Dr. Pombe Magufuli, ashindwa kutokea kwenye Mdahalo wa Urais wa Tanzania

asakuta same

JF-Expert Member
Mar 1, 2011
14,829
5,030
Habari wanajamvii,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo tofauti na ccm kutamba kwenye media na social media kuhusu utayari wa mgombea wao kushiriki mdahalo utakaofanyika leo tarehe 18/10/2015, duru za kiuchunguzi zinazonesha hiyo ilikuwa ni danganya toto na propaganda za kisiasa.

Leo Magufuli anaendelea na ziara yake kanda ya ziwa na sasa hivi anaelekea kwenye mkutano wake wa kwanza kwa siku ya leo huko Misungwi.

Update :

Hatimaye Magufuli aukacha mdahalo rasmi pamoja na tambo za makada wa ccm kuonesha kuwa wapo tayari kwa Mdahalo.

Ni aibu kubwa sana kwa ccm, makamba na magufuli kwa kuwalaghai Watanzania.

Mnapaswa kutuomba radhi kwa kutudanganya na kumsema mgombea wa Urais wa ukawa.



-------------

Mgombea Urais wa CCM Dr.John Pombe Magufuli, ameshindwa kuhudhulia katika Mdahalo wa Marais wanaogombea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao Unaendelea Hivi sasa.

Hapo mwanzo alitoa taarifa kwamba atashiriki, lakini dakika 45 kabla ya kuanza mdahalo, ametoa taarifa kwa waandaaji kwamba hatahudhulia, hali ambayo imepokelewa kwa hisia tofauti.

Hadi sasa Wagombea urais waliohudhulia ni wawili tu ambao ni Mgombea wa ADC Chief Lutasola Yemba, Mgombea wa ACT Wazalendo Mama Anna Mghwira huku akisubiriwa mgombea wa CHAUMA Hashim Rungwe ambaye amesema yupo airport anakuja kwenye mdahalo.

Kwa yanayojiri katika mdahalo huo fuatilia hapa => https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ahalo-wa-wagombea-urais-oktoba-18-2015-a.html
 
Magufuli hana cha kuwaambia Watanzania zaidi ya hadaa zilezile za ccm ileile. Kastuka
 
Kila kitu Magufuli aiga UKAWA, kwanini? Mpaka Lowassa kutoshiriki mdahalo. Sera yake moja tu ambayo kabuni[hajaiga] ni kupiga push up.
 
anaogopa kuulizwa atapata wapi meli mbili mpya, wakati mentor wake kashindwa. tilioni zaidi ya mia atazitoa wapi kutimiza vague promises zake.

kufikiri kwa kiwango cha push up kutalicost taifa
 
Mgombea Urais wa CCM Dr.John Pombe Magufuli, ameshindwa kuhudhulia katika Mdahalo wa Marais wanaogombea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao Unaendelea Hivi sasa.

Hapo mwanzo alitoa taarifa kwamba atashiriki, lakini dakika 12:40, ametoa taarifa kwa waandaaji kwamba hatahudhuria, hali ambayo imepokelewa kwa hisia tofauti.

Hadi sasa Wagombea urais waliohudhulia ni wawili tu ambao ni Mgombea wa ADC Chief Lutasola Yemba, Mgombea wa ACT Wazalendo Mama Anna Mghwira huku akisubiriwa mgombea wa CHAUMA Hashim Rungwe ambaye amesema yupo airport anakuja kwenye mdahalo.

Hii sio picha nzuri kwa wagombea wetu. Ni aibu Mdahalo wa Marais kukudhuliwa na Marais wawili tu kati ya Marais wanane.
 
Kwa mujibu wa TWAWEZA, Magufuli katoa taarifa za kutoshiriki mdahalo saa 6 mchana wa leo!
 
Wakuu
Kila linalofanywa na mgombea wa urais wa cdm naye magufuli mgombea wa ccm naye anafanya,ni juzi ccm wamesema watahudhuria kwenye mdahalo lakini kwa taarifa zilizotolewa na maria sarungi zinasema mgombea wa ccm naye hatahudhuria,wadau mnasemaje kuhusu hili
 
Naanza kufikiri upya juu ya kura yangu kwenu!
Nimekuwa nawapigia debe toka kampeni zimeanza, lkn kwa kukwepa mdahalo leo, mmeenda chini kama ukawa!
Siwezi kuwapigia ukawa, lkn nitakuwa kimya kwa uchungu kuona kuwa nanyi mmejaa ubabaishaji tu! Vyama hivi vviwili vya ccm na chadema nadhani mnatarget Mama lishe na bodaboda pekee!
Watanzania wenye uelewa wa kutosha tunataka kumpima Magufuli akiwa hajakariri, tunataka kujua visions zake mwenyewe na mipango yake na sio mashairi ya kwenye majukwaa!
Mungu ibariki Tanzania, ipate chama imara mbadala wa ccm!
Nahisi ACT wanaweza kuhusika sana baada ya uchaguzi huu!
 
Ccm ni waongo miaka yotee...ndo muone kama ameshindwa kutimiza ahadi ya siku moja atawezaje kutimiza ahadi ya miaka 5...???
 
Binafsi nasikitika kwa kukosa kuwahoji wagombea ambao wanaonekana wana wafuasi wengi!. Hakuna mwenye afadhali...
Inaleta mantiki kwa Magufuli kutohudhuria kwani alitaka wapimane pumzi na Lowassa.
 
Back
Top Bottom