance in some African countries while noting with concern recent setbacks in other countries. This year the Prize Committee has considered some credible candidates. However, after in-depth review, the Prize Committee could not select a winner."

  The Prize Committee is composed of several eminent personalities of world stature who have one thing in common as far as Africa is concerned. They are firmly committed to supporting Africa's struggle in all its forms and manifestation. Chaired by the former Secretary General of the united Nations and Nobel Peace laureate, Kofi Annan, the committee's membership include: Marti Ahtisaari, former President of Finland and Nobel Peace laureate, Mohamed El Baradei, currently Head of the International Atomic Energy Agency and Nobel Peace Laureate, Mary Robinson, former President of Ireland and High Commissioner for Human Rights and Aicha Bah Diallo, former Minister of Education of Guinea and former assistant Director General of UNESCO and Graca Machel, a leading voice on Humanitarian Issues and a strong promoter of the Rights and Welfare of the Children.

  As a member of the Prize Committee, I can only reiterate the Statement that was made. When you start raising questions, let me at the outset make it clear that I will not be able to answer any questions about the deliberations of the Prize Committee. Clause 11 of its terms of reference state that:

  "The deliberations and supporting materials of the prize Committee are totally confidential. No member of the Prize Committee will reveal the thrust or details of deliberations, or the fate unsuccessful candidates, at any time."

  However, as a member of the Board let me make a few observations: First, members of the Prize Committee ascribe to the values of the Prize and operate on the basis of clearly laid guidelines. They do so on the basis of independence, integrity and lack of conflict of interest. Secondly, in selecting a winner, the Board expects the Prize Committee to take several factors into account. These include (but not exclusive) the performance of countries as assessed by the Ibrahim Index and other analysis of repute. Eligible candidates are former executive heads of state or government who have taken office through proper elections and who have left office in the previous three years, having served the constitutional term as stipulated when taking office. Thus in this particular case, the period concerned was 2006, 2007 and 2008.

  Ladies and Gentlemen of the Media,
  I will now be pleased to take up your questions
   
 2. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  kwa maana nyingine kikwete sio kiongozi bora
   
 3. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,081
  Likes Received: 1,728
  Trophy Points: 280
  YES DR SaLIM
  bUT WHaT MaDE YOU FaIL TO ELEVaTE MWaLIMU nYERERE TO aT LEaST a REGIOnaL LEVEL?
  MO IbRaHIM FOUnDaTIOn? FInE WHY nOT EXPLaInInG THE InDERCURREnT bEHInD THE FaILURES OF MnF?
  nI HaYO TU KWa LEO
   
 4. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kikwete si "KIONGOZI MSTAAFU", na Mkapa amepitwa na wakati baada ya kuzidiwa na Chissano 2007.

   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Oct 25, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kusema tunayajua sana... salimA salim alitakiwa kufanya haya alipokuwa Nyerere Foundation. Ingekuwa faraja gani kama Nyerere Foundation ingekuwa na sauti na nguvu kama foundation hii..
  Kifupi viongozi wetu wengi sii wabunifu hadi mtu mwingine afanye kitu wao wazuri sana wa kusema.. viongozi hawa huitwa Mtajidomo, hawana tofauti na wasanii Waimbaji..
   
 6. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,400
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  Unasahau kuwa kwa Mo Ibrahim kuna Mapesa Mengi?
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Oct 25, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Interesting Observer,
  Mo katengenezwa na hao hao viongozi lakini msingi wa Utajiri wake ni Ubunifu. Mtu kama huyu ndiye anatakiwa kuwa kiongozi wa nchi na sii watu wanaofuata misahafu kama uongozi wa dini. Ni mtu ambaye unaweza sema kasoma.. yaani ELIMU yake imeweza kufanya kazi ktk mfumo huu wa Utandawazi na bado anaendeleo kujipanua.
  Kifupi, umuhimu wa Mo Foundation ni ile Idea ya kuwatunuku viongozi bora jambo ambalo hata salim angeweza kabisa kulifanya.. michango na sponsorship ndio inayoendesha Mo Foundation huyu jamaa hatumii ndululu toka mfukoni mwake zaidi ya kutuweka sawa..
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mkandara,
  Kwa hakika kinachofanywa na taasisi ya Mo Ibrahim kingeweza kufanywa vizuri tu na Nyerere Foundation. Lakini kama alivyosema IO Mo ana hela. Hata ukiangalia kundi la viongozi wote walio kwenye kamati ya tuzo ni viongozi ambao walikuwa na uhusiano mzuri na Mwalimu Nyerere, na Mo Ibrahim anaweza kuwa na hela lakini sidhani jina lake linabeba uzito wa jina la Julius Nyerere.
   
 9. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,758
  Trophy Points: 280
  wakuu mimi nadhani mnayoyaongea humu yana ukweli lakini nadhani kuna kitu kimoja tunasahau. Mwalimu Nyerere Foundation haiwezi kufanya jambo la maana kwa sababu inaendeshwa kama taasisi ya kisiasa zaidi. Inategemea ionewe huruma na kupewa pesa simply because jina lake liko associated na Mwalimu. Hebu jiulizeni tangu ile taasisi ianzishwe inaendeshwa na Butiku..almost miaka kumi baada ya kuanzishwa..a retired man..ambaye sina uhakika hata kama aliwahi kuhudhuria darasa la management maishani mwake! Kifupi ile taasisi haina strategy yoyote zaidi ya kutaka kunufaika kwa kutumia jina la Nyerere. Na katika hali ya uhalisia, ni vigumu hilo jambo likafanikiwa.

  Sasa tofautisha na taasisi kama ya Mandela Foundation. Inaendeshwa na watu walio smart walio katika hiyo fani. Kinachofanyika...kunakuwa na board of trustees na wengineo ambao kazi yao ni kufanya fundraising na kuisadia secretariat inayoendesha day today activities za Foudation. I can assure you, ukiwa na Director ambaye yuko ontop of his game..MNF inapotential kubwa ya kuraise pesa...Salim can only do as much as the Secreatriat wants him to.

  Kinachotakiwa kufanyika: Butiku aachie ngazi..waajiriwe watu wenye utaalamu wa management na shughuli kama hizo za kuendesha taasisi. Ni vigumu mtu kama Butiku kukaa chini na kuweka strategies za kutafuta pesa..He simply cant! MNF ina potential ya kuwa taasisi makini sana ikipata waendeshaji makini ambao wako accountable kwa board iliyo makini. Watu kama wakina SALIM mnawaonea tuu..wale the best they can do ni kuwa Goodwill Ambassadors kuisaidia taasisi ile ipewe michango..lakini ideas inabidi ziletwe na waendeshaji. Unfortunately, there you have Butiku!

  In all, Mwalimu Nyerere Foundation cant do much, in the current way it does business. Nadhani ndo maana hata serikali inawa-ignore. Honestly, even if it were me, siwezi poteza resources zangu kwa taasisi inayoendeshwa na retiree kama Butiku ambaye..the best he can bring on the table..ni kwamba alifanya kazi na Mwalimu. Hivi..hawajifunzi kwenye Foundations nyingine kama Clinton, Mandela nk..zinavyoendeshwa?

  I just get fed up...maana vitu kama hivi..hutafundishwa darasani! Sadly, watu wanautumia il taasisi kama personal project. Yet taasisi kama ile ingeweza kuwa the best in its own right. It just needs right people. And Butiku isnt.

  Masanja,
   
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Oct 25, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Jasusi,
  Mkuu bado watu hawajamwelewa Mo Ibrahim.. Huyu ni msomi mbunifu na above all Mfanyabiashara.
  Ebu soma maelezo kisha chukua juice yako ukae karibu na TV kuyatafakari..
  The Mo Ibrahim Foundation believes that one of the best ways to channel its resources is to strengthen great African leadership by recognising and celebrating the individuals who play such a critical role in determining the future of their countries. Considering that in 2008 alone, aid to sub-Saharan Africa from G7 countries totalled just over an estimated US$25 billion, the Foundation believes that the money it is contributing through the .Ibrahim Prize is a comparatively small investment But given to an individual with a proven ability to contribute to Africa the money has the potential for very significant returns.
  The prize money is designed to work in conjunction with billions of dollars of development spending, foreign investment and national resources. If a country is well governed this means there will be a significant increase in the effectiveness and impact of all funds in the country.

  Halafu basi ukisoma homepage yao utagundua kwamba, hakika Nyerere Foundation inaonyesha kuchukua njia ndefu na isiyo na maana zaidi kwani huwezi kufikia maazimio ya Nyerere Foundation pasipo mikakati sawa na ya Mo Foundation
   
 11. E

  Eddie JF-Expert Member

  #11
  Oct 25, 2009
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 516
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Masanja,

  u have said it all, huyu mzee Butiku hana jipya zaidi ya stereo type zake za "enzi za Mwalimu" and the biggest item in his CV ni hiyo kufanya kazi na Mwalimu.

  Juhudi zake na za vikongwe wenzio kuigeuza MNF kuwa ya kisiasa za kum groom SAS kuwa rais zimeangukia poa na ndio maana kabaki na visasi.

  No one is taking MNF serious because of these vidingi na elimu zao kiduchu, zinaipeleka taasisi kaburini. Its time huyu mzee apumzike awaachie kijiti watu wenye uwezo.
   
 12. p

  p53 JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Huyu mzee angetangaza kugombea urais 2010 ningemuona wa maana sana
  Hizo nyingine blabla.com hazina tija yoyote
   
 13. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Taasisi ya Mwalimu Nyerere ipo kwa kuwa inabeba jina la Mwalimu Nyerere. Kama isingekuwa na jina hili na kama isingeanzishwa na Mwalimu Nyerere siku nyingi ingefutwa. Inashindwa kufanya kazi vizuri kwa kuwa inapingana na mengi yanayoendelea sasa hapa Tanzania, na ni kama mwiba kwa baadhi ya watu serikalini.

  Butiku, Salim na wengine wengi hawawezi kuiendeleza MNF kwa kuwa wao wenyewe wanaonekana kama ni maadui, wanakumbana na vikwazo kila kukicha kwa kusimamia yanayotakiwa kusimamiwa na kwa kukemea yanayotakiwa kukemewa.

  Siasa za ubaguzi wa rangi ni kikwazo kikubwa sana kwa Salim, lakini ideas zake na uzalendo wake kwa Tanzania haviwezi kuwa questioned.
   
 14. Z

  Zungu Pule JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 2,139
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Ninadhani sasa ni wakati wa kuipitia tena article aliyoandika Prof. Shivji, wakati hii tuzo ya Mo inaanzishwa. The article title was The Mo Ibrahim Prize: Robbing Peter to pay Paul and appeared for the first time in The Citizen. Follow the link http://www.pambazuka.org/en/category/features/44153
   
 15. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #15
  Nov 1, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,081
  Likes Received: 1,728
  Trophy Points: 280
  Nadhani tunatakiwa kurejerea kuwa mwenyekiti wa sasa wa MNF ni Dr. Salim A Salim! Nastahili kubeba zigo la failures za MNF pia! Wajumbe wa Bodi ya MNF ni pamoja na Kate Kamba, Joseph Sinde Warioba, Nimrod Mukono na wengine. Zigo la matatizo ya MNF asibebe Mzee Butiku peke yake ati!
   
Loading...