Dr Rashid aliifufua Tanesco au aliizika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Rashid aliifufua Tanesco au aliizika?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zak Malang, Jun 5, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Dr Rashid aliifufua Tanesco au aliizika?  Tafakuri na Na Mbasha Asenga, Mwanahalisi

  MIONGONI mwa mambo ambayo serikali ya Awamu ta Tatu inakumbukwa ni kutumia Askari wa Kutuliza Ghasia (FFU) kuwaingiza katika ofisi za Shirika la Umeme (Tanesco), watendaji wa kampuni ya Net Group Solutions (Pty) ambayo ilipewa mkataba wa kimenejimenti kuendesha shirika hilo pekee la kuzalisha na kusambaza nishati ya umeme nchini.

  Kwa wengi, walioshuhudia sekeseke lile, hadi leo wanaona kwamba kitendo cha kutumia FFU kuwaingiza ofisini watendaji wakuu waliotarajiwa kushirikiana na wafanyakazi wa Tanesco kubadilisha hali ya kudorora kwa utendaji wa shirika hilo, ni ubabe uliokosa sura ya kibinadamu wala hisia za baadaye juu ya mahusiano ya kikazi baina ya makundi hayo mawili, yaani mabosi wapya na wafanyakazi.

  Hata hivyo, pamoja na dosari hiyo, Net Group Solutions waliingia kwa mkwara mzito Tanesco. Mbali ya kusindikizwa na FFU, wakati huo, mkuu wa nchi naye alikuwa na mkwara wake kwa wafanyakazi.

  Aliwaambia kama wanataka kugoma waendelee kugoma lakini kitendo cha kumzuia mwenye mali kufanya kazi zake, kwa maana ya serikali, si kitendo ambacho kinakubalika wala kuvumiliwa.

  Kwa wale wanaokumbuka, wafanyakazi wa Tanesco walikuwa wamegoma katakata kuruhusu uongozi wowote mpya kuingia shirikani hapo bila kwanza serikali na wao kusaini mkataba wa hali bora ya kazini, ambao pamoja na mambo mengine, ungeainisha haki zao za mafao wakati wa kubinafsishwa kwa shirika hilo kwani mwelekeo uliokuwapo wakati huo ni kuibinafsisha Tanesco.

  Hata hivyo, muda si mrefu wafanyakazi wale wale waliokuwa wanawapinga Net Group Solutions walianza kuwafurahia baada ya kuona kuthubutu kwao; waliona walivyothubutu kuendesha operesheni ya kukusanya madeni ambayo iliwafikisha hadi kwenye ofisi nyeti za umma; jeshini. Hata ikulu ilitishiwa kukatiwa umeme, ila bahati nzuri ililipa deni lake kwa wakati.

  Kwa muda wote, Net Group Solutions walipokuwa wanaendesha Tanesco, walipongezwa na kupewa kila aina ya msaada waliohitaji kutoka kwa ofisi namba moja ya nchi—ikulu—ili tu wafanikishe majukumu yao. Kila ofisi ya umma iliambiwa waziwazi kwamba ni lazima ilipie umeme inaotumia.

  Wakati operesheni hiyo imepamba moto, nilishangaa kuwakuta viongozi waandamizi wa jeshi wakikimbizana kwenye ofisi za Tanesco kulipia bili zao ambazo walikuwa wamelimbikiza miezi na miezi. Wengi hawakuamini walichokuwa wakiona kwamba kumbe hata serikali inaweza kulipa madeni yake ya umeme, na kwamba kumbe bajeti ya kulipia bili ya umeme ilikuwapo!

  Sasa swali likaulizwa, hivi ni kwa nini basi msaada waliopewa Net Group Solutions hawakupewa Waswahili ili wakusanye fedha hizo na kulifanya shirika lijiendeshe vizuri na kwa faida pengine hata kuwa na uwezo wa kutekeleza wajibu wake wa kuzalisha umeme zaidi na kuusambaza maeneo mengi zaidi ya nchi hasa inapozingatiwa kwamba wakati huo ni kama asilimia nane tu ya Watanzania waliokuwa wanapata huduma hiyo?

  Baada ya muda, fungate ya Net Group Solutions na serikali ilipofikia tamati, hasa baada ya serikali ya Awamu ya Nne kuingia madarakani, kukawa na msukumo mpya wa kutaka Net Group Solutions waondoke na wakabidhi kazi kwa wazawa.

  Ni kweli wakafanya hivyo; ndipo aliibuliwa Gavana mstaafu Dk. Idris Rashid huko alikokuwa kuwa mkurugenzi mkuu mpya wa Tanesco.

  Watu wakasubiri waone mikiki yake, lakini kadri alivyojaribu kuiendesha Tanesco ikaonekana kama vile hana anayemuunga mkono.

  Ilifika wakati aliamua kujiuzulu baada ya kuagiza kiwanda cha sementi Tanga kikatiwe umeme kutokana na kulimbikizia deni. Lakini wakubwa wakataka umuzi wake utenguliwe, na kwa bahati mbaya waliokuwa wanamchimba alikuwamo Mwenyekiti wa Bodi.

  Tukiwa na maruweruwe ya Waswahili walivyofanywa pale Tanesco, wiki iliyopita mkurugenzi mkuu mpya ameibuliwa, huyu ni Mhandisi William Mhando, aliyekulia na kukomaa ndani ya Tanesco.

  Siku chache tu baada ya uteuzi wake, ametangaza operesheni ya kusanya madeni. Amesema Tanesco inawadai wateja wake kiasi cha Sh. 300 bilioni, kati ya hizo, Sh 58.5bilioni ziko mikononi mwa taasisi na idara za serikali wakati sekta binafsi wanadaiwa kiasi cha Sh. bilioni 241.5 hivi.

  Sasa swali linaibuka, je, ile operesheni waliyoanza nayo Net Group Solutions waliondoka nayo ndiyo maana leo hii miaka takribani minne baada ya kuondoka kwao habari za kuwapo kwa deni la bili lililofikia Sh bilioni 300 zinawekwa wazi?

  Pengine ni mapema kumpima Mhando ambaye amechukua nafasi ya Rashid ambaye tangu Novemba mwaka jana, alipomaliza muda wake, alijiengua Tanesco ikiwa ni pamoja na kukabidhi ofisi na hata nyumba aliyokuwa amepewa na shirika.

  Lakini kwa vyovyote itakavyokuwa, watendaji wa shirika hili, hasa kuanzia ngazi ya mameneja, hawawezi kujivua lawama juu ya mrundikano wa bili hisi hadi kufikia Sh bilioni 300.

  Wanasema nini juu ya mrundikano huu, wakati kila siku iendayo kwa Mungu kilio cha Tanesco ni kutokuwa na uwezo wa kifedha kutimiza majukumu yake kama ilivyokusudiwa?

  Hivi Tanesco wanakuwa na ujasiri gani basi wa kuingiza taifa hili katika dunia ya ushindani hasa kwenye soko la kila kitu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kama haiwezi kukusanya hata madeni yake makubwa kama haya ya kiasi cha Sh. bilioni 300, asilimia kubwa yakiwa ni kutoka makampuni binafsi ambayo huwezi kusema kwamba ni nyeti na yanalindwa na serikali?

  Mhando, juzi wakati anazungumza na waandishi wa habari hakusema wazi kwamba madeni hayo ni ya kuanzia lini mbali tu ya kusema kwamba ni ya miezi miwili na kuendelea.

  Swali linalozidi kuumiza kichwa ni kwamba hawa wakubwa wa Tanesco wanapata wapi ujasiri na utulivu wa mioyo na akili zao kama kweli kuna madeni makubwa kiasi hiki nje?

  Kuna mgogoro wa ndani kwa ndani Tanesco juu ya jinsi kiasi cha Sh. bilioni 300 zilizokopwa kutoka vyanzo vya ndani ya nchi katika kusaidia kufufua miundombinu ya shirika hilo ambayo kwenye baadhi ya maeneo nchini yanatia huzuni, kilivyotumika.

  Sh. bilioni 300 nje ni mtihani mkubwa na mwanzo wa maswali mengi Tanesco. Kama Tanesco inaweza kuendelea na shughuli zake huku Sh. 300 bilioni zikiwa nje, ni kwa nini basi watu wasiamini sababu mojawapo ya ughali wa umeme wake ni pamoja na kufidia uzembe kama huu wa kushindwa hata kukusanya kile walichouza?

  Si nia ya uchambuzi huu kumvua nguo Mhando, lakini itoshe tu kusema kwamba amethubutu walau kuonyesha ujasiri wa kutamka na kuanza ‘operesheni kusanya madeni na kata umeme’ kwa wadeni sugu.

  Lakini pia ni vema akakumbuka kwamba kabla ya kukalia kiti cha enzi alikuwa mmoja wa mabosi wa juu pia wa shirika hilo, akiwa meneja Mkuu Usambazaji Umeme na Masoko.

  Ni mfanyakazi ambaye aliajiriwa Tanesco tangu Oktoba mwaka 1987. Anaifahamu Tanesco chini ya wakurugenzi wakuu zaidi ya wanne. Je, anaweza kabisa kujivua lawama juu ya madeni haya?

  Mwisho kwa madeni haya makubwa kiasi hiki, hivi umma sasa uelezwe Dk. Idris Rashid, alikuwa anafanya nini Tanesco? Je, hawezi kushitakiwa kwa uzembe wa kushindwa kutimiza wajibu?

  Gazeti toleo na. 191
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hakufanya lolote la maana kwa sababu mgao bado uko pale pale na hakuna maendeleo yoyote yaliyopatikana ktk uzalishaji wa umeme.
   
 3. P

  Paul S.S Verified User

  #3
  Jun 5, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Tatizo maamuzi mengi ya tanesco yalikua yanafanywa kisiasa zaidi kuliko kitaaluma
   
 4. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hafai hata kuwa kiongozi wa mbio za mwenge! Ameizika TANESCO
   
 5. Sugar wa Ukweli

  Sugar wa Ukweli JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  No amejitahidi sana huyu bwana,kuna wakati ilifikia ukilipia service line ndani ya three weeks unajengewa,jambo hii hapo jnyuma ilikuwa ndoto!
   
Loading...